Kwa Ukata Huu Turudi Kwenye Barter System

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Kwetu sie wa mtaani Kama jinsi tunavyoiona hali halisi ya mzunguko , pesa Hakuna ila vitu vipo, hivi kwanini tusifikirie plan B ya kuanza kubadilishana commodities?Mf chakula, Samani za ndani, Mitambo,electronics..nk
Huenda kuna mtu hapa akawa mkulima na msimu huu alivuna kwa wingi mchele ila ana changamoto ya mahindi, na kuna mwingine ana mahindi na mifugo hana mchele, mwingine TV ameichoka anakosa soko na mwingine Anahitaji TV ila hela hana ana kitanda asichokihitaji.... Mwingine nae anapenda apate wa kubadilishana ampe mtu I phone 6 ibadilishwe kwa Laptop.... Mwingine ana Carina Ti labda anamtafuta mwenye Suzuki Carry wabadilishane.. Nk
Haliwezekani hili?
 
Mtoa mada uko sahihi kabisa, nimeshuhudia kijiji kimoja hivi sikitaji jina watu wanaenda sokoni kuuza bidhaa wanaambulia patupu inabidi wabadilishane. Ukitoa noti ya elfu kumi ni balaa watu wanashangaa ni wapi imetoka na mtatafuta chenchi muda mrefu sana.

Kuna haja ya monetary policy kuangaliwa na serikali kwa kupitia benki kuu waongeze hela kwenye mzunguko. La sivyo barter trade itarudi na kumbuka hii ni mbaya sana kwa serikali kwa sababu inaweza kudidimiza kabisa thamani ya pesa na kupungua kwa kodi.
 
Back
Top Bottom