Kwa tume hii: Muungano umevunjwa rasmi

Hii stori na tishio vya kuvunja muungano mbona siyo vipya. Mkithutubutu tutawavamia na kuwatawala milele bila hata ya kuwapa nafasi ya kuwa na rais wa baraza kama ilivyo sasa. By the way hata tukiamua kuwaacha mhangaike mtaishije bila bara wakati hamna viwanda na kila kitu mnategemea bara? Sana sana mkivunja muungano CUF itawatawala kimabavu na kihafidhina hadi mkome. Bila muungano zanzibar haitakuwapo. Pemba watataka wajitenge na Unguja na vile visiwa vingine vidogo navyo vitaamua kuwa jamhuri. Hivyo tutakuwa na utitiri wa jamhuri za kiwendawazimu kibao.
 
Nimejiunga JF baada ya kuona majina yaliomo kwenye tume ya katiba,
Upande wa zanzibar tumeridhishwa kiasi na uteuzi ingawa kuna baadhi ya watu ni watetezi wa muungano, lakini tuna furaha kwa kuwa idadi ya watetezi wa serikali 2 ni ndogo kuliko wale wanaotaka muungano wa mkataba kamailivyo kenya na tanzania. T
unashukuru baadhi ya wajumbe wameshiriki katika mijadala mali mbali na tumeona mitizamo yao.
Hongera sana JK, Wazanzibar sasa tunavunja muungano rasmi tuwaache na UFISADI wenu, na mtaona baada ya muda mfupi tutakuwa na maendeleo.
Kama hamtakubali kutawaliwa na ccm na pia kama utapatikana ufadhili toka bara Arabu maana kimsingi hakuna mnachozalisha huko kiasi kwamba bara wawe wanawafilisi kwa ufisadi, tatizo huko tunawabeba lakini hamuoni - jiulize kuhusu umeme tu acha mengine (viwango vya kodi)
 
Nilijua tu kwamba chokochoko lazima zianze tu. Ok let's wait.
 
Ni lini sisi wabara tuliwalazimisha wazanzibar kuhusu MUUNGANO? Zanzibar mna nchi, mna katiba, mna rais wa Zanzibar ambavyo sisi hatuna. Sisi kama wabara hatujawahi hata siku moja kuulizwa tunautaka muungano au la, hivyo walaumuni viongozi wenu wa Zanziba na CCM kwa kulazimisha muungano. Na si kuanza kuzungumza as if sisi wabara tunawalazimisha au tunawang'ang"aniza wazanzaiba kuwemo ktk muungano. Kama hamtaki muungano muda ni huu tunapo jadili katiba wekeni mambo hadharani na si kulalama lalama ili Dunia ione WATANGANYIKA ndio tunawalazimisha muwe ktk MUUNGANO. KARUME alishawaambia Muungano ni sawa na koti likikubana unalivua, sasa kama MUUNGANO una wabana UVUENI. TUMECHOKA NA MANENO MANENO YENU UTANZANI CC NA NYINYI TUPO KWENYE UKE WENZA

Babuu, nadhani hujafuatilia mambo tunavyoyaanika hadharani huku Zenji, imefka hadi mmeshtaki kwa Police kwamba tunawanyanyasa kwa kuwaita Watanganyika ktk makongamano yetu. Mimi nimeshangaa huyu Kikwete kujipendekeza kwetu na tayari khabari ameshaipata kutoka Bwawani Hotel, Viwanja vya Kisonge, Kibanda maiti nk. kwamba Waznzbari hatuutaki muungano na pia ujumbe huu alipewa Samuel sitta auwasilishe kwa Bos wake.
 
Hii stori na tishio vya kuvunja muungano mbona siyo vipya. Mkithutubutu tutawavamia na kuwatawala milele bila hata ya kuwapa nafasi ya kuwa na rais wa baraza kama ilivyo sasa. By the way hata tukiamua kuwaacha mhangaike mtaishije bila bara wakati hamna viwanda na kila kitu mnategemea bara? Sana sana mkivunja muungano CUF itawatawala kimabavu na kihafidhina hadi mkome. Bila muungano zanzibar haitakuwapo. Pemba watataka wajitenge na Unguja na vile visiwa vingine vidogo navyo vitaamua kuwa jamhuri. Hivyo tutakuwa na utitiri wa jamhuri za kiwendawazimu kibao.

Ama kweli wewe Mpayukaji, labda jiulize kabla ya muungano ilikuwa na uchumi gani mpaka Nyerere alihisi tishio kwake na kulazimisha huu muungano feki ? Bora kujitawala hata kama utakuwa maskini kuliko kutawaliwa.
Hayo mambo ya UUnguja na Upemba yalipandikizwa na Watanganyika na ndio maaana Serikali ya umoja wa kitaifa Watanganyika wengi hawakuipenda, kwa kuwa wao wamezoea kutugawa ili watutawale, lakini mara hii hamtowahi aabadan.
 
Muungano wa Tanganyika na Zenji ni sawa na muungano wa ng'ombe na kupe. Dawa yake DDT.
 
Nimejiunga JF baada ya kuona majina yaliomo kwenye tume ya katiba,
Upande wa zanzibar tumeridhishwa kiasi na uteuzi ingawa kuna baadhi ya watu ni watetezi wa muungano, lakini tuna furaha kwa kuwa idadi ya watetezi wa serikali 2 ni ndogo kuliko wale wanaotaka muungano wa mkataba kamailivyo kenya na tanzania. T
unashukuru baadhi ya wajumbe wameshiriki katika mijadala mali mbali na tumeona mitizamo yao.
Hongera sana JK, Wazanzibar sasa tunavunja muungano rasmi tuwaache na UFISADI wenu, na mtaona baada ya muda mfupi tutakuwa na maendeleo.

Charles Njonjo wa Kenya alisheherekea kwa kunywa mvinyo siku EAC ilipovunjika mwaka 1977.
Mimi Mtanganyika bado napanga nitasheherekeaje siku Tanganyika yangu itakaporejeshwa. Na hii ya kuwa na wajumbe 15 kuja kutuamulia mambo ya Watanganyika million 40 ni kioja na ujinga lakini kwa kuwa itarahisisha kurejeshwa kwa Tanganyika yangu basi bora niifumbie macho.
 
Ni udini tu umetumika hapa! Kufanya ujanjaujanja wa kichinichini kwa kutumia mwavuli wa wajumbe wengi wa Zanzibar ambao wote ni waislamu ni maandalizi ya awali ya kutaka kuwatumia wawakilishi wa Zanzibar kuhalalisha mambo wanayoyataka wao, kama vile mahakama ya kadhi n.k. Hebu fikiri kwa mfano inatokea kwamba hoja fulani inatakiwa ipigiwe kura, ni nini kitafanyika? Poleni watanzania. Bado tuna safari ndefu!
 
Ama kweli wewe Mpayukaji, labda jiulize kabla ya muungano ilikuwa na uchumi gani mpaka Nyerere alihisi tishio kwake na kulazimisha huu muungano feki ? Bora kujitawala hata kama utakuwa maskini kuliko kutawaliwa.
Hayo mambo ya UUnguja na Upemba yalipandikizwa na Watanganyika na ndio maaana Serikali ya umoja wa kitaifa Watanganyika wengi hawakuipenda, kwa kuwa wao wamezoea kutugawa ili watutawale, lakini mara hii hamtowahi aabadan.

Unapozungumzia Watanganyika wengi hawakuipenda serikali ya umoja wa kitaifa znz una data zipi? Kama unazungumzia ccm ina maana ya watu kama million tano hivi. Na hata huko ccm majority hawana habari na haiwahusu mnachofanya huko zenj. Maswala yenu huko zenj yanawahusu viongozi zaidi. Kwa Mtanganyika wa kawaida na wako mamillioni he couldnt care less kama muna umoja wa kitaifa au utengano wa kitaifa.
 
Muungano hautavunjika kwa wajumbe wa tume waliopo ..

Na hiyo si katika hadidu za rejea; ila muundo wa muungano ultimately unatakiwa ubadilike ...

Wazenj tupambane kubadili mfumo wa muungano kwenda serikali tatu na kuvunja muungano hilo halitawezekana abadan
 
Back
Top Bottom