Kwa tabia hii una tofauti gani na Ibilisi?

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,524
6,505
Tabia iliyomponza Ibilisi ni KIBURI. Baada ya kuambiwa na Mwenyezi Mungu amsujudie Adam sijida ya heshima basi yeye alikataa Kwa kujawa na Kiburi kwasababu yeye alijiona Bora sana.

Na alipoambiwa kwanini ulikataa kumsujudia Adam akasema;

Mimi ni Bora nimeumbwa Kwa Moto na yeye ameumbwa na Udongo

Kwahiyo Ibilisi akajiona yeye ni Bora zaidi ndio maana akakataa amri ya ya Mola wake.

Na Mwenyezi Mungu anasema hakika Kiburi ndio vazi lake kwahiyo yeyote ambaye analeta kiburi basi anafanya kosa kubwa Sana.

Na ili ujue Kibri ni kosa kubwa Sana mpaka Mwenyezi Mungu akamhukumu Ibilisi aende Motoni ,ebu tuangalie Ibilisi alikuwa wa namna gani.

Inasemwa Ibilisi alikuwa anafanya ibada Sana kiasi ambacho hakuna sehemu yoyote katika ardhi hakuacha Kusujudu,alisujudu kila sehemu Kwa AJILI ya kumwabudu Mola wake

Lakini

Pamoja na yote hayo basi Kiburi kikamuweka mbali na Mola wake na kuhukumiwa adhabu mbaya kabisa

Sasa baadhi yetu nasi tuna Uibilisi Fulani hivi ingawa ukitutazama machoni tunaonekana kama watu vile lakini tumejawa na Kiburi kupindukia katika Maisha yetu.

Kisa wewe ni CEO sehemu Fulani basi unajiona wewe ndio wewe, unajiona mpanaaa na wengine wote unawaona hawana maana kabisa,husikilizi shida za wafanyakazi wako,hujali mahitaji Yao kwasababu wewe ndio kila kitu hapo,usichojua ni kwamba kila kitu kina mwisho na IPO siku hiyo nafasi utaiacha, kwahiyo usitumie cheo kunyanyasa watu.

Malecture mpo? Nyie nanyi huwa mnajiona mko juu Sana kwasababu Maisha ya taaluma ya mwanachuo yapo mikononi mwenu basi mmejawa na Kiburi kuwa angamiza wanafunzi wenu tena saa nyingine kwasababu za kipuuzi Sana,machoni mnaonekana kama watu lkn mna Uibilisi Fulani hivi.

Madaktari na Manesi mpo? Nyie nanyi kwakuwa afya za binadamu wenzenu zipo mikononi mwenu basi Kiburi ni sehemu ya Maisha yenu. Mko radhi wagonjwa wafe au waendelee kupata maumivu kwasababu tu ya kiburi chenu,tena hawa manesi ndio balaa kabisa, mnayowafanyia wanawake wenzenu huko sehemu za kujifungua yaani Mungu Tu ndio anajua kwakweli, acheni Kiburi mwisho wenu utakuwa mbaya Sana.

Wana usalama kwanza nawapa Salute Kwa heshima yenu! Lakini nanyi pia huwa mnazingua Sana mnapokuwa katika majukumu yenu,kwa nafasi yenu huwa mna Kiburi Sana kwakuwa mna nguvu ambayo mmepewa na Katiba,niwakumbushe Tu ubinadamu ndio kila kitu katika Maisha IPO siku utaacha hayo majukumu na utarudi mtaani na huenda karma itafanya kazi yake.

Hiyo ni mifano michache Tu ambayo nimeitumia lkn watu viburi ambao Wana Uibilisi ndani yake wapo wengi Sana na wanakiburi Sana Kwa nafasi zao hadhi zao walizo kuwa nazo.

Niwakumbushe Tu kwamba Kiburi ni vazi la Mwenyezi Mungu kwahiyo unapokuwa Kiburi ni kana kwamba unataka kuchukua vazi lake nadhani mwisho wake unaujua utakuwaje.

Niwakumbushe nyie ni viumbe wa Allah hamna mnachokimiliki hapa duniani, kwahiyo muishi vizuri na watu na muwatendee wema daima dawamu ili muwe na mwisho mwema.

Ni hayo tu!

Kazakh destroyer
adriz
Msonjo
baby zu
reymage
To yeye
Mademoiselle
 
Ila mungu alikosea sana kusema adam amsujidie iblis maana adam kaombwa na udongo dhalili wakati iblis kaumbwa kwa moto na ukitoa jambo la iblis kukataa kumsujudia adam hana jambo baya alilowahi kufanya hapa duniani wakati huyo mwanadamu ana mabaya kila kukicha na baadhi umeyataja kwa makundi ya watu wanaofanya mabaya kunzia madokata wanausalama viongozi

Nakumbuka malaika walimwambia mungu usiumbe mtu binadamu kwakuwa atakuja kuleta fitna mauvo mabaya duniani ila malaika hawakuwahi kumwambia mungu usimuumbe iblis utakuja kuona iblis hana baya ila watu ndio wabaya ila ushauri wako mzuri saana kwa jamii
 
Allah anafanya atakalo.
Ila jina lako ni mtihani, kwa nini umeamua kujipa jina hilo
Tabia iliyomponza Ibilisi ni KIBURI. Baada ya kuambiwa na Mwenyezi Mungu amsujudie Adam sijida ya heshima basi yeye alikataa Kwa kujawa na Kiburi kwasababu yeye alijiona Bora Sana .

Na alipoambiwa kwanini ulikataa kumsujudia Adam akasema;

Mimi ni Bora nimeumbwa Kwa Moto na yeye ameumbwa na Udongo

Kwahiyo Ibilisi akajiona yeye ni Bora zaidi ndio maana akakataa amri ya ya Mola wake.

Na Mwenyezi Mungu anasema hakika Kiburi ndio vazi lake kwahiyo yeyote ambaye analeta kiburi basi anafanya kosa kubwa Sana.

Na ili ujue Kibri ni kosa kubwa Sana mpaka Mwenyezi Mungu akamhukumu Ibilisi aende Motoni ,ebu tuangalie Ibilisi alikuwa wa namna gani.

Inasemwa Ibilisi alikuwa anafanya ibada Sana kiasi ambacho hakuna sehemu yoyote katika ardhi hakuacha Kusujudu,alisujudu kila sehemu Kwa AJILI ya kumwabudu Mola wake

Lakini

Pamoja na yote hayo basi Kiburi kikamuweka mbali na Mola wake na kuhukumiwa adhabu mbaya kabisa

Sasa baadhi yetu nasi tuna Uibilisi Fulani hivi ingawa ukitutazama machoni tunaonekana kama watu vile lakini tumejawa na Kiburi kupindukia katika Maisha yetu.

Kisa wewe ni CEO sehemu Fulani basi unajiona wewe ndio wewe, unajiona mpanaaa na wengine wote unawaona hawana maana kabisa,husikilizi shida za wafanyakazi wako,hujali mahitaji Yao kwasababu wewe ndio kila kitu hapo,usichojua ni kwamba kila kitu kina mwisho na IPO siku hiyo nafasi utaiacha, kwahiyo usitumie cheo kunyanyasa watu .

Malecture mpo? Nyie nanyi huwa mnajiona mkuu juu Sana kwasababu Maisha ya taaluma ya mwanachuo yapo mikononi mwenu basi mmejawa na Kiburi kuwa angamiza wanafunzi wenu tena saa nyingine kwasababu za kipuuzi Sana,machoni mnaonekana kama watu lkn mna Uibilisi Fulani hivi.

Madaktari na Manesi mpo? Nyie nanyi kwakuwa afya za binadamu wenzenu zipo mikononi mwenu basi Kiburi ni sehemu ya Maisha yenu. Mko radhi wagonjwa wafe au waendelee kupata maumivu kwasababu Tu ya kiburi chenu,tena hawa manesi ndio balaa kabisa,mnayowafanyia wanawake wenzenu huko sehemu za kujifungua yaani Mungu Tu ndio anajua kwakweli, acheni Kiburi mwisho wenu utakuwa mbaya Sana.

Wanausalama kwanza nawapa Salute Kwa heshima yenu! Lakini nanyi pia huwa mnazingua Sana mnapokuwa katika majukumu yenu,kwa nafasi yenu huwa mna Kiburi Sana kwakuwa mna nguvu ambayo mmepewa na Katiba,niwakumbushe Tu ubinadamu ndio kila kitu katika Maisha IPO siku utaacha hayo majukumu na utarudi mtaani na huenda karma itafanya kazi yake.

Hiyo ni mifano michache Tu ambayo nimeitumia lkn watu viburi ambao Wana Uibilisi ndani yake wapo wengi Sana na wanakiburi Sana Kwa nafasi zao hadhi zao walizo kuwa nazo.

Niwakumbushe Tu kwamba Kiburi ni vazi la Mwenyezi Mungu kwahiyo unapokuwa Kiburi ni kana kwamba unataka kuchukua vazi lake nadhani mwisho wake unaujua utakuwaje.

Niwakumbushe nyie ni viumbe WA Allah hamna mnachokimiliki hapa duniani, kwahiyo muishi vizuri na watu na muwatendee wema daima dawamu ili muwe na mwisho mwema.

Ni hayo Tu!

Kazakh destroyer
adriz
Msonjo
baby zu
reymage
To yeye
Mademoiselle

Ila mungu alikosea sana kusema adam amsujidie iblis maana adam kaombwa na udongo dhalili wakati iblis kaumbwa kwa moto na ukitoa jambo la iblis kukataa kumsujudia adam hana jambo baya alilowahi kufanya hapa duniani wakati huyo mwanadamu ana mabaya kila kukicha na baadhi umeyataja kwa makundi ya watu wanaofanya mabaya kunzia madokata wanausalama viongozi

Nakumbuka malaika walimwambia mungu usiumbe mtu binadamu kwakuwa atakuja kuleta fitna mauvo mabaya duniani ila malaika hawakuwahi kumwambia mungu usimuumbe iblis utakuja kuona iblis hana baya ila watu ndio wabaya ila ushauri wako mzuri saana kwa jamii
 
Umesema kweli kaka na nadhani hili ni vema hata ktk malezi ya watoto tuwafunze kujishusha kwa walio chini yao hii itawasaidia huko mbele wakikua waweze kuishi vema, allah atuepushe na viburi ktk hali tulizo nazo na akitupandisha madaraja basi atujaze hekima
 
Allah anafanya atakalo.
Ila jina lako ni mtihani, kwa nini umeamua kujipa jina hilo
Ukisoma vizuri kitabu cha ARBAIN HADITHY NNAWAY kuna hadihi inasema mtume anasema INNAMAL AMALU BI NIYYAT hakika kila tendo kwa niya na mtu hunuiya anayofanya maana ni kwamba angalia nia ya mtu wengi wenu nyinyi waislam na wakristo ni majina tu matendo yenu zero wazinifu wao wasengenyi wao wezi wao wanafki wao sasa kuna tofauti gani kati ya iblis na waislam au wakristo wa sasa
 
Shukran japo sijaelewa hili jibu ni la swali la jina lako au
 
Ila mungu alikosea sana kusema adam amsujidie iblis maana adam kaombwa na udongo dhalili wakati iblis kaumbwa kwa moto na ukitoa jambo la iblis kukataa kumsujudia adam hana jambo baya alilowahi kufanya hapa duniani wakati huyo mwanadamu ana mabaya kila kukicha na baadhi umeyataja kwa makundi ya watu wanaofanya mabaya kunzia madokata wanausalama viongozi

Nakumbuka malaika walimwambia mungu usiumbe mtu binadamu kwakuwa atakuja kuleta fitna mauvo mabaya duniani ila malaika hawakuwahi kumwambia mungu usimuumbe iblis utakuja kuona iblis hana baya ila watu ndio wabaya ila ushauri wako mzuri saana kwa jamii
Asante Kwanza Kwa mchango wako

Unajua kama ulivyosema Malaika walionyesha wasi wasi juu ya kuumbwa Sisi kwasababu wakiangalia uzoefu kuna miamba ilimwaga damu Sana na mabalaa

Sasa

Mungu alitaka kuwaonyesha kuwa yeye anajua anachokiumba,ndo akamfundisha Adamu majina ya kila kitu halafu akawauliza malaika wataje lkn wakashindwa ndio Adam akataja

Kwahiyo ndio akawaambia wamsujudie Kwa heshima na kuwaonyesha kwamba huyo waliye dhani ni balaa kumbe yupo vizuri

Kosa la Ibilisi na kupinga amri ya Muumba wake kwasababu ya kiburi akaambiwa pita huku
 
Ukisoma vizuri kitabu cha ARBAIN HADITHY NNAWAY kuna hadihi inasema mtume anasema INNAMAL AMALU BI NIYYAT hakika kila tendo kwa niya na mtu hunuiya anayofanya maana ni kwamba angalia nia ya mtu wengi wenu nyinyi waislam na wakristo ni majina tu matendo yenu zero wazinifu wao wasengenyi wao wezi wao wanafki wao sasa kuna tofauti gani kati ya iblis na waislam au wakristo wa sasa
Una point mkuu
 
lakini huoni mungu alimdhalilisha iblis maana iblis tayri alikuwa mtu mkubwa na aliumbwa kabla ya adam alikuwa anaitwa ABAA SAJID baba wa kusujudu ni sawa na ww uwe na cheo flani na hadhi kubwa katika nchi na na umri upatao miaka 50 halafu raisi wa nchi akwambie mwamkie mtoto wa miaka 20 kisa amejibu swali vizuri huo udhalilishaji wa kijinsia
 
lakini huoni mungu alimdhalilisha iblis maana iblis tayri alikuwa mtu mkubwa alikuwa anaitwa ABAA SAJID baba wa kusujudu ni sawa na ww uwe na cheo flani na hadhi kubwa katika nchi na na umri upatao miaka 50 halafu raisi wa nchi akwambie mwamkie mtoto wa miaka 20 kisa amejibu swali vizuri huo udhalilishaji wa kijinsia
Ni maoni mazuri Kwa hapa duniani

Lakini

Mwenyezi Mungu yeye ndio muuumba wetu kwahiyo kitendo cha Ibilisi kuleta Kiburi mwa Muumba wake kilikuwa ni Kiburi Kikubwa Sana.

Na Kiburi ni sifa ya Mwenyezi Mungu kwahiyo aliingia katika anga za mwenye mwenye mamlaka
 
Back
Top Bottom