Kwa vyovyote vile Maalim Seif atagombea Urais Zanzibar. Je! Ni demokrasia?

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,614
Kuna wapuuzi fulani wanalalamika Mbowe kugombea uenyekiti Chadema. Wanatoa sababu za kijinga kana kwamba Mbiwe kugombea Uenyekiti Chadema amevunja hata robo ya kipengele cha katiba ya Chadema iliyopitishwa na mkutano mkuu wa Chadema. Kwa msiojua, Mkutano Mkuu ndio wanachama wenyewe. Kwa maana hakuna eneo katika nchi hii lililokosa mwakilishi. Kwa maana hiyo wanachama WOTE wa CHADEMA walikubali mabadiliko ya katiba yanayompa MBOWE haki ya kugombea tena. Hata Msajili hana kikwazo cha Mbowe kugombea.

Wanaolia lia sana mitandaoni ni CCM wakifuatiwa kwa karibu sana na ACT. Tena ACT wa huku bara. Kwa CCM kulalamika sishangai na wala sio ishu. Wote tunajua namna Chama Dola kilivyojaribu kumdhoofisha Mbowe lakini lijamaa lipo imara! Wanaonichekesha ni ACT wakiongozwa na mpuuzi KIGOGO.

Huyu Kigogo ni sehemu ya Mradi wa Zitto Kabwe akifadhiliwa na CCM wenzie anaowatumikia.

Wamemchafua sana Mbowe lakini mpaka sasa ni kama wanapiga ngumi hewani. Chadema bado inazidi kuwa ngangari.

Maalim Seif atagombea tena Urais wa Zanzibar (Kama Mungu atamweka hai na mwenye nguvu) Sote tunatambua Seif ameanza kugombea Urais wa Zanzibar tangu 1995. Hajawahi kumwachia mtu mwingine yeyote nafasi hiyo. JE! nayo ni demokrasia? Kwamba Zanzibar hakuna mgombea yeyote wa Upinzani mwenye nguvu kama Seif? Na ACT wanataka kutuaminisha kuwa Seif ni Alfa na Omega Zanzibar?

Kujenga demokrasia ni mapambano na mbinu kali. Hamuwezi kusukuma mapambano hata na watu dhaifu kwa mgongo wa Demokrasia. Ndio maana hata hao CCM kwenye uchaguzi wao wa Mwenyekiti mwenyekiti hagombei na mtu. Mwenyekiti huenda kuthibitishwa tu. Na iwapo atatokea mtu kujaribu kutenganisha Urais na Uenyekiti wa Chama atakiona cha moto. Kwa nini? Kwa sababu wanataka kuwa na Mwenyekiti mwenye nguvu. Na Chadema wanahitaji Mwenyekiti mwenye nguvu. Mwenyekiti aliyethibitisha kwa macho na kwa ngozi na kwa pua kuwa ana nguvu. Hawahitaji kupeleka mtu akajaribishe tuone kama ana nguvu au la! Amewekwa Mashinji pale sote tunaona anavyopwaya!

Kwa maana hiyo, ACT na KIGOGO Company inayomilikiwa na ZITTO KABWE, Komeni kabisa kukisema Chadema vibaya katika huu uchaguzi kwa sababu na nyie mtafanya hivyo hivyo kwa Seif Zanzibar Mwakani.

Acheni Chadema wafanye yao na nawahakikishia, HAMTAKUWA CHAMA KIKUU CHA UPINZANI kwa mbinu za kipumbavu hizi mnazozifanya.

Alamsiki!

Mzito.
 
Tunafaidikaje sie wananchi kwa Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti?
 
Huyo Kigogo nimemdharau kweli, kumbe ni jamaa fulani asiejielewa yupoyupo tu, kama popo!, ni kama robot fulani, anatumiwa na kiongozi fulani wa upinzani mwenye muonekano na matendo ya ki_opportunistic, siku zote haaminiki na kauli zake!, na bahati nzuri alishawahi kusema tusiwaamini wanasiasa ni waongo, kwangu mimi yeye ndie muongo namba moja.

Kigogo my friend you should know where to hit and how, sio una hit everywhere, kwasababu ya chuki zako binafsi, wajanja watakudharau!
 
Marehemu Mwalimu JKN alikuwa mwenyewekiti wa TANU/CCM kwa muda gani??

Jibu la swali hili litanisaidia kujenga hoja.
 
Kwani unanufaikaje Magufuli anapokuwa Rais na wwkati huo huo mwenyekiti wa CCM?
Sina nachofaidika,ndiyo nashangaa watu kuacha kujadili masuala muhimu yenye kugusa masilahi yao na kuanza kujadili au kufurahia Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa chadema,tuseme ccm walitaka Mbowe asiwe mwenyekiti na hiyo ni kwa masilahi yao ila sielewi sie wananchi kushabikia Mbowe kuwa mwenyekiti na ccm kufeli kwa hilo tuna masilahi gani nako hapo?

Yani tumekuwa watu wakuchezeshwa ngoma za wanasiasa tunashabikia mambo tusiofaidika nayo tumegawanywa yani tupo tupo tu.
 
Acha uongo. Kamati Kuu haikupitisha kipengele cha nafasi ya mwenyekiti kutokua na ukomo. Kipengele hicho kiliondolewa kinyemela.

Lakini nawahakikishia baada ya uchaguzi wa 2020 huyu huyu mbowe mtamtupia mawe kwa kusema bora tungechagua akili mpya.
 
Huyohuyo jamaa unasema anamtumia ndo huyo huyo kigogo mwenyewe yaani anajitumia
Huyo Kigogo nimemdharau kweli, kumbe ni jamaa fulani asiejielewa yupoyupo tu, kama popo!, ni kama robot fulani, anatumiwa na kiongozi fulani wa upinzani mwenye muonekano na matendo ya ki_opportunistic, siku zote haaminiki na kauli zake!, na bahati nzuri alishawahi kusema tusiwaamini wanasiasa ni waongo, kwangu mimi yeye ndie muongo namba moja.

Kigogo my friend you should know where to hit and how, sio una hit everywhere, kwasababu ya chuki zako binafsi, wajanja watakudharau!
 
Ni jamaa hata ukimwangalia huwezi amini kama ndo yeye mi hua namwambiaga "siku watakukamata hatutakuona tena"basi anacheeka eti ananiambia broo kausha niwakimbize hawa "mafala"hili tusi ndo tusi anapenda sana kulitumia
kigogo ni mwanamke aliyekosa mme
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom