Kwa umri wangu sijawahi ona uzalendo Huu

jmchimbadhahabu

JF-Expert Member
Sep 26, 2014
218
106
Jaman,kwa umri wangu toka nimekua sijawahi ona uzalendo na mwitikio mkubwa wa wananchi karibia kila kona ya nchi wakifanya usafi tena kwa furaha isiyo na kifani,nasikasikia kuwa enzi za mwalimu uzalendo huu ulikuwepo wa watu kujitoa kwa masuala ya kitaifa,yaani leo kwa hapa dar mji uliitikia vya kutosha,yaani mpaka raha!! Viva Magufuli,Mungu akujalie maisha marefu kwa kuwaunganisha watanzania waliokuwa wanaelekea kutengana!
 
Watu walikuwa wanaisubiri kwa hamu Tisa desemba hakuna kusubiri balozi wala bibi afya kila mtu aliamka na usafi katika maeneo yanayowahusu.JPM ndio chaguo sahihi la wananchi
 
Tofautisha kati ya uzalendo na amri! Wananchi waliambiwa ambao hawatafanya usafi kwenye maeneo yao watapigwa faini

Mimi sijafanya usafi wala sijaona jirani yoyote akifanya usafi na sijakamatwa wala kupigwa faini.
 
Enzi za Mkwere watani wake wa kisiasa wangewaambia watu wasifanye usafi kwa kuwa wanalipa kodi
 
Rais wa nchi akiwa ni mchapakazi watendaji wanakuwa wachapakazi,wananchi nao wanakuwa wachapaka kazi.Rais akiwa goigoi watendaji wanakuwa goigoi vivyo hivyo kwa wananchi.
Rais akiwa mzalendo na wananchi wanakuwa na uzalendo.rais akiwa mpenda mapenzi.....malizia
 
Tofautisha kati ya uzalendo na amri! Wananchi waliambiwa ambao hawatafanya usafi kwenye maeneo yao watapigwa faini

i can smell unyumbulization in mawimbi ya matumaini

Mleta mada nakupongeza kwa dhati. Nasikitika kusoma maneno humu ambayo kimsingi si ya kukusaidia, isipokuwa kukukatisha tamaa. Umenena la moyoni. Ulichosema ni kweli kabisa. Mie nilipoona mamia ya wananchi kona zote za nchi wakiimba na kushangilia wakati wote wa kufanya usafiri, nilifarijika mno. Nilitokwa machozi ya furaha. Nikaiona Tanzania ile ya Nyerere na Karume tuliyoijua. Hakika suala la usafiri limewarejesha Watanzania kwenye umoja wao, hata kama wapo wachache ambao hawakuitikia.
Enzi za Mwalimu haya mambo yalikuwa ya kawaida sana. Watu walipendana. Walishiriki misaragambo ya aina hii kwa mioyo mikunjufu. Dk. Magufuli anairejesha Tanzania kule kunakotakiwa. Mleta mada nakuombe uendelee kuchimbua historia ya umoja wa Watanzania huko tulikotoka. utafaidi mengi.
 
Kabisaa Kabisaa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom