Kwa rasimu hii, CCM inakufa


kama kweli ni mzima huumwi wakati unaandika unafikiri hii ni hoja ya kubadili sura ya siasa kwa ujumla tuombe mungu atupe uzima bado mda kidogo tu mtakuja mkimbiane watu hawaongei mambo yaliyopita wanatafakari maisha mapya wewe mkuu vipi kwa mwendo wa mawazo haya utataabika siku ikifika.
 

Ni kweli umenena yote. Na hivi vyama vidogodogo vina kazi kama havitaki kujiuza kwa wabongo.
 
Maana yake ni kwamba, imagine Lowassa anaangushwa na Sitta. Watu wengi wa Lowassa walikuwa tayari kumpigia kura mgombea wa chama kingine kuliko kumpa Sitta au vice versa.

Lakini kwasasa wanaweza kuhama na Lowassa akiamua kugombea kama binafsi. Watagawa kura za CCM lakini pia wataondoa zile kura za wapenzi wa Lowassa ambao wangelikuwa tayari kumuunga mkono mgombea wa kiti cha upinzani.

Chukulia mifano ya ubunge Iringa na Arusha. Imagine Arusha Mrema angegombea kama mgombea huru, chance ya Lema kushinda ingelikuwa ndogo sana. Hivyo hivyo Iringa, huenda Mwakalebela angeshinda kama mgombea huru.

Mfano mzuri ni uchaguzi wa Malawi ambao kwa vipindi viwili umetoa Wabunge huru wengi sana

Yaani waondolewe CCM kwa kuonewa then wagawe kura za upinzani how!. Imagine Lowassa afanyiwe mizengwe halafu agombee kama mgombea binafsi unategemea kura za CCM zitabaki zilezile.
 
Rasimu bado ni skeleton sana,haijsema kama kutakuwa na rais wa tanganyika,siungi mkono suala la mgombea binafsi kwasababu nafuata misingi sio watu.naogopa kuwa na kiongozi asiye na discipline na uoga wa mamlaka ya kitaasisi,naogopa kuwa na kiongozi asiye na kanuni na taratibu zinazomsimamia katika utekelezaji wa majukumu yake,naogopa zaidi kuwa na kiongozi anayeongoza kwa muono wake na mkewe,ni hulka ya binadamu kupenda uhuru ili afanye maovu.
 

Mkuu, hunijui, sikujui, matusi ya nini?
 
Matola siwezi kuomba radhi kwa sababu niko sahihi kwa hiki ninachokisema.

Bila kujali hoja ya mgombea binafsi niya nani. CCM katika kuwasilisha maoni yao kama chama katika tume, walipendekeza wagombea binafsi watambuliwe kwenye katiba mpya. I'm 100% sure pamoja na kwamba kichocheo alikuwa ni Mtikila.

Hoja ya serikali tatu lilikuwa niya CHADEMA katika mapendekezo yao kama chama kwenye tume lakini siyo kwamba CCM hawakulitaka hili. CHADEMA wamewalahisishia CCM kupata kile walichokuwa wanakitafuta kwa muda mrefu. Serikali tatu ingekuwa tayari zipo kama isingekuwa Mwl. Nyerere kulia na kuandika kitabu cha uongozi wetu na hatima ya Tanzania. Malecela mpaka leo hana hamu tena na Mwl. Nyerere so as G55.

Mahakama ya kadhi inakuja kwa njia ambao huwezi kuamini. comment ya Mzee Warioba kuhusiana na hili, inasema zaidi ya neno alilolitamka na hii itakuwa ndiyo kete kwa CCM katika chaguzi zijazo. Warioba amesema swala la mahakama ya kadhi siyo la muungano na nchi ya Tanganyika wanapaswa wajifunze kutoka Zanzibar ambako kuna mahakama ya Kadhi. Umeipata hiyo?

Tukubali kutokubaliana.
 
Mungu atatuongoza kuona ccm inaingia kzburini yenyewe
 

Jackton rasimu inazungumzia mgombea binafi kwa nafasi ya urais tu weye umesoma rasimu gani? Ndio maana unaandamwa!

Kuna Serikali za Shirikisho ambazo imependekezwa zitakuwa na katiba zake, yaani serikali ya Mapinduzi na Tanzania bara.

Labda cha kuiuliza tume ni hierachy ya ungozi wa serikali washirika na utambulisho wao ktk shirikisho maana kama tuna Rais wa Shirikisho na ambaye atakuwa amiri jeshi mkuu viongozi wa juu bara na visiwani wataitwaje?
 
Bado sijaona cha kufurahia ikiwa wakuu wa mikoa na wilaya wataendelea kutusulubu kwa mgongo wa katiba!!! Yaani rais=mkuu wa mkoa=mkuu wa wilaya,mkuu wa mkoa=mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mkoa ambaye ni=na supreme judge wa mkoa ambaye pia ni mwenezi wa chama CHAKE mkoani,yaani ambaye ni ADUI wa ADUI wa chama chake,hili ni tundu kubwa sana,ukizingatia tanzania imegawanywa kimikoa,wilaya nk na kote huko ma supreme judge hawa wataendelea kuwepo na kuendelea ku determain future ya wananchi wa huko,laana bado ipo mezani!! Hakuna cha kujifariji hapa.
 

Hao watoa rushwa nje ya vyama ni rahisi kuwadhibiti kuliko walio ndani ya chama. Kwa CHAMA CHA MAPINDUZI kwa sababu yeye ndiye alikuwa mdhibiti na mtoa rushwa ilikuwa rahisi kwao kutoa kirahisi. Sheria tulizonazo katika habari za rushwa katika uchaguzi ni nzuri sana lakini msimamizi ambaye ni CHAMA CHA MAPINDUZI mwenyewe alizifumbia macho ili aziruke.
 

Unajua hao wafuas wa Lowasa inaweza kufika wakatambua kuwa kuna suala la UTAIFA kwanza hivyo mwishoni wanaweza mgeuka hata mambo ya kanisani sijui kama ni turufu ya moja kwa moja ya kumfanya yeye ashinde kwa sabab kuna watu wa dini ya kiislamu wanaweza wasimuunge mkono na hata walioko upinzan pia hivyo hilo la kampen makanisani linaweza mfelisha! Suala la mgombe binafsi hata upinzan linaweza kuwaathir kwa sabab hakutakuwa na ongezeko la wanachama kama ilivyokuwa imezoeleka kwamba mtu anatoka ccm anaenda upinzan na wao kuongeza wanachama. Suala hili litaondoa haya mambo ya uvyama na watu watakuwa wanachagua zaid mtu na sifa zake,hivyo hili litaleta uwajibikaji kwa watu wote bila kufungamana au kutetea maslah ya chama. Asante bwana Manyerere kwa hoja yako japo kuna watu walikushambulia sana hapo mwanzo.
 

Kwa kuwa bado ni Draft tusubiri tuone final product itakuwaje. Watu walikuwa na wasiwasi Rasimu itakuwaje lakini imekuja na mapendekezo ambayo ukiyaangalia unaona kabisa kwamba watu wameandaa kitu ambacho nia ni kuwa na level playing field. Kazi itakuwa kwa Vyama kuchakarika katika kujiuza kwa Wapiga kura na kuacha ulaghai wa kisiasa. Siyo CCM tu bali ni Vyama vyote kufanya homework kwa umakini zaidi. Tuombe tu kuwa at the end of the day tupate Katiba bora.
 
Tatizo siyo sheria kufumbiwa macho. Tatizo wasimamizi wa sheria ndiyo wala rushwa.

Sijaamini bado kama Tanzania ina sheria za kudhibiti rushwa inayotokea kwenye wagombea binafsi. let's put in this way. Hivi unafahamu kama kuna uwezekano wa nchi fulani ku-sponsor mtu/watu kuwa wagombea ili baadaye waingie serikalini au bungeni na kulipa fadhira kwa kufanya mambo ambayo hayana maslani kwa wananchi bali kwa sponsor wao.

Tunaweza kupata hata Rais wa aina hii.
 

Wanaomrushia matusi Manyerere ni hao hao maccm wamekasirika sana. Sijuiwataipigia kura?
 

haupo arusha mjini wewe,umeandika upuuzi.MREMA hajawahi shinda zaidi ya ubingwa wa wizi wa kura.LEMA hata angesimamisha na nani mwaka 2010 na 2015 atapeta kiulaini.LEMA mashine ingine
 



Ukurasa wa 5 wa Hotuba ya Jaji Warioba unasema, "Tume imependekeza mgombea binafsi aruhusiwe". Akatoa ufafanuzi wa nyongeza kwamba inapendekezwa mgombea binafsi kuanzia Kitongoji hadi urais. watu wakapiga makofi. Kasema kama mtu ana haki ya kupiga kura, ni haki pia akapigiwa kura, ingawa kipengele hicho kimepigwa ngwala kwenye urais!
 
Wewe nawe unajifanya Mwandishi lakini uandishi wako uko shallow kupita maelezo.

Nyie ndio maripota wa matukio halafu mnajiita wandishi.

Imekuuma sana hii, na bado. Miti imeanza kuteleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…