Mazungumzo Mabaya Huharibu Tabia Njema

John Magongwe

Member
Jan 4, 2024
22
24
Mazungumzo Mabaya Huharibu Tabia Njema
Katika maisha, kila mwanadamu ana tabia yake, malengo yake na mipango ya kufika kwenye malengo yake. Pamoja na hayo, wanadamu hukutana, kuchanganyikana na kubadilishana mawazo. Katika hali hiyo, wengine wana uwezo wa ushawishi mkubwa kuliko wengine. Hiyo hutokea kutokana aidha na karama za mtu binafsi katika ushawishi, au nia njema au mbaya dhidi ya wanaomzunguka.

Je, unajua kuwa mazungumzo mabaya, yanaharibu tabia njema?
Kikristu, Biblia inasema katika 1Wakorintho 15:33: “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”. Hapo haisemi, “mazungumzo mabaya yanachochea tabia mbaya”, bali inasema “yanaharibu tabia njema”. Maana yake ni kuwa mtu mwenye tabia njema, na nzuri na inayovutia, anapoketi kuzungumza, au kusikiliza mazungumzo mabaya, kidogo kidogo anaanza kuiharibu ile tabia yake njema. Haijalishi, hatashiriki kwenye hayo mazungumzo, lakini hata kile kitendo cha kusikiliza tu, tayari akili yake hutafakari kinachozungumzwa, na tabia yake itaanza kuathirika. Ndiyo maana Biblia inatuonya tukae mbali na mazungumzo yote mabaya.

Je, mazungumzo mabaya ni yapi?
Haya ni mazungumzo yote yenye maudhui ya uzinzi, usengenyaji, umbea, wizi, au anasa na starehe za kidunia, na mengine ya aina hiyo. Kwa ujumla, ni mazungumzo yote yanayoenda kinyume na maandiko kwenye Biblia.

Baadhi ya njia ambazo mazungumzo mabaya hupatikana ni katika sehemu zifuatazo.

Kwenye Vijiwe
Vijiwe ni sehemu yoyote watu wanapokutana kujifurahisha kwa maneno, au michezo. Kwa mfano vijiwe vya watu wanaocheza michezo ya drafti, au bao, wanaobashiri, au mipira, waendesha bodaboda, n.k.

Kwenye Mitandao
Mtu anapotumia muda mwingi kukaa kwenye mitandao kama vile facebook, au whatsapp na mingine, anapojiunga kwenye makundi yasiyo ya neno la Mungu, au yasiyo na maana kwa maudhui ya kimaendeleo, hata kama hachangii chochote katika mijadala inayozungumziwa, yeye ni msomaji tu, afahamu kuwa anaiharibu tabia yake njema.

Luninga
Unapotazama tamthilia za kidunia, pamoja na vipindi vingine vya kidunia na mijadala, na midahalo mbalimbali katika luninga, ambayo maudhui yake ni ya kidunia, fahamu kuwa unaingiza agenda mbalimbali akilini mwako, ambazo zinaweza kuharibu tabia yako njema. Hata kama wewe huchangii chochote, ni mtazamaji tu, bado tabia yako inaguswa na kuharibika.

Vitabu vya Simulizi
Unaposoma vitabu vya simulizi za kidunia, ambazo ni tungo za watu, ambazo nyingi maudhui zake ni kuchochea anasa, uasherati, na wakati mwingine kuamini uchawi, tabia huathirika. Vitabu hivyo vinaharibu tabia njema uliyokuwa nayo, vinaharibu tabia nzuri, ambayo pengine Roho Mtakatifu alikuwa ameshaanza kuiimba ndani yako.

Hivyo ukitaka tabia yako isiharibike jihadhari na mambo hayo. Kama ni mwanaume kaa mbali na makundi au kampani mbaya au hatarishi. Nenda katika vijiwe kuhubiri injili, lakini si kusikiliza mambo yanayoendelea pale, au kushiriki mijadala yao. Kama ni mwanamke au binti, nenda vijiweni kuhubiri lakini si kwenda kusikiliza wala kushiriki kwenye mazungumzo yao.

Hebu tujifunze kutoka kwenye mfano mmoja kwenye Biblia kuhusu binti mmoja aliyekuwa na tabia nzuri, kuliko wenzake wote katika familia yao, lakini siku alipotoka na kwenda kukutana na mabinti wengine wa kidunia, akajikuta amebadilika tabia na kuwa mtu mwingine.

Msichana huyo ni yule binti wa Yakobo, aliyeitwa Dina. Katika biblia, Mwanzo 34:1: “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kwenda kuwaona binti za nchi. 2: Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri”.

Umeona chanzo cha Dina kuharibika tabia? Si kingine zaidi ya kutoka na “kwenda kukutana na mabinti wa kidunia”, ambao hadithi zao huenda ni kuzungumzia wanaume tu, na hadhi zao. Dina akiwa katika kusikiliza akajikuta ameshawishika na kujikuta anazini na mwana wa mfalme wa nchi, ambaye alikuwa ni mpagani. Jambo hilo lilikuwa baya sana, mbele za Mungu na mbele ya baba yake, Yakobo.

Sasa kujua Dina alikuwa ni binti wa tabia gani hapo awali, ni vizuri kujua yaliyopo kwenye maandiko ya Biblia.

Mwanzo 34:19 inasema “Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye”.

Kumbe, Dina alikuwa ni mwenye heshima kuliko wote kwenye familia, lakini ndiye aliyeharibika kuliko wote. Jambo linahuzunisha sana. Sasa kama mwana wa Yakobo, mrithi wa ahadi za Mungu aliharibiwa, wewe ni nani usiharibike? Kilichotokea kwa Dina kinaweza kutokea pia kwa binti ye yote.

Hivyo, kamwe usijivunie tabia yako, na kusema "hakuna mtu anayeweza kukubadilisha, wala hakuna chochote kitakachoweza kukubadilisha", na huku ni mtu wa kuzunguka katika vijiwe vibaya na mitandao. Fahamu kuwa Neno la Mungu halibahatishi, bali ni thabiti. Limesema “tukae mbali na mazungumzo mabaya ili tusiharibu tabia zetu”. Wewe na mimi hatuwezi kulisahihisha Neno la Mungu, na kusema “si mazungumzo yanayoweza kumbadilisha mtu, bali ni mtu mwenyewe ndio anayeweza kujibadilisha”, la hasha. Ndani ya mazungumzo kuna ushawishi.

Baadhi ya watu wanaorudi nyuma katika imani ya Kikristu ni kwa sababu hiyo. Wanazama katika kusikiliza na kushiriki mazungumzo mabaya na hatimaye wanajikuta tayari wameshapoa na kukana imani zao.

Hivyo, dawa ni pamoja na kukaa mbali na mazungumzo yote mabaya, au kinyume chake, tafuta mazungumzo mazuri ili ujenge tabia yako. Mazungumzo mazuri, utayapata kanisani, kwenye Biblia, na kwenye makala au vipindi vya Neno la Mungu.
 
Mazungumzo Mabaya na Tabia Njema
Katika maisha, kila mwanadamu ana tabia yake, malengo yake na mipango ya kufika kwenye malengo hayo. Pamoja na hayo, wanadamu hukutana, kuchanganyikana na kubadilishana mawazo. Katika hali hiyo, wengine wana uwezo wa ushawishi mkubwa kuliko wengine. Hiyo hutokea kutokana aidha na karama za mtu binafsi katika ushawishi, au nia njema au mbaya dhidi ya wanaomzunguka.

Unajua kuwa mazungumzo mabaya, huharibu tabia njema?

Kikristu, Biblia inasema katika 1Wakorintho 15:33: “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”. Haisemi kuwa “mazungumzo mabaya yanachochea tabia mbaya”, bali inasema “yanaharibu tabia njema”. Maana yake ni kuwa mtu mwenye tabia njema, na nzuri na inayovutia, anapoketi kuzungumza, au kusikiliza mazungumzo mabaya, kidogo kidogo anaanza kuiharibu ile tabia yake njema. Haijalishi, hatashiriki kwenye hayo mazungumzo, lakini hata kile kitendo cha kusikiliza tu, tayari akili yake hutafakari kinachozungumzwa, na tabia yake itaanza kuathirika. Ndiyo maana Biblia inatuonya tukae mbali na mazungumzo yote mabaya.

Mazungumzo mabaya ni yapi?
Haya ni mazungumzo yote yenye maudhui ya uzinzi, usengenyaji, umbea, wizi, au anasa na starehe za kidunia, na mengine ya aina hiyo. Kwa ujumla, ni mazungumzo yote yanayoenda kinyume na maandiko kwenye Biblia.

Baadhi ya njia ambazo mazungumzo mabaya hupatikana ni katika sehemu zifuatazo.

Kwenye Vijiwe
Vijiwe ni sehemu yoyote watu wanapokutana kujifurahisha kwa maneno, au michezo. Kwa mfano vijiwe vya watu wanaocheza michezo ya drafti, kamari au bao, wanaobashiri, au mipira, n.k.

Kwenye mitandao
Mtu anapotumia muda mwingi kukaa kwenye mitandao kama vile facebook, au whatsapp na mingine, anapojiunga kwenye makundi yasiyo ya neno la Mungu, au yasiyo na maana kwa maudhui ya kimaendeleo, hata kama hachangii chochote katika mijadala inayozungumziwa bali yeye ni msomaji tu, afahamu kuwa anaiharibu tabia yake njema.

Luninga
Unapotazama tamthilia za kidunia, pamoja na vipindi vingine vya kidunia na mijadala, na midahalo mbalimbali katika luninga, ambayo maudhui yake ni ya kidunia, fahamu kuwa unaingiza agenda mbalimbali akilini mwako, ambazo zinaweza kuharibu tabia yako njema. Hata kama wewe huchangii chochote, ni mtazamaji tu, bado tabia yako inaguswa na kuharibika taratibu.

Vitabu vya Simulizi
Unaposoma vitabu vya simulizi za kidunia, ambazo ni tungo za watu, ambazo nyingi maudhui zake ni kuchochea anasa, uasherati, na wakati mwingine kuamini uchawi, tabia huathirika. Vitabu hivyo vinaharibu tabia njema uliyokuwa nayo, vinaharibu tabia nzuri, ambayo pengine Roho Mtakatifu alikuwa ameshaanza kuiimba ndani yako.

Hivyo ukitaka tabia yako isiharibike jihadhari na mambo hayo. Kama ni mwanaume kaa mbali na makundi au kampani mbaya au hatarishi. Nenda katika vijiwe kuhubiri injili, lakini si kusikiliza mambo yanayoendelea pale, au kushiriki mijadala yao. Kama ni mwanamke au binti, nenda vijiweni kuhubiri lakini si kwenda kusikiliza wala kushiriki kwenye mazungumzo yao.

Hebu tujifunze kutoka kwenye mfano mmoja kwenye Biblia kuhusu binti mmoja aliyekuwa na tabia nzuri, kuliko wenzake wote katika familia yao, lakini siku alipotoka na kwenda kukutana na mabinti wengine wa kidunia, akajikuta amebadilika tabia na kuwa mtu tofauti.

Msichana huyo ni yule binti wa Yakobo, aliyeitwa Dina. Katika biblia, Mwanzo 34:1: “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kwenda kuwaona binti za nchi. 2: Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri”.

Umeona chanzo cha Dina kuharibika tabia? Si kingine zaidi ya kutoka na “kwenda kukutana na mabinti wa kidunia”, ambao hadithi zao huenda ni kuzungumzia wanaume tu, na hadhi zao. Dina akiwa katika kusikiliza akajikuta ameshawishika na kujikuta anazini na mwana wa mfalme wa nchi, ambaye alikuwa ni mpagani. Jambo hilo lilikuwa baya sana, mbele za Mungu na mbele ya baba yake, Yakobo.

Sasa kujua Dina alikuwa ni binti wa tabia gani hapo awali, ni vizuri kujua yaliyopo kwenye maandiko ya Biblia.

Mwanzo 34:19 inasema “Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye”.

Kumbe, Dina alikuwa ni mwenye heshima kuliko wote kwenye familia, lakini ndiye aliyeharibika kuliko wote. Jambo hilo linahuzunisha sana. Sasa kama mwana wa Yakobo, mrithi wa ahadi za Mungu aliharibiwa, wewe ni nani usiharibike?

Kamwe usijivunie tabia yako, na kusema "hakuna mtu anayeweza kukubadilisha, wala hakuna chochote kitakachoweza kukubadilisha", na huku ni mtu wa kuzunguka katika vijiwe vibaya, mitandao na kwingineko.

Fahamu kuwa Neno la Mungu halibahatishi, bali ni thabiti. Limesema “tukae mbali na mazungumzo mabaya ili tusiharibu tabia zetu”. Wewe na mimi hatuwezi kulikosoa Neno la Mungu, na kusema “si mazungumzo yanayoweza kumbadilisha mtu, bali ni mtu mwenyewe ndio anayeweza kujibadilisha”, la hasha. Ndani ya mazungumzo kuna ushawishi.

Baadhi ya watu wanaorudi nyuma katika imani ya Kikristu ni kwa sababu hiyo. Wanazama katika kusikiliza na kushiriki mazungumzo mabaya na hatimaye wanajikuta tayari wameshapoa na kukana imani zao.

Hivyo, dawa ni kukaa mbali na mazungumzo yote mabaya, au kinyume chake, tafuta mazungumzo mazuri ili ujenge tabia yako. Mazungumzo mazuri, utayapata kanisani, kwenye Biblia, na kwenye makala au vipindi vya Neno la Mungu.
 
Mazungumzo Mabaya Huharibu Tabia Njema
Katika maisha, kila mwanadamu ana tabia yake, malengo yake na mipango ya kufika kwenye malengo yake. Pamoja na hayo, wanadamu hukutana, kuchanganyikana na kubadilishana mawazo. Katika hali hiyo, wengine wana uwezo wa ushawishi mkubwa kuliko wengine. Hiyo hutokea kutokana aidha na karama za mtu binafsi katika ushawishi, au nia njema au mbaya dhidi ya wanaomzunguka.

Je, unajua kuwa mazungumzo mabaya, yanaharibu tabia njema?
Kikristu, Biblia inasema katika 1Wakorintho 15:33: “Msidanganyike; mazungumzo mabaya huharibu tabia njema”. Hapo haisemi, “mazungumzo mabaya yanachochea tabia mbaya”, bali inasema “yanaharibu tabia njema”. Maana yake ni kuwa mtu mwenye tabia njema, na nzuri na inayovutia, anapoketi kuzungumza, au kusikiliza mazungumzo mabaya, kidogo kidogo anaanza kuiharibu ile tabia yake njema. Haijalishi, hatashiriki kwenye hayo mazungumzo, lakini hata kile kitendo cha kusikiliza tu, tayari akili yake hutafakari kinachozungumzwa, na tabia yake itaanza kuathirika. Ndiyo maana Biblia inatuonya tukae mbali na mazungumzo yote mabaya.

Je, mazungumzo mabaya ni yapi?
Haya ni mazungumzo yote yenye maudhui ya uzinzi, usengenyaji, umbea, wizi, au anasa na starehe za kidunia, na mengine ya aina hiyo. Kwa ujumla, ni mazungumzo yote yanayoenda kinyume na maandiko kwenye Biblia.

Baadhi ya njia ambazo mazungumzo mabaya hupatikana ni katika sehemu zifuatazo.

Kwenye Vijiwe
Vijiwe ni sehemu yoyote watu wanapokutana kujifurahisha kwa maneno, au michezo. Kwa mfano vijiwe vya watu wanaocheza michezo ya drafti, au bao, wanaobashiri, au mipira, waendesha bodaboda, n.k.

Kwenye Mitandao
Mtu anapotumia muda mwingi kukaa kwenye mitandao kama vile facebook, au whatsapp na mingine, anapojiunga kwenye makundi yasiyo ya neno la Mungu, au yasiyo na maana kwa maudhui ya kimaendeleo, hata kama hachangii chochote katika mijadala inayozungumziwa, yeye ni msomaji tu, afahamu kuwa anaiharibu tabia yake njema.

Luninga
Unapotazama tamthilia za kidunia, pamoja na vipindi vingine vya kidunia na mijadala, na midahalo mbalimbali katika luninga, ambayo maudhui yake ni ya kidunia, fahamu kuwa unaingiza agenda mbalimbali akilini mwako, ambazo zinaweza kuharibu tabia yako njema. Hata kama wewe huchangii chochote, ni mtazamaji tu, bado tabia yako inaguswa na kuharibika.

Vitabu vya Simulizi
Unaposoma vitabu vya simulizi za kidunia, ambazo ni tungo za watu, ambazo nyingi maudhui zake ni kuchochea anasa, uasherati, na wakati mwingine kuamini uchawi, tabia huathirika. Vitabu hivyo vinaharibu tabia njema uliyokuwa nayo, vinaharibu tabia nzuri, ambayo pengine Roho Mtakatifu alikuwa ameshaanza kuiimba ndani yako.

Hivyo ukitaka tabia yako isiharibike jihadhari na mambo hayo. Kama ni mwanaume kaa mbali na makundi au kampani mbaya au hatarishi. Nenda katika vijiwe kuhubiri injili, lakini si kusikiliza mambo yanayoendelea pale, au kushiriki mijadala yao. Kama ni mwanamke au binti, nenda vijiweni kuhubiri lakini si kwenda kusikiliza wala kushiriki kwenye mazungumzo yao.

Hebu tujifunze kutoka kwenye mfano mmoja kwenye Biblia kuhusu binti mmoja aliyekuwa na tabia nzuri, kuliko wenzake wote katika familia yao, lakini siku alipotoka na kwenda kukutana na mabinti wengine wa kidunia, akajikuta amebadilika tabia na kuwa mtu mwingine.

Msichana huyo ni yule binti wa Yakobo, aliyeitwa Dina. Katika biblia, Mwanzo 34:1: “Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka kwenda kuwaona binti za nchi. 2: Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi, mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye, akambikiri”.

Umeona chanzo cha Dina kuharibika tabia? Si kingine zaidi ya kutoka na “kwenda kukutana na mabinti wa kidunia”, ambao hadithi zao huenda ni kuzungumzia wanaume tu, na hadhi zao. Dina akiwa katika kusikiliza akajikuta ameshawishika na kujikuta anazini na mwana wa mfalme wa nchi, ambaye alikuwa ni mpagani. Jambo hilo lilikuwa baya sana, mbele za Mungu na mbele ya baba yake, Yakobo.

Sasa kujua Dina alikuwa ni binti wa tabia gani hapo awali, ni vizuri kujua yaliyopo kwenye maandiko ya Biblia.

Mwanzo 34:19 inasema “Na yule kijana hakukawia kulifanya neno lile, maana amependezewa na binti Yakobo, naye alikuwa mwenye heshima kuliko wote nyumbani mwa babaye”.

Kumbe, Dina alikuwa ni mwenye heshima kuliko wote kwenye familia, lakini ndiye aliyeharibika kuliko wote. Jambo linahuzunisha sana. Sasa kama mwana wa Yakobo, mrithi wa ahadi za Mungu aliharibiwa, wewe ni nani usiharibike? Kilichotokea kwa Dina kinaweza kutokea pia kwa binti ye yote.

Hivyo, kamwe usijivunie tabia yako, na kusema "hakuna mtu anayeweza kukubadilisha, wala hakuna chochote kitakachoweza kukubadilisha", na huku ni mtu wa kuzunguka katika vijiwe vibaya na mitandao. Fahamu kuwa Neno la Mungu halibahatishi, bali ni thabiti. Limesema “tukae mbali na mazungumzo mabaya ili tusiharibu tabia zetu”. Wewe na mimi hatuwezi kulisahihisha Neno la Mungu, na kusema “si mazungumzo yanayoweza kumbadilisha mtu, bali ni mtu mwenyewe ndio anayeweza kujibadilisha”, la hasha. Ndani ya mazungumzo kuna ushawishi.

Baadhi ya watu wanaorudi nyuma katika imani ya Kikristu ni kwa sababu hiyo. Wanazama katika kusikiliza na kushiriki mazungumzo mabaya na hatimaye wanajikuta tayari wameshapoa na kukana imani zao.

Hivyo, dawa ni pamoja na kukaa mbali na mazungumzo yote mabaya, au kinyume chake, tafuta mazungumzo mazuri ili ujenge tabia yako. Mazungumzo mazuri, utayapata kanisani, kwenye Biblia, na kwenye makala au vipindi vya Neno la Mungu.
Amina
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom