1xbet Sports - EA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2017
- 789
- 729
Hiki kikundi nimekifuatilia utendaji kazi wake wa kutoa huduma kwa watumishi wa umma na wasio wa umma, kwa sababu mfanyakazi mpya anapoajiriwa anakosa sifa za kupata huduma ya mkopo kutoka bank, nimegundua kuwa Bayport wanatumia fursa hiyo kupokea maombi ya mikopo kwa kujisifu kwamba wanatoa mikopo yenye riba nafuu, wanakukalisha na kukupigia hesabu ambazo zinaonesha makato yao ni ya kawaida, mziki unakuja pale watakapokuweka kwenye mzani wao, kwanza watakupigia simu kukueleza kwamba kiasi cha mkopo ulichoomba kimeshuka hivyo badala ya kupata mfani million 2, watakupa million 1.8, baada ya hapo ukija kupiga hesabu vizuri, makato yale waliokuandikia wakati wanakipokea kwa tabasamu hayaendani.
Tatizo la pili wana shida kwenye kutoa huduma kwa wale wanaowakata, mfano pale mteja anapoomba balance.
Unaweza ukaomba balance ukakaa miezi Sita hujajibiwa, sasa swali langu Wanakuwa na lengo gani.
Kwa uhuni huu wanaofanya Bayport nadhani wanajiharibia wenyewe, na nashauri ni bora ufe na shida zako kuliko kwenda kuomba mkopo Bayport.