Kajunjumele BA
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 673
- 351
Mkuu hapa anajicontradict mwenyewe ingekuwa kweli CHADEMA haikui asingeisema kwenye makala yake niajabu katika vyama vinavyo karibia ishirini mtu anakazana kutaja CHADEMA lakini namshukuru mwishoni kaliweka vizuri kwamba yale yalikuwa maoni yake .Kusema 'kwa ukali' ni kujaribu kufanya unnecessary amplification ya jambo ambalo hata halipo, labda kutaka kuharibu mjadala tu.
Ni vigumu kuelewa kwa nini wanatumia hata uongo kuhalalisha hoja zao au matendo yao dhidi ya CHADEMA. Ni kitu kinachoshangaza sana.
But it tells a lot.
Mimi maoni na mtazamo wangu CHADEMA inakua tena kwa kiwango kizuri kabisa ndo maana karibu sehemu nyingi hata ambazo wengi walitarajia na kuzoea CCM ikishinda kwa mbwembwe kulikuwa na kukabana koo na mtu anatoka na ushindi mwembamba tena sehemu za vijijini kabisa .
Katika ukuaji wa CHAMA is a gradual Process ,Siasa siyo Mechi ya Ndondo hapana ni hatua na kila hatua inachangamoto zake tunachotaka kuangalia ni chama kipi kinauwezo wa kuyamsimamia kile kinacho ya sema jibu moja ni CHADEMA.kILA MWENYE AKILI HILI ANALITAMBUA Mf.tunaongelea Katiba Mpya ..katika eneo hili CHADEMA haijatetereka,Kuchukua maamuzi magumu na ya msingi katika kulinda na kujenga nidhamu ya CHAMA...hapa CHADEMA na CUF ni wakupigiwa mfano na siyo CCM ambao wanalalamikia kwenye vungu za vitanda na wengine wakiwa wamevaa vinyago usoni(Kulalamika kupitia Mamluki).
Itakuwa ni kosa kubwa sana kwa CHADEMA kusikiliza ushauri mbovu eti kwa kisingizio cha kulinda mtu...hapana mtu hana nidhamu fukuza ...Hiki ni chama siyo kikundi cha wavuta bangi.Lazima kuwe na nidhamu ya Chama.Ni hatari mtu kujikweza na kuleta uhuni kama waliofanya hao "WAFUKUZWA" kwa kukosa nidhamu na kujiona yeye kuwa bora kuliko wengine. Viongozi wako sahihi ,na CHAMA kiko katika uelekeo mzuri zaidi ni aibu kwa msomi yeyote kuzungumzia matokeo haya na kujidai kipofu kwa kuto kuzungumzia na kuona athari zinazotokana na Tume ya uchaguzi kusuasua katika uboreshaji wa daftari la wapiga kura.