NMB mjirekebishe, mnakera sana huduma ya mikopo kwa watumishi wa umma

NAMBA MOJA AJAYE NCHINI

JF-Expert Member
Oct 29, 2019
8,538
17,473
NMB ndio benki yenye wateja wengi sana nchini karibia asilimia tisini ya wafanyakazi wa umma mishahara yao inapitia benki hii. Lakini tatizo kubwa la NMB kama benki mama ni huduma ya mikopo mbovu kwa watumishi wa umma kuna mlolongo na usumbufu wa kutosha kwa mtumishi hadi anashawishika kutoa rushwa kwa afisa mikopo za benki ili ahudumiwe haraka.

Mlolongo wa kutembea na fomu za mikopo hadi kwa wanasheria, maafisa utumishi na n.k ni tatizo na adha kwa mkopaji hasa mteja wa kudumu kama mtumishi wa umma.

Najiuliza kitengo cha IT cha benki hii kazi yake nini? Kwanini mikopo isitumie digital technology hadi mtu ahangaike na mafomu kibao wakati taarifa zinaweza zikajazwa na kutumwa moja kwa moja kwa maafisa utumishi?

Mtumishi wa umma taarifa zake zipo kwenye server ya halmashauri kwanini wasiwasiliane na maafisa utumishi moja kwa moja na kupiga hesabu za makato na mkopo husika? Kwanini mtumishi asipate mkopo moja kwa moja bila kufika benki kwa mawasiliano tu ya simu kama BAYPORT WANAVOFANYA KWA WATEJA WAO? Huduma ya salary advance ni nzuri lakini haikidhi haja ya watumishi wa umma.

NMB badilikeni tumechoka kutembea na mifomu ya mikopo wakati tungewasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu na kuzijaza fom na kupatiwa mkopo bila kuhangaika kusaga soli mitaani kwenye ofisi za wanasheria kugongewa mihuri pia na maofisa utumishi kisa mihuri na sahihi wakati yote yanawezekana kidigitali.

Utakuta mtumishi yupo mbali na mji anataka mkopo !matokeo yake mlolongo mrefu una muumiza kwa gharama za kufuatilia mwisho wa siku anakimbilia kwa wanyonyaji kama Bayport na Platnum credit.

Badilikeni MNAWAAIBISHA NA KUWAVUNJA MOYO WATEJA WENU WA KUDUMU WATUMISHI WA UMMA!

Kama mna lolote changieni.

Karibuni.
 
Tatizo sio NMB tatizo ni Serikali yako, usifanye kosa uchaguzi ujao, watumishi wa umma mkirudia kosa mlilofanya 2015 mtaipata tabu.
 
Sio kweli kuwa form ya mtumishi anapoomba mkopo anaenda kwa mwanasheria. Kufanya nini?

Kwa ofisa utumishi wako lazima upite, ili benki ijue kama bado umeajiriwa hapo au umeishakimbia
 
Kuna tawi moja huku wahudumu wananyodo hatari majibu yao kichefuche, walinikera mpka Basi .N BC wako wapi, haw hapa changu mkononi maishabyanaendelea.
 
NMB ndio benki yenye wateja wengi sana nchini karibia asilimia tisini ya wafanyakazi wa umma mishahara yao inapitia benki hii. Lakini tatizo kubwa la NMB kama benki mama ni huduma ya mikopo mbovu kwa watumishi wa umma kuna mlolongo na usumbufu wa kutosha kwa mtumishi hadi anashawishika kutoa rushwa kwa afisa mikopo za benki ili ahudumiwe haraka.

Mlolongo wa kutembea na fomu za mikopo hadi kwa wanasheria, maafisa utumishi na n.k ni tatizo na adha kwa mkopaji hasa mteja wa kudumu kama mtumishi wa umma...
Huu utaratibu upo pia CRDB, sijui ndio sheria zao???
 
Wamekuja na NMB app lakini hakuna huduma ya mikopo ya muda mrefu! Eti wana salary advance pekee!!Sasa kama wana huduma hiyo hiyo nyingine mnashindwa nini? Wasiwasi wa nini sasa!kama tayari una huduma ya salary advance!!!
 
Wapuuzi sana nmb, walianzisha uzi wao humu lakini Wala hawajali, watu wanauliza maswali, wanatoa kero zao Wala hawajaliwi. Mtu unaomba mkopo wiki nzima hakuna jibu la maana wakati taratibu zote umekamilisha.

Nawahama rasmi, bora kwenda kujaribu kwingine.
 
Taasisi unayoifanyia kazi, haijaweka sawa mambo, kwingine ukishajaza form, ya mkopo kazini kwako, wewe umemaliza, ni taasisi yako ndiyo watakawasiliana na benk, benki form ya mkopo wakishaipata leo, wanakuwekea hela leo ama kesho yake, kutoa rushwa kutaka mwenyewe tu.
 
Ni wiki ya 3 Sasa tangu niombe kulipa deni lao.
Hapa nasubiri barua ya deni.
Wanasema HQ hawajarudi shauri ya korona so hawapo ofisini.
Sijui hii bank inatuonaje
 
Mmmh!! Sio kweli, labda huko kwenye tawi lenu. Kuna mtu last week alikwenda bank akachukua form kisha akaipeleka wilayani ikasainiwa, same day akaipeleka bank na same day jioni akawekewa mkopo wake.
 
Mmmh!! Sio kweli, labda huko kwenye tawi lenu. Kuna mtu last week alikwenda bank akachukua form kisha akaipeleka wilayani ikasainiwa, same day akaipeleka bank na same day jioni akawekewa mkopo wake.
Wewe unafanya kazi nmb? Mimi nimejaza fom na kuikamilisha ofisini kwangu na kuipeleka benki toka ijumaa ya tarehe 29/5 hadi leo sijapata mkopo. Hakuna jibu la maana zaidi ya majibu ya hovyo.
 
Back
Top Bottom