Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Kwa Ukali Dr Kitila Amjibu Ansbert Ngurumo

Status
Not open for further replies.
Hivi Mr Kitila mkumbo!!? Kama baba yako anataka kujenga nyumba ya familia na ukafanikiwa kuuona mchoro wa nyumba, je! utaenda kuchora mchoro mwingine wa nyumba bila baba yako kuujua au utamwelekeza kuwa mchoro wa nyumba na hasa sehemu iliyokosewa haijakaa sawa!? na je ukienda kuchora mchoro mwingine wa nyumba ukakuta baba ameshaaanza nyumba na tayari imepauliwa, itasaidia kweli!!!??? vinginevyo kama hata kama baba yako atakubaliana na wewe itabidi kubomoa nyumba yote na kuanza upya!!! KITILA HUKUWA NA NIA NJEMA NA CDM, mimi ni mwanaccm mwaminifu sana lkn nakuhakikishia hata kama ulikuwa hujui kuwa nia yako ni ovu, nia yako haikuwa njema, ulitaka kuleta zile siasa za vyuoni kama ulivyokuwa ukifanya pale UD za kufitiana kwa siri kwa lengo la kubomoa, Nakumbuka kuna siku moja wakati tukiwa wote Pugu Secondari wewe ukiwa mwenyekiti wa bweni letu la Azimio tulipanga kugoma tena tukiwa ofisini kwako pale Azimio lkn ulitugeuka na ukaenda kumwambia Marehemu Mnyabuso kidogo tufukuzwe shule, nakumbuka tulikula mboko za kutosha za akina Charwe na Mtera na walituambia kuwa wewe ndo umesema, tena tukasodolewa mbaya kwamba eti tunajifanya kupanga mgomo kwamba ni siri kumbe tunapanga na wanafunzi wanaowapenda waalimu, kama unakumbuka ile issue Form 4 walitaka kukuchapa mpaka siku moja ukaenda kulala kwa head prefect kwa kuogopa, kulikuwa na fununu kuwa vijana walitaka kukula tigo kabisaaa kwa kuwasaliti, na aliyeongoza hii issue kama unakumbuka ni Jamaa mmoja aliitwa Peter Nolasko au Jaa galaganzi jina la utani.
KITILA wewe ni msaliti na ninajua hata hao waliokutuma utakuja kuwasaliti tu, Tatizo lako kitila una kiburi sana na unajiona wewe ni mwerevu sana na huamini wala kukubali kuwa wapo watu wanaoweza kuwa hawajasoma lkn wakawa na akili za mambo kuliko hata wewe, na ninajua kinachokusumbua ni historia yako pia na ulipotoka na mazingira uliyokulia, Kitila wewe ni Mnafiki sana na hauaminiki na kama hutaki kukubali we endelea na mipasho yako mwisho wake utaona.
Duh! kumbe alianza usaliti toka long,asante mkuu kwa kuliweka sawa hili...................!
 
Ndugu Ngurumo,

Nashukuru sana kwa maoni yako . Mimi binafsi ni muumini wa kutofautiana kimawazo katika msingi wa hoja. Siogopi hata kidogo mtu kupinga hoja zangu madamu tu anafanya hivyo kwa hoja. Hivyo naheshimu maoni yako pamoja na kwamba s ikubaliani nawe.

Nadhani utakuwa hujasoma makala zangu zote za hivi karibuni na hasa ya juzi iliyochambua matokeo ya udiwani. Nasema hivi kwa sababu nimeogopa sana unaposema najenga hoja zangu kwa hisia bila ushahidi wa takwimu. Hapana. Soma makala zangu vizuri. Mimi ni muumini wa evidence based writing na nimejitahidi sana katika makala zangu kufanya hivyo.

Makala yako ina maoni mengi, ya msingi na mengine siyo ya msingi sana kama hilo la kusema kwamba ninaandika ninavyoandika sasa hivi kwa sababu nimetoka (nimefukuzwa) CHADEMA. Hii siyo hoja ya msingi kwa sababu hata wewe unajua ukweli kwamba mimi siungi au kukosoa jambo kwa minajili ya uchama, bila kujalai mimi ni wamachama wa husika au la. Sijaanza kuikosoa CHADEMA leo. Nilliikosoa CHADEMA nilipokuwa mwanachama ndani na nje ya vikao. Tofauti pekee. Nitakukumbusha matukio machache.

i) Tarehe 20 Nov 2013 niliandika makala iliyochapishwa katika Gazeti la Raia Mwema nikijadili umuhimu wa kutokuwakatisha tamaa wanaofanya vizuri katika jamii yetu. Katika makala haya, pamoja na mambo mengine, nilikosoa tabia ya viongozi wa CHADEMA ya kumzodoa mwenzao Zitto kwa kukataa posho. Nikaeleza waziwazi kwamba Zitto anapigwa vita ndani na nje ya chama kwenye mambo ya posho. Kwenye kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 21 Nov 2013 Mhe Lema alinilalamikia kwamba kwa nini nawasema viongozi magazetini. Nikajibu kwamba mimi ninaandika kama mtu huru na kama mwanataaluma na ninapotoa mawazo yangu katika umma siangalia mambo ya vyama. Nitatoa maoni yangu kadri fikra zangu na evidence niliyo nayo zinavyonielekeza. Kwa kifupi, kama alivyowahi kusema Steve Biko, 'I write what I like'.

ii) Kwenye matokeo ya udiwani wa mwaka 2012 ambapo CHADEMA ilipata viti 5 kati ya viti 29 vilivyokuwa vinagombaniwa niliandika nikasema CHADEMA inakuwa lakini kwa kasi ndogo. Nikaeleza kwamba kasi ya ukuaji wa chama hiki ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa hamasa na mapenzi kwa chama yaliyopo mitaani. Nikajenga hoja kwamba ni muhimu kikajitathimini kwa nini hakipata kura sawasawa na aina ya hamasa iliyopo. Nikaeleza kwamba kwa kiwango hiki cha ukuaji, kinaweza kuongeza idadi ya madiwani na wabunge, lakini hakitaweza kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa maana ya kushika dola. Jambo hili nililieleza pia ndani ya Kamati Kuu lakini kwa ukali zaidi. Wenzangu hawakufurahishwa na wakasema kwamba mimi sielewi mambo ya field. Nikakubali yakaisha.

iii) Mwaka jana huohuo niliwapinga viongozi wangu wa chama ndani na nje ya vikao kuhusu kumuunga mkono Mbatia kwamba nchi yetu haina mtaala wa elimu. Niliwaeleza viongozi wangu kitaaluma jambo hili si kweli kwa sababu nchi haiwezi ikatoa elimu bila mtaala, na kwamba mtaala sio lazima uwe kwenye document moja inayoitwa mtaala. Niliandika hadi makala. Niliongea kwa simu na kiongozi wa chama akiwa Dodoma kuhudhuria vikao vya bunge. Wapo walionielewa na wengine hawakunielewa.

Kwa hiyo ndugu Ngurumo unaposema kwamba nilikuwa sikosoi kabla sijatoka CHADEMA unanionea au umeamua tu kujiridhisha juu ya hoja yako.

Unasema kwamba kusema CHADEMA si mbadala bila kuonyesha mbadala ni kuwachanganya wasomaji? Kwamba nasema hivi kwa sababu ya uchungu, hasira na chuki. Yes, nina uchungu na hasira, lakini sina chuki hata kidogo. Nina uchungu na hasira kwa sababu chama ambacho nilikitegemea kijenge taswira mpya ya siasa katika nchi hii kimeshindwa. Kinafanya mambo yale yale ambayo CCM wameyafanya kwa miaka chungu nzima. Nitaeleza kidogo hili.

Vyama vingi vilipoanza, CCM walipanick sana wakawa wanawatukana sana wapinzani. Wakawapa kila aina ya majina: mbwa, wanafiki, wasaliti, n.k., kisa wanatofautiana na wao kimsimamo. Lakini leo hii baada ya upinzani (soma CHADEMA) kukua na kujipatia wafuasi nao wanaanza kufanya mambo hayohayo ya kijinga waliyofanya CCM miaka ya tisini: kukebehi, kukejeli, kuwapaka matope na kuwaita wasaliti watu wanaotofautiana nao kimwazo na misimamo. Wapinzani wamejikuta wanauvaa uCCM bila wao kujua.

Sura ya chama inajengwa katika msingi wa hoja na uadilifu wa viongozi. Mambo yote haya hayapo katika upinzani wetu. Viongozi wetu nao wanapenda matumizi ya kutanua huku wakikandia serikali katika matumizi mabaya. Viongozi wetu wanabariki na kupokea maposho ya ajabuajabu bungeni huku wafanyakazi wengine katika nchi hii wakiteseka na viujira vidogo na wakijua msingi mojawapo wa chama ni usawa. Viongozi wanatukana na kukandia mashangingi ya serikali lakini wao wenyewe wananunua hayohayo kwa pesa za uma walizokopeshwa bila riba, na wengine wanachukua mashangingi ya serikali na kutembea nayo barabarani kwa madaha. Sasa huu si ndio uCCM wenyewe au? Unataka CHADEMA ionekana tofauti kwa kuuvaa uCCM?

Tukisema mnasema tuna hasira na uchungu. Ndio tuna uchungu kwa sababu chama hiki tulichokitegemea sana kimeuvaa uCCM na haiwezekani kikaaminika na kuchagulika kwa kuendeleza utamaduni wa uCCM. Ndio maana tunahitaji mbadala. Kwamba kwa sasa hivi hatuna mbadala haimanisha tusitamani na kutafuta mbadala. Tukishakujenga hoja ya uhitaji watu wanaojua namna ya kuanzisha mbadala wataanzisha. Kazi yangu ni kutoa mchango tu na wapo wengine nao watatoa mchango wao.

Mwisho, unaandika kana kwamba maoni yako ndiyo ukweli kiasi cha kusema kwamba sisi tuliyoenda shule tunapaswa kuyajua haya unayoyaandika, ebo kwani maoni yako ndiyo yamekuwa 2+2 ndugu yangu? Maoni yako ni maoni yako kama ambavyo ya kwangu ni maoni yangu, sio sheria. Hatuna uwezo wa kulazimisha watu wakubaliane na maoni yetu. Tunachofanya ni ushawishi tu wa hoja. Wapo watakaoshawishika na wapo ambao hawatashawishika kwa sababu zao: ama kwa kuona au kutoona uzito wa hoja au kwa kuwa tu wanampenda au hawampenda mwandishi wa hoja husika. Hiyo ndiyo tabia ya hadhira na huna namna ya kubadilisha hili. Tujifunze kuheshimu maoni ya wengine bila kulazimika kukubaliana nayo. Na tujifunze pia kutokulazimisha maoni yetu kuwa ndiyo ukweli!

Ahsante

Kitila
Kitila mkumbo,
Binafsi nakusalimia,na pia nakujulisha kwamba mimi si msomi,lakini naweza kupambanua uzuri na ubaya,au uchungu na utamu wa jambo!

binafsi ninachokiona ni uchungu kwako kwa deal yenu ilitibuliwa mapema(usaliti).

Na pia wewe una ile hulka ya wasomi wa kitanzania walio wengi ambao hudhani ukishasoma na kuwa na kiwango cha shahada ya chuo kikuu.basi wewe uko sahihi muda woote.

Lakini kwa hakika si kweli na mimi nikionacho kwako ni mambo mawili.

*ulikwisha kuwa na ndoto za kuukwaa ubunge kupitia cdm na hivyo kutimuliwa kwako ni pigo pengine kubwa kuliko hata kupoteza kazi hapo udsm kwa sababu ulikwisha anza kula kiheshimiwa na kuota kiheshimiwa

*Pili ni kwamba huenda walio nyuma ya haya mambo bado wana kusumbua kwani mkakati umeharibika kabla ya malengo na hivyo uko kwenye plan b" ya kuiwa cdm kwa kutumia taaluma yako kwa mgongo wa makala.

Haiingi akilini kwa mtu yeyote makini asikushangae ghafla umeibuka na kuwa mshambulizi wa cdm ghafla wakati ukijinasibu kama msomi na si mwanasiasa

na tukizingatia kwamba una ajira serikalini na cha ajabu wao serikali wamekaa kimya bila kukuchukulia hatua zozote pamoja na wewe kukiri kufanya siasa(tena upinzani)wakati ni muajiriwa wao pale udsm kitu ambacho Proff baregu hakufanikiwa na alinyimwa mkataba wakati akiwa bado anahitajika.

Kama una nguvu za kuweza kuona mbadala anahitajika kwa nini usikae na wenzako mnaoona mnaendanana kisera na kuamua kanzisha hiyo taasisi yenu,badala ya kudumaza upinzani kwa kutumia kalamu na usomi kutuchanganya tusiosoma kwa manufaa yako binafsi?
Ingawa hutaona matokeo yake kwa sasa lakini utakuja kuyaona ikiwa umeishaimaliza akiba yote ya heshima uliyokuwa umebakiza kwa wapenda mageuzi wote nchini.

Ansbert ngurumo yuko sahihi
 
Ni uungwana na jambo la kistaarabu inapotolewa hoja inayokulenga uijibu kwa uzito wa hoja iliyotolewa. Kwa hiyo ulitaka hoja ya Ngurumo ipite bila kujibiwa ili ionekana anachosema ndicho? Uungwana ni kuacha hoja zote zitolewe ili watu wapime uzito wa hoja zote mbili. Hii tabia inayoibuka ya kupenda kusikiliza yale tu tunayotaka kuyasikia tena kutoka upande mmoja tu haitatusaidia kujenga jamii inayoheshimu uhuru wa kutoa maoni kama msingi wa demokrasia. NINAUKATAA USHAURI WAKO CATEGORICALLY!

kwa vile umejitokeza nadhani unaweza kujibu haya maswali machache,,
*hivi ni kweli ulikuwa ukipokea lak 2 kutoka kwa zitto kila wiki/mwezi????
*kwa nini hamkuuweka waraka wenu hadharani na badala yake mkauweka gizani kichawi???
* Waraka unaongelea gharama za kutengeneza mtandao wenu ndani ya chama,hizo gharama angetoa nani na kwa maslahi yapi????
 
dr kitila usichoke kutuwelimisha kwani tuliona viongozi wetu wa chama kama wako sawa kumbe wamepotea na kutupeleka jahanam kwenye joto kali umewajibu kwa point lakini wameshindwa kutowa wao record yoyote mimi nilijuliza inakuwaje cdm kikakosa udiwani namna hii nikaona kunakasoro ndani ya uongozi hafla nikaona ripoti toka kwa afsa habari wa cdm tumaini makene akitowa data kuwa za udiwani kuwa imeongeza wapiga kura lakini kwenye kata mbili tu zingine akufafanuwa nikamuona -------- kweli mjinga eti daftari liboreshwe ndio mana mi ssm yameshinda nakaona tena mzushi nasati alishinda ubunge je waliboresha daftati lakupigia kura? Jib hapana nikarudi nyuma kuwangalia data za chaguzi za udiwani mwezi wa 11 /2012 watu walipiga kura kwenye kata 29 cdm kilipata kata 7 mwingine ulifanyika mwezi 6/ 2013 kikashinda kata 6 sasa nikiona na haya matokeo yaliopita ya chopa tatu naona kama cdm badala ya kusonga mbele kinarudi nyuma kwa spid kubwa kwani wengi wetu tulitarajia sasa cdm kipate hata madiwani wa 10 kutokana na mda wenyewe kuwelekeya kwenye uchaguzi mkuu je mbowe na dr slaa bila kumsahau tundu lisu kuwa dr kitla falsafa yake kuwa viongozi hao wamechoka hawna jipya? Unaweza ukawa na mtu mkaongea lakini mawazo yake yapo sehemu nyingine kabisa ndio ya cdm na wAfwasi wengi kwenye mikutano kura zinaenda kwa missm dr washauri hata kama ipo nche ya chama asante kitila
 
Anachoota DrKitila hakijikutokea labda chama hicho kiwe chake mwenyewe. Palipo na wengi pana mengi.Sikuzote kinachotuweka pamoja ni sheria kanuni na taratibu nje ya hapo ni fujo na vurugu.Na ndicho Dr kitila unachotaka. Na hupaswi kuaminika coz unajikana mwenyewe eg ooh mimi sikua kiongozi Cdm.Wote ni binadamu hakuna alie sahihi.
 
Kusema 'kwa ukali' ni kujaribu kufanya unnecessary amplification ya jambo ambalo hata halipo, labda kutaka kuharibu mjadala tu.

Ni vigumu kuelewa kwa nini wanatumia hata uongo kuhalalisha hoja zao au matendo yao dhidi ya CHADEMA. Ni kitu kinachoshangaza sana.

But it tells a lot.

acha kupotosha kamanda, wapi dr kasema kwa ukali?! au kwa vile katia msisitizo usiyotaka kuyasikia ndo ulebo huo ndo ukali - wahafidhina hamuachi vituko!!
 
Kitila is right na ana uelewa mkubwa zaidi ya wengi

tatizo nchi yetu tunaongozwa na hisia zaidi

we should learn from wasomi type ya Kitila

Kama ni msomi makini asingjikita kufanya siasa anazozifanya sasa bali angejitokeza rasmi na kufungua chama ili wasomi wenzake wamfuate huko na aiache cdm na watu wake
 
Kusema 'kwa ukali' ni kujaribu kufanya unnecessary amplification ya jambo ambalo hata halipo, labda kutaka kuharibu mjadala tu.

Ni vigumu kuelewa kwa nini wanatumia hata uongo kuhalalisha hoja zao au matendo yao dhidi ya CHADEMA. Ni kitu kinachoshangaza sana.

But it tells a lot.
mkuu hujajibu hoja upo kama wewe binafsi au kama mkurugenzi wa CDM??hoja mzito kama za kitila unazijibu kwa ushuzi?
 
uko sahihi hatofautiani na wasomi wengine kama dr,bana, prof, kapuya, dr,kikwete nk

it is your low understanding capacity na upuuzi unaojiwekea kichwa huku ukitegemea changes

such a waste of a human being

probably this is the reason tutaendelea kuchukulia kila kitu kipumbavu huku wanawake na watoto wanateseka kupata hata mlo wa siku, elimu bora na matibabu

SORRY FOR WASTING MY TIME FOR SUCH A PIECE ON HUMAN WASTE
 
Kitila is right na ana uelewa mkubwa zaidi ya wengi

tatizo nchi yetu tunaongozwa na hisia zaidi

we should learn from wasomi type ya Kitila

Hebu rekebisha sentensi yako isomeke Kitila ana uelrwa zaidi yako, usituingize wengi kwenye kundi la mambumbumbu kama mabehewa kinapoelekea kichwa na wao ndio hukohuko.

And to me nothing to learn from Kitila Mkumbo na kama alivyosisitiza kuhusu kuheshimu maoni ya wengine, mimi kwa maoni yangu Kitila Mkumbo ni jinga na pumbavvu kabisa.
 
dr kitila usichoke kutuwelimisha kwani tuliona viongozi wetu wa chama kama wako sawa kumbe wamepotea na kutupeleka jahanam kwenye joto kali umewajibu kwa point lakini wameshindwa kutowa wao record yoyote mimi nilijuliza inakuwaje cdm kikakosa udiwani namna hii nikaona kunakasoro ndani ya uongozi hafla nikaona ripoti toka kwa afsa habari wa cdm tumaini makene akitowa data kuwa za udiwani kuwa imeongeza wapiga kura lakini kwenye kata mbili tu zingine akufafanuwa nikamuona -------- kweli mjinga eti daftari liboreshwe ndio mana mi ssm yameshinda nakaona tena mzushi nasati alishinda ubunge je waliboresha daftati lakupigia kura? Jib hapana nikarudi nyuma kuwangalia data za chaguzi za udiwani mwezi wa 11 /2012 watu walipiga kura kwenye kata 29 cdm kilipata kata 7 mwingine ulifanyika mwezi 6/ 2013 kikashinda kata 6 sasa nikiona na haya matokeo yaliopita ya chopa tatu naona kama cdm badala ya kusonga mbele kinarudi nyuma kwa spid kubwa kwani wengi wetu tulitarajia sasa cdm kipate hata madiwani wa 10 kutokana na mda wenyewe kuwelekeya kwenye uchaguzi mkuu je mbowe na dr slaa bila kumsahau tundu lisu kuwa dr kitla falsafa yake kuwa viongozi hao wamechoka hawna jipya? Unaweza ukawa na mtu mkaongea lakini mawazo yake yapo sehemu nyingine kabisa ndio ya cdm na wAfwasi wengi kwenye mikutano kura zinaenda kwa missm dr washauri hata kama ipo nche ya chama asante kitila

mkuu mtu kama mimi na wewe wa kuchambua facts,statistics then tuka make comparison hakiyanani naapa hatuwezi ku survive CDM tutaitwa tu wasaliti
 
Hebu rekebisha sentensi yako isomeke Kitila ana uelrwa zaidi yako, usituingize wengi kwenye kundi la mambumbumbu kama mabehewa kinapoelekea kichwa na wao ndio hukohuko.

And to me nothing to learn from Kitila Mkumbo na kama alivyosisitiza kuhusu kuheshimu maoni ya wengine, mimi kwa maoni yangu Kitila Mkumbo ni jinga na pumbavvu kabisa.

nilikua nataka nione ajabu ipite mada hujatukana ,yaani wewe point/facts zako zinajazwa uzito na matusi
 
kitila ndo unakata roho kisiasa afu pia sio lazima ufanye siasa japo siasa ni maisha kwa sasa unatapatapa tu huna hoja umepanic tulia kwanza ujipange ndipo uanze kuandika makala zako kwa sasa una hasira na chadema huwezi kuandika chochote kizuri juu ya chadema kama mimi vile ninavokuchukia kwa kuwa msaliti siwez kukuongelea mahali popote kwa mazuri.na kibaya zaidi dili yako imekufa huko ccm pia napenda ujue kuwa wewe ni muoga sana ndiyo maana mara m2 mara mapango wa mabadiliko kwa kificho

kwa upofu ulio nao - ni kweli dr kaandika utumbo mtupu, siumeona hata matokeo ya kata za majuzi tulivyofanya vizuri, ongeza mahaba tu, 2015 mbowe anatungiza ikulu chini ya mshauri mkuu kamanda lema!!
 
Hebu rekebisha sentensi yako isomeke Kitila ana uelrwa zaidi yako, usituingize wengi kwenye kundi la mambumbumbu kama mabehewa kinapoelekea kichwa na wao ndio hukohuko.

And to me nothing to learn from Kitila Mkumbo na kama alivyosisitiza kuhusu kuheshimu maoni ya wengine, mimi kwa maoni yangu Kitila Mkumbo ni jinga na pumbavvu kabisa.
Kitila ana uelewa zaidi yangu na wewe...:smile-big:
 
Kama ni msomi makini asingjikita kufanya siasa anazozifanya sasa bali angejitokeza rasmi na kufungua chama ili wasomi wenzake wamfuate huko na aiache cdm na watu wake

sio kila mwanassiasa lazima afungue chama... we need neutral political candidates as well
 
Maneno sawa kabisa kutoka kwa dr Mkumbo.
Ngurumo anamtumikia kafiri ili apate mradi wake wakati Mkumbo yuko huru, hafungwi na minyororo ya itikadi kwa sasa!.
Hivi ngrumo haoni jinsi Wabunge wa CHADEMA kama kina Lema wanavyotumia nguvu kuhalalisha posho za kijinga.
Hivi Ngurumo haoni jinsi wabunge wa CHADEMA wanavyobehave kama wabunge wa CCM pindi linapokuja suala la mijihela?

Nianze na boded area, viongozi wengi wa CCM wameshadhihirisha kuwa ni mafisadi na wafujaji wa mali ya umma na hilo halina mjadala. Siku hizi wasemaji wengi wa chama tawala wamekubali kuwa CCM ni wafujaji, hivyo basi kuweka neno 'kama' inawafanya waamini kuwa basi wananchi hawana haja ya kuiamini CDM kwa kuwa wako kama CCM kwa tabia.
Kwenye kikolezo cha rangi ya blue, posho inayodaiwa mh. ZZK aliipinga na wanachama wenzie wakakasirika kwa kuwa wao waliipenda imekuwa ni kigezo kikuu kwa wanachama wa CCM dhidi ya CDM.
Sasa, swali langu linakuja, hivi katika swala la posho ukiacha wabunge wa CCM na CDM ambao wengi wao hupendelea hiyo posho, wabunge wengine wa vyama vingine wanasemaje? Kwa kuwa mi nafikiri hii issue CCM wameifanya tu kete ya comparison, kuwafanya wananchi waone CDM hakifai, na wa vyama vingine je? Au ndio haijalishi, maana ukiinuka kusema jambo liwe baya au jema kama kuna mbaya wako alikuwa anakutafuta, kauli yake utaiona tu, atakuambia 'nilikuwa nakutafuta sana wewe', haijalishi wengine nao wanasema kama wewe, ali mradi kakupata wewe mbaya wake hana shida na wengine.
Na maana yangu hapa ni hii, Zito huenda aliikataa kweli posho, lakini akiwa na lengo lake. Kwa walioafiki labda na wenyewe waliona ni haki yao na hata wakisema waiteme na hali wanaitaka watakuwa waongo. Na isikute wengine wanaichukua na kufanyia mambo ya msingi tu kwenye jamii, si ni hela za watanzania hizo? Wangeikataa ndio tuseme wa CCM wasingechukua? vitu vingapi vinapingwa na bado wa chama tawala wanavipitisha?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom