Kwa taarifa za kuaminika Ukraine anavamiwa sio muda na Urusi

Masamila

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
6,411
7,306
Kwa mujibu wa gazeti la muda mrefu sana na la kuaminika sana la New York Times , Russia anadaiwa kumaliza kujiandaa kuivamia nchi ya Ukraine ambapo ipo nafasi kubwa kuzuka vita kubwa sana ikihusisha mataifa mengi

Madai ya Russia kwa Ukraine mojawapo ni unyanyasaji wa Ukraine kwa raia wa Ukraine wenye asili ya kirusi katika ardhi ya Ukraine ndani ya majimbo kama Donbass na mengineyo

Gazeti la New York Times limeeleza pia kuwa taarifa za serikali za kijasusi za serikali ya Marekani zinasema kuwa Russia ameandaa jeshi la Wanajeshi laki moja na elfu sabini na tano (175,000) na silaha nzito ardhini na angani karibia na mpaka wake na Ukraine

Mengineyo Kutoka katika ripoti hiyo hiyo ya New York Times ni kwamba Russia ndani ya mwezi ujao au miezi miwili ijayo anaivamia Ukraine

------UPDATE as of 26th December 2021--------

Kingine kitakachomponza Ukraine ni Upanuzi wa Nato kuelekea mipaka ya Urusi

Mcheki hapo chini Putin akiongea kwa jazba na hasira

Updates as of Jan First 2022:

Mgogoro waelekea kubaya zaidi na siku chache zilizopita PM wa Uingereza aliliambia bunge kuwa Russia akiivamia Ukraine basi Nato itachukua hatua ya kuyapeleka majeshi ya Nato mipakani mwa Urusi

Urusi hataki majeshi ya NATO yawe karibu yake kama ambavyo Marekani hakutaka makombora ya Soviet yawe karibu yake nchini Cuba ile 1961 na chanzo cha Cold War.

NATO inamzunguka Urusi kona nyingi na kashaamua lolote na liwe kwa Ukraine. Kina Georgia nao walitaka hivyo hivyo, Ukraine baada ya kuondoshwa Rais Viktor Yanukovichy kwa maandamano ya Maidan Square, ambaye alikuwa pro-Russian tangu hapo Russia alisema nchi haikaliki. Sera za waliofuata wote kina Alseniy Yatsenyuk zilikuwa kukaribisha majeshi ya NATO kwanza na kufanya mchakato wa Ukraine kujiunga na NATO.

Urusi kaanzisha War in Donbass kuitenga Ukraine ili upande jirani yake uwe kibaraka wake na hivyo iwe buffer endapo upande wa Ukraine utakuwa NATO. Pale Donetsk region ndio mstari wa maili 250 wa kutenga usio rasmi upo. No man's land iko na kama mita 25 tu na snipers wa separatist wanashambulia wanajeshi wa Ukraine ili kuwachokosha wajibu mashambulizi na vita ianze hapo.

Russia inasemekana anaweza vamia mwezi January, dalili za kuvamia mwezi huu hamna. Nowadays patrol aircrafts za NATO zinazurula mpakani na Russia hasa upande wa majini na zinarudishwa na Russian Airforce.
 
Putin kwisha na ujamaa unaelekea kuzikwa kwann Ukraine anaingia umoja wa ulaya hivyo nipenyezo au langu la babylon kusambaratisha udikiteta wa mwamba Putin ...tusishangae 10 years later democrasia ,Law and reasonings zinatamalaki urusi ,naona urusi mpya
 
Sasa Ukraine kuingia NATO na Urusi kuwa na demokrasia vina uhusiano gani? Au hujui mipaka ya Ukraine.
Na hiyo Babylon inahusiana vipi na eneo la hizo nchi mbili? Babylon iko Iraq ya sasa, hakuna ukaribu wala uhusiano wowote
 
Ili unielewe nilichosema nilazima ufikirie zaidi kwann urusi amekua mbogo ukraine kujihusisha nakujiunga na umoja wa ulaya ,ukigundua Hilo ndipo utaelewa kua ahaaa kumbe...umenielewa mkuu
 
Putin kwisha na ujamaa unaelekea kuzikwa kwann Ukraine anaingia umoja wa ulaya hivyo nipenyezo au langu la babylon kusambaratisha udikiteta wa mwamba Putin ...tusishangae 10 years later democrasia ,Law and reasonings zinatamalaki urusi ,naona urusi mpya
Kesho Putin akitangaza kuweka vikosi vya jeshi na makombora yake pale Cuba msije mkaanza kulia Lia.
 
Back
Top Bottom