Kwa ufaulu huu naweza pata chuo cha afya cha serikali?

DALT

Senior Member
Jul 17, 2021
168
74
Mimi ni mwanafunzi niliyemaliza kidato Cha nne na kupata ufaulu ufuatao kwenye masomo ya sayansi, Physics-C, Chemistry-A, Biology-B, B/math-B.

Sasa nilikuwa nataka nifanye maombi yangu kwenye vyuo vya afya vya serikali kwa ngazi ya stashahada, na kozi ninayotaka kuisoma ni utabibu, je kwa ufaulu huu naweza pata chuo cha afya cha serikali?

Shukrani kwenu nakaribisha mawazo yenu.
 
Maksi zako nzuri japo sikushauri uombe vyuo vikongwe maana ushindani mkubwa
 
Mtwara
Mafinga
Kibaha
Kilosa
Tanga

Ila vingine ukiomba unapata kirahisi sana maksi zako nzuri ...au nakushauri kama kweli unataka pesa za fasta bila mawazo hapi baadae kaombe Radiology Muhimbili pale ada ni sawa na vyuo vingine vya kati...
 
Nitapata nafasi kweli hapo Muhimbili bila refa mkuu
 
Mimi ni mwanafunzi niliyemaliza kidato Cha nne na kupata ufaulu ufuatao kwenye masomo ya sayansi, Physics-C, Chemistry-A, Biology-B, B/math-B.

Sasa nilikuwa nataka nifanye maombi yangu kwenye vyuo vya afya vya serikali kwa ngazi ya stashahada, na kozi ninayotaka kuisoma ni utabibu, je kwa ufaulu huu naweza pata chuo cha afya cha serikali?

Shukrani kwenu nakaribisha mawazo yenu.
Dogo unaelekea shimoni..bora kasome pharmacy..co sasahivi hawana tofauti na walimu kwaingi wa idadi ya wahitimu.

Ila kama unataka sifa ya kuvaa koti jeupe huku umening'iniza stetho..ila njaa kali huna hela sawa kakomae but usije unalilia ahapa mshahara madogo au umekosa kazi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu C.O ni njia tu ninayotaka kupitia lakini lengo langu nataka niwe daktari(MD)
 
Mimi ni mwanafunzi niliyemaliza kidato Cha nne na kupata ufaulu ufuatao kwenye masomo ya sayansi, Physics-C, Chemistry-A, Biology-B, B/math-B.

Sasa nilikuwa nataka nifanye maombi yangu kwenye vyuo vya afya vya serikali kwa ngazi ya stashahada, na kozi ninayotaka kuisoma ni utabibu, je kwa ufaulu huu naweza pata chuo cha afya cha serikali?

Shukrani kwenu nakaribisha mawazo yenu.
Ushindani ni mkubwa college za serikal, probability kubwa ya kupata vyuo vya private
 
Mkuu C.O ni njia tu ninayotaka kupitia lakini lengo langu nataka niwe daktari(MD)
Unadhani ni ragisi kiasi hicho? Sasa kwa taarifa yako tu kwa sasa njia rahisi kua MD ni kupitia Form 6 kibao kimegeuka...unakuta Nafasi za MD kwa C.O zipo 10 na waombaji elfu 3..Kipaumbele wanapewa sana form 6.Mimi ni C.O nimemaliza 2020 lakini tangu nipo mtaani naliona gemu lilivyo wanaowini ni kozi zingine kabisa Radiology,Dental(hapa nina jamaa angu tulimaliza mwaka mmoja lakini simfikii hata robo).
 
Omba Dental Au Radiology hizo maksi nzuri unapata bila shaka na hautakuja kujuta na kama utadharau huu ushauri miaka 3 baadae utakuja kuukumbuka katika majuto.
Nimekupata mkuu tafanya hivyo,Asante kwa kunifumbua macho mdg wako
 
Fata ushauri achana na CO, japo unaweza kusoma kitu unachokipenda hatujui labda mna zahanati yenu,
Kozi mzuri za afya kwa ngazi cheti na diploma Kwa Sasa ni
-Pharmacy
-Radiology
-Laboratory
-Dental
 
Kazana utafte pesa za mtaji ukajiajil, hayo mambo ya vyuo sjui nn unapoteza muda ndugu yangu.

Ukweli mchungu lkn lazima usemwe ili watu wapate kupona.

Akili za kuajiliwa bado mnazo?? Shame on you
 
umeongea point ingawa wapo waliojiajiri wanatamani wangesoma maana so kwa msoto huo wanaokutana nao
 
Back
Top Bottom