Kwa staili hii, CHADEMA itavunja muungano

Sasa kanda na mikoa huoni kanda zinaweza kuwa chache zaidi ya mikoa? mikoa ndio kugawana vyeo, kanda vyeo ni vichache
 
Hizi sikukuu ndo zinaongeza umasikini wa nchi yetu, Kwa Bara zima la Africa Tanzania ndo inaongoza kwa kuwa na Public Holiday nyingi sana,
Na hapo uwanjani sioni cha maana zaidi ya ngoma na magwaride, yamepia masaa mengi lakini hakuna cha maana hapo,
 
Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka endapo wataendelea kuwa kwenye muungano.

Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

CHADEMA inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

Yaani umeniudhi, unasema upuuzi wa utanganyika? una maana gani. Unajua unachozungumza, usitutusi tafadhali.
 
Wanzanzibar wanalalamika kuhusu muungano wa bara nao hivyo hivyo basi uuvunjwe tuone nani atakae uumia
 
Mkishavunja muungano mtaanza kubagua kwa ukanda, udini na mwishoni ukabila. Ndio maana mimi bado naamini kifo cha chadema ni bora kuliko kifo cha mama Tanzania.

Mbona ubaguzi wa ki-CCM huuzungumzii? Ila afadhali wabakie na ubaguzi wao maana kuwa na ushirika na ufisadi, fitina na umbea uliopo ccm HAIKUBARIKI
 
Yaani umeniudhi, unasema upuuzi wa utanganyika? una maana gani. Unajua unachozungumza, usitutusi tafadhali.

Uzanzibari na utanganyika ni upuuzi sawa na ukaburu na watetezi wao ni wabaguzi sawa na wale wazungu wa Afika kusini waliokuwa wanabagua waafrika kwa rangi.
 
Mkishavunja muungano mtaanza kubagua kwa ukanda, udini na mwishoni ukabila. Ndio maana mimi bado naamini kifo cha chadema ni bora kuliko kifo cha mama Tanzania.

Sioni faida yeyote ya muungano, zaidi ni ujinga wa maneno ya kejeli dhihaka na dharau dhidi ya wabara. Hatusemi lkn tunajua kila kitu. Wabara si wapiga porojo kama hao.
 
mara zote mafisadi mmegoma kusikia ukweli kwn huwachoma kama ncha ya mkuki; alichosema Lisu ndio ukweli japo ww na wengine wenye manufaa na muungano hewa hamtapendezwa
 
wanajf katika sherehe za muungano zinazoendelea hapa uwanja wa uhuru sijaona kiongozi wa Chadema hata mmoja, kuna akina Cheyo,Lipumba hii imekaaje?
Unamaana gani unasema hujaona kiongozi hata mmoja mbona mimi nipo? au ulitarajia nani awepo hata mwenye kiti wa kitpogoji kupetia chadema nae ni kiongozi wa chadema.....
 
Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka endapo wataendelea kuwa kwenye muungano.

Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

CHADEMA inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

Mkuu, naomba nikuulize? Watokea upande upi wa Tanzania.
Siamini kwamba mtu mwenye akili zake timamu anaweza kutamka au kuandika maneno hayo niliyoyatilia rangi nyekundu.
Unathubutu kuuita Utanganyika upuuzi!!!!?????.
 
Ndiyo hao wasio na uwezo wa kutafakari. Hivi kusema watanzania kuamua waamue namna ya muungano wanaoutaka ni kuvunja muungano au ni kutaka kuimarisha Muungano. Ndiyo hao mtoto akimwambia Baba naona ule mpamgo wa kutaka kununua gari uubadirishe badala yake tujenge nyumba mjini inaweza kutufaa zaidi, ataanza kumshambulia mtoto kwa maneno mengi ya kashfa, naona unampango mbaya na mama yako, huna adabu, hufai wewe wewe... badala ya kumuuliza mtoto hivi kwanini unapendekeza hivyo ili kusikia mawazo yake. Tubadilike, hatuwezi kijipendekeza kwa Nyerere kwa njia hiyo bali na tujipendekeze kwa kuwa waadilifu na kuhakikisha kila siye mwadilifu anaondloewa kwa nguvu ya Umma. Ground zero don't be zero in thinking.
 
wanajf katika sherehe za muungano zinazoendelea hapa uwanja wa uhuru sijaona kiongozi wa Chadema hata mmoja, kuna akina Cheyo,Lipumba hii imekaaje?

Ulikua na shida na nani wa cdm wesheherekea muungano wako ambaa zako kama una shida na cdm njoo ofisini alah! We wa wapi?
 
Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka endapo wataendelea kuwa kwenye muungano.

Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

CHADEMA inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

Ground Zero,

Wewe umefuatilia mijadala katika Baraza la Wakilishi, Zanzibar? Umesahau kwamba Wazanzibari kadhaa wamediriki hata kwenda UN New York (Umoja wa Mataifa) kudai nchi yao iwe huru? Umesahau mijadala kuhusu gesi na mafuta, kama maliasili ya nchi?

Kwa nini Chama kinachonuia kuunda Katiba endelevu kisiwe na mtu mchambuzi atakayezungumzia haya? Sasa ni wakati wa kuchambua Katiba ya sasa ili tuweze kuunda katiba mpya. Viongozi makini, jasiri na wa ukweli kama Tundu Lissu ndiyo wanatakiwa wajitokeze.

Unafiki uwe mwiko kwa Watanzania wa kweli.
 
Muungano hauna issue na huko kwa maslahi ya Magamba tu...kurubuni watu.
 
Sioni faida yeyote ya muungano, zaidi ni ujinga wa maneno ya kejeli dhihaka na dharau dhidi ya wabara. Hatusemi lkn tunajua kila kitu. Wabara si wapiga porojo kama hao.
Sija wahi kuona faida za muungano kwa watanganyika zaidi ya kuumia kuhudumia mijitu kutoka Zanzibar..
 
Nimemsikiliza kwa makini sana waziri kivuli wa wizara ya katiba na sheria Mh. Tundu Lissu.

Nilisikitishwa sana na kauli ya Lissu kwamba Zanzibar iamue ni aina gani ya muungano wanataka endapo wataendelea kuwa kwenye muungano.

Hii ni kauli hatari kwa maslahi ya taifa letu. Mwalimu alishawahi kusema kwamba viongozi walifilisika hutafuta kujihalalisha kwa makundi.

CHADEMA inataka kujihalalisha kwa upuuzi wa utanganyika, tuwakatae hao jamani!

hahaha! Kwa iyo we si mtanganyika? No wonder unatumwa na kina nape.
 
Back
Top Bottom