watu wanakodi magari ya wazi yenye maspika na watu wanaserebuka mji mzima. kuoa kumekua complex mno. kwanza sendofu na utoaji wa mali ni harusi tosha kwa jinsi wanavyozikocompleksisha.Kinachoniboa ni hii culture ya michango jamannii,si tulage dinner tu hivi watu wachache afu basi
Haaaa...Sawia kabisa, wengine tunaolewa ili kutoa nuksi tu.
Hatujajiandaa na maisha ya kindoa
Asante kwa mawazo mazuri.Nakubaliana na wewe mkuu kwa asilimia zote,watu wanafikiria Ndoa ni lele mama,mie ningejua mwanzo Ndoa ikoje mbona ningesema basi staki tena,kama hukujikaza wallah hukai hata miezi 6,manake baada ya ndoa tuu ndio ma buzi ndio yatakua mengi mpaka unajiuliza jamani mlikua wapi mwanzo,kwa upande wa mume nae Totoz wanajileta mpaka unasikia kichefuchefu,upande wa pili kuna ma wifi na na mashemeji wana midomo na maneno makali utadhani wao hawana watoto au hawana mume/mke, lakini chamsingi bora hizo hela za mchango ukalipie japo kodi ya nyumba na usitake harusi kubwa
kwanza hapo kwenye harusi unaweza ukapa mtu akakutonya "yule alovaa nguo ya red anaecheza sana ndio mwanamke wake
na yeye ndio kamualika aje akuone tena kaja na wapambe wake wakuthamini kama unamfikia uzuri" hapo bi harusi picha lazima zitoke kama analia...
Ni kweli.Ndoa ni mpango wa Mungu, akili na mawazo ya Mungu hayachunguziki hivyo sioni sababu ya kujiuliza saaaaaana, let's me do my best and God will do the rest.
aseee... asante kwa mawazo.Ndoa ni wito hahaaa manake km huna wito unaoa/unaolewa ijumaa jumatatu taraka
Heeee...Haaaa...
Asante kwa maoni.Hata ukikaa na kufikiri miaka mia, haibadilishi changamoto zilizopo kuhusu maisha ya wawili.
..niwaze kuhusu watoto, kwani anayeleta watoto ni mimi au Mungu? Nitafanya lillilo chini ya uwezo wangu then Mungu atanipa kwa kadri apendavyo.
..niwaze kuhusu maradhi, hata nikiwa peke yangu, bado naweza kuumwa au kupata changamoto ya kiuguza ndugu au mzazi.
Kupata mtu anayefikiria ndoa zaidi ya sherehe ndio changamoto mliyonayo vijana ambao hamjaoa/kuolewa, mtu anayedhani kuwa maisha kwa ujumla wake ni "rollercoaster", kuwa kuwa na pesa, magari na nyumba "as you call it bonus" ni utimilifu wa ndoa. Maisha ya ndoa is more than that. Again even the one you think is your soul mate can put you to h3ll, hata muishi miaka mia kwenye uchumba, majaribu ni LAZIMA!!
Usiogope ndoa.Kati ya vtu ninavoviogopa ni ndoa nikiona watu walioolewa na kuoa wanavoteseka. Mwanaume anaoa michepuko daily migogoro. Nadhani before entering kwenye marriage lazima kujiandaa kiakili kimwili na kiroho na kuacha mambo yote na kuwa committed haswa pia kuwa na hofu ya Mungu bila hivo aisee
Ukitamani kufa kwa ishu ndogo kama hiyo ujue bado hujiamini. Angekuwa mzuri sana si angeolewa yeye?Umeona eeeeh! Binadamu wengine nuksi huko kote hawajasema pale ndio wanapokutia jiti la Roho ukatamani kufa..
Well said mkuuNDOA KWANINI HAZIDUMU SIKU HIZI
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa obssesed na wedding ceremony imaginations, bila kujua ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna ndoa na kuna harusi...
Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni suti kali, boonge la shela kutoka Uturuki, make up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, mashosti kuingia ukumbini na wimbo wa selfie,wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.
Je, Umewahi kuwaza?
1. Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?
2. Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?
3. Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya mama mkwe na mawifi kwamba unawajazia choo cha kaka yao na huna kizazi?
Ndoa ni zaidi ya sherehe ya harusi. Baada ya yale matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni majukumu mazito na kiapo kisichovunjika.
Achana na fantasy za kwaito,waza mbali kidoogo.
Je, Uko tayari kuwa mme au mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako?
Huwa mnawaza hayo au mnawaza zawadi ya kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?
Sidhani kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,unatamani ndoa au ni tamaa ya sherehe ya harusi?
Asante sana.Very good posts. It is More educative.
Asante sana kwa maoni mazuri.Kimsingi ndoa ni jambo jema na lenye kuleta faraja kubwa sana maishani kwa wana ndoa. Mambo sio mabaya kama hivyo yanavyotiwa chumvi, kuna ndoa nyingi zimedumu kwa upendo, furaha na amani. Asiliamia kubwa ya wana ndoa wana maisha bora zaidi kuliko waliyokuwa nayo kabla kuoa au kuolewa. Ndoa zimewafanya wamekua kiakili na kutambua majukumu kimaisha katika jamii. Kuoa au kuolewa kunatimiza misingi mikuu ya maisha ya mwanadamu. Ndio kuna changamoto za hapa na pale hazikosekani lakini hiyo ni kawaida ya maisha, bila changamoto hakuna maisha, changamoto zinatufundisha kukomaa na kujenga ukaribu wa wanandoa, hata ukiishi na wazazi, ndugu lazima mikwaruzano ya hapa na pale ijitokezee, huwezi kuacha kuishi kwsabababu kuna matatizo katika ndoa. Ndoa moja ya ndugu au rafiki kuwa mbaya au kuvunjika haina maana kwamba 'Ndoa Hazidumu Siku Hizi' na kupelekea kuchochea mawazo mabaya kuhusu ndoa. Inasikitisha kuona vijana wengi wakiwa na mawazo hasi kuhusu ndoa wakati wala hawajaingia katika ndoa. Ni faraja ilioje unaporudi nyumbani kwako jioni baada ya siku ndefu na ngumu kazini unakuta angalau kuna mwenzako wa kumshirikisha jinsi siku yako ilivyoenda leo. Tuitazame ndoa kwa mapana na marefu na sio kirahisi rahisi tu na kejeli. Wanaokejeli ndoa hebu wajiulize wao wangekuwa wapi leo kama taasisi hii ya ndoa isingekuwepo.