Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,618
Kuna wapuuzi fulani wanalalamika Mbowe kugombea uenyekiti Chadema. Wanatoa sababu za kijinga kana kwamba Mbiwe kugombea Uenyekiti Chadema amevunja hata robo ya kipengele cha katiba ya Chadema iliyopitishwa na mkutano mkuu wa Chadema. Kwa msiojua, Mkutano Mkuu ndio wanachama wenyewe. Kwa maana hakuna eneo katika nchi hii lililokosa mwakilishi. Kwa maana hiyo wanachama WOTE wa CHADEMA walikubali mabadiliko ya katiba yanayompa MBOWE haki ya kugombea tena. Hata Msajili hana kikwazo cha Mbowe kugombea.
Wanaolia lia sana mitandaoni ni CCM wakifuatiwa kwa karibu sana na ACT. Tena ACT wa huku bara. Kwa CCM kulalamika sishangai na wala sio ishu. Wote tunajua namna Chama Dola kilivyojaribu kumdhoofisha Mbowe lakini lijamaa lipo imara! Wanaonichekesha ni ACT wakiongozwa na mpuuzi KIGOGO.
Huyu Kigogo ni sehemu ya Mradi wa Zitto Kabwe akifadhiliwa na CCM wenzie anaowatumikia.
Wamemchafua sana Mbowe lakini mpaka sasa ni kama wanapiga ngumi hewani. Chadema bado inazidi kuwa ngangari.
Maalim Seif atagombea tena Urais wa Zanzibar (Kama Mungu atamweka hai na mwenye nguvu) Sote tunatambua Seif ameanza kugombea Urais wa Zanzibar tangu 1995. Hajawahi kumwachia mtu mwingine yeyote nafasi hiyo. JE! nayo ni demokrasia? Kwamba Zanzibar hakuna mgombea yeyote wa Upinzani mwenye nguvu kama Seif? Na ACT wanataka kutuaminisha kuwa Seif ni Alfa na Omega Zanzibar?
Kujenga demokrasia ni mapambano na mbinu kali. Hamuwezi kusukuma mapambano hata na watu dhaifu kwa mgongo wa Demokrasia. Ndio maana hata hao CCM kwenye uchaguzi wao wa Mwenyekiti mwenyekiti hagombei na mtu. Mwenyekiti huenda kuthibitishwa tu. Na iwapo atatokea mtu kujaribu kutenganisha Urais na Uenyekiti wa Chama atakiona cha moto. Kwa nini? Kwa sababu wanataka kuwa na Mwenyekiti mwenye nguvu. Na Chadema wanahitaji Mwenyekiti mwenye nguvu. Mwenyekiti aliyethibitisha kwa macho na kwa ngozi na kwa pua kuwa ana nguvu. Hawahitaji kupeleka mtu akajaribishe tuone kama ana nguvu au la! Amewekwa Mashinji pale sote tunaona anavyopwaya!
Kwa maana hiyo, ACT na KIGOGO Company inayomilikiwa na ZITTO KABWE, Komeni kabisa kukisema Chadema vibaya katika huu uchaguzi kwa sababu na nyie mtafanya hivyo hivyo kwa Seif Zanzibar Mwakani.
Acheni Chadema wafanye yao na nawahakikishia, HAMTAKUWA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI kwa mbinu za kipumbavu hizi mnazozifanya.
Alamsiki!
Mzito.