MUTUYAMUNGU
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 1,824
- 4,385
BAYPOT NA PLATNUM CREDIT WAMEANZA KUWAIBIA MANESI NA WAALIMU ZAIDI YA MIAKA 10 ILIYOPITA ILA WANADUNDA HADI LEO... ELIMU ELIMU ELIMU
Hivi serikali hawalioni hili?Mkuu usirogwe uakopa Bayport utalia. Nilishafanya kazi hapo kipindi nimemaliza form six nasubiri kwenda chuo. Ni majanga hao watu ubabaishaji na wizi kwa wateja ndio utaratibu wao.
Makato hata siku moja hawawezi wakakuonyesha ile schedule halisi wanakuwa nazo zile za uongo za kuvuta wateja na baada ya hapo ukishaingia king umeliwa. Ukiopa milioni moja utalipa milioni nne.
Pole sana. Laki 7 mpaka million 3! Hao ni washenzi sana.Nakumbuka 2007 nilikopa bayport sh laki 7 haki ya Mungu nililipa karibia milioni 3.
Kuna siku walipigia simu wakaniambia wameniongezea hela laki 2 ya maelezo ambayo hayaelweki na kweli iliwekwa kwenye acount. Haloo makato yalitaradadi...
Mwambie ndugu na rafiki yeyote asithubutu kukopa bayport.
Pia ukimuona mtu anaingia ofcn kwao msaidie tu kumuambia maana hiyo ni kuzimu
Bila shaka kuna mwana ccm yuko nyuma yao.BAYPOT NA PLATNUM CREDIT WAMEANZA KUWAIBIA MANESI NA WAALIMU ZAIDI YA MIAKA 10 ILIYOPITA ILA WANADUNDA HADI LEO... ELIMU ELIMU ELIMU
Wana mawasiliano na halamashauri zote, Nafikiri kwenye kuwatapeli watumishi, kuna Mrahaba unabaki halmashauriHarafu sijui wanatoa wapi taarifa washenzi hawa,maana wanakupigia simu wanakueleza hadi mkoa ulipo wanakubembeleza ukope. Nimemtukana mmoja nadhani hata rudia.
BAYPOT NA PLATNUM CREDIT WAMEANZA KUWAIBIA MANESI NA WAALIMU ZAIDI YA MIAKA 10 ILIYOPITA ILA WANADUNDA HADI LEO... ELIMU ELIMU ELIMU
Hiki kikundi nimekifuatilia utendaji kazi wake wa kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wasio wa umma, kwa sababu mfanyakazi mpya anapoajiriwa anakosa sifa za kupata huduma ya mkopo kutoka bank, nimegundua kuwa Bayport wanatumia fursa hiyo kupokea maombi ya mikopo kwa kujisifu kwamba wanatoa mikopo yenye riba nafuu, wanakukalisha na kukupigia hesabu ambazo zinaonesha makato yao ni ya kawaida, mziki unakuja pale watakapokuweka kwenye mzani wao, kwanza watakupigia simu kukueleza kwamba kiasi cha mkopo ulichoomba kimeshuka hivyo badala ya kupata mfani million 2, watakupa million 1.8, baada ya hapo ukija kupiga hesabu vizuri, makato yale waliokuandikia wakati wanakipokea kwa tabasamu hayaendani.
Tatizo la pili wana shida kwenye kutoa huduma kwa wale wanaowakata, mfano pale mteja anapoomba balance.
Unaweza ukaomba balance ukakaa miezi Sita hujajibiwa, sasa swali langu Wanakuwa na lengo gani.
Kwa uhuni huu wanaofanya Bayport nadhani wanajiharibia wenyewe, na nashauri ni bora ufe na shida zako kuliko kwenda kuomba mkopo Bayport.