Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

George Betram

George Betram

JF-Expert Member
3,147
2,000
Wakongwe,

Kuna ndugu yangu ameanza mradi wa ufugaji kuku wa kisasa miezi kadhaa iliyopita. Ila changamoto anayopata ni katika kupata masoko, aliingia kwenye ufugaji bila kufanya utafiti wa masoko.

Kwa wenye kufahamu namna anaweza kupata masoko naomba mtusaidie.
 
cadey

cadey

JF-Expert Member
1,389
2,000
Kuna mtu kanunua silverlands na bdo analalamika hawakui na wanakula sana.
Cha muhimu hata hizo za mtaani mi ninazo na sasahv ndo nafuga kibiashara maana mwanzo nilifuga kwa matumizi yangu tu. Kuku we mpe chanjo zote na kuna ugonjwa mmoja mbaya sana unaitwa coccidiosis unakuwa unawapa dawa tu ukiona choo cha ugoro au dalili ya damu.

Vinginevyo hamna changamoto yoyote mwaka jana mwishoni niliuza kuku 160.
Sahv nina kuku 270 tayari kwa pasaka...maisha ni kudhubutu maana mwanzoni niliona hawana faida ila nikitoa gharama ya ulishaji faida naiona.

Pumba tani 1 nanunua kwa laki 3. Then mahindi,mashudu,uduvi au dagaa,mifupa na chumvi. Chakula cha kununua cha ready made ni gharama sana maana kuroiler wanakula balaaa hadi usiku kama ukiwasha taa wao ni kula tu hawajui kingine.

Jaribu huwezi jua bahati yako iko wapi mana kila mtu na mkono wake. Kuna mwingine biashara ya kuku anaona hailipi,mwingine biashara ya gari hataki kusikia kabisa,mwingine kilimo anaona hakilipi ila kwa waliotoboa kupitia hivyo vitu ina mana walijaribu bila kuangalia hasara kwa awali

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuku wako unawauzia wapi?
 
MANI

MANI

Platinum Member
7,261
2,000
Nadhani Toleo la sasa sio zuri ni kweli Ukuaji wao sio mzuri
Kuna mtu kanunua silverlands na bdo analalamika hawakui na wanakula sana.

Cha muhimu hata hizo za mtaani mi ninazo na sasahv ndo nafuga kibiashara maana mwanzo nilifuga kwa matumizi yangu tu Kuku we mpe chanjo zote na kuna ugonjwa mmoja mbaya sana unaitwa coccidiosis unakuwa unawapa dawa tu ukiona choo cha ugoro au dalili ya damu.

Vinginevyo hamna changamoto yoyote mwaka jana mwishoni niliuza kuku 160. Sahv nina kuku 270 tayari kwa pasaka, maisha ni kudhubutu maana mwanzoni niliona hawana faida ila nikitoa gharama ya ulishaji faida naiona.

Pumba tani 1 nanunua kwa laki 3. Then mahindi,mashudu,uduvi au dagaa,mifupa na chumvi. Chakula cha kununua cha ready made ni gharama sana maana kuroiler wanakula balaaa hadi usiku kama ukiwasha taa wao ni kula tu hawajui kingine.

Jaribu huwezi jua bahati yako iko wapi mana kila mtu na mkono wake. Kuna mwingine biashara ya kuku anaona hailipi,mwingine biashara ya gari hataki kusikia kabisa,mwingine kilimo anaona hakilipi ila kwa waliotoboa kupitia hivyo vitu ina mana walijaribu bila kuangalia hasara kwa awali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Renatus Edward

Renatus Edward

Member
46
125
Swali la kutaka kufahamu, wife ameanza project ya kuku, anafuga kuku aina ya Sasso wanaendelea vizuri lakini changamoto ya hawa kuku unakuta kuku wako wazima lakin ghafla tu ukienda bandani kuwaangalia unakuta mmoja wapo amekufa, mpaka sasa hii hali imetokea mara mbili huwa ni sababu ya nini? Chanjo zote anazingatia na anawapatia mwenye kufahamu zaidi naomba kunielimisha.na vipi kuhusu kodi ya serikali kwenye kuku ikoje mfugaji anapofanya kuku wake kama biashara.
 
Herman0888

Herman0888

New Member
3
45
Mbali na chanjo mkeo inabidi azingatie vitu vifuatavyo; itamsaidia;usafi w banda; awe na special slippers za au viatu vya kuingilia kwenye banda la kuku, awape kuku maji y kutosha kw ushauri zaid kuku akifa usimtupe; mpeleke kw Dr w mifugo au muite Dr w mifugo am chungu ze il ajue nn 7bu y kifo ch uyo kuku!!
 
shabil magalla

shabil magalla

Member
8
45
Samahani wanaJF me ni muhitimu wa chuo fulani#kulingana na upepo nimefikilia kujiajili na nauna ufugaji utanifaa naombeni experience yenu juu ya ufugaji wa kuku WA kisasa au naweza Pata wapi dalasa ili nifuge kwa ufanisi mkubwa
 
okwonkwo II

okwonkwo II

Member
25
45
Habarini mabibi na mabwana.

Natafuta tender ya ku-supply vumbi la dagaa, kwa wafugaji/watengenezaji Wa chakula cha kuku.
Mwenye uhitaji 0789925300.
 
moshi norbert

moshi norbert

Member
14
45
Habari wa ndugu kwa wale wafugaji wa kuku wa nyama nafahamu katika kuandaa banda la kuku kwa ajiri ya kuingiza vifaranga n lazima pawepo na malanda na malanda mazuri hasa ambayo hayana mazala kwa kuku wako n malanda ya mpunga japo kwa hapa Dar n garama kidogo kwa roba moja ni 7000 ad 8000 mimi nawapa solution na unafuu kidogo wa haya malanda kwa roba moja utapata kwa 5000 na pia kadri unavyozid chukua tunaweza fanya biashara ya mali kauli na punguzo zaidi ya hapo tuwasiliane wana ndugu.
 

Forum statistics


Threads
1,424,514

Messages
35,065,616

Members
538,005
Top Bottom