Kwa Rais huyu, CCM wana hali mbaya sana!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Ilinichukua miezi mitano kufahamu kuwa Rais Samia hana maisha marefu ya kisiasa kwa sababu hana karama, kipaji na ujuzi wa uongozi.

Unaweza kuukataa ukweli lakini hata kama ukiukataa hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere aliwahi kusema, “Ukweli una tabia moja nzuri sana, haujali mkubwa wala mdogo, hujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa. Ukiniona nataka kupiga teke jiwe kwa kuwa unafikiri kuwa ni dongo au mpira, natumaini utanionya. Lakini nikilipuuza onyo lako kwa sababu eti wewe ni mdogo au kwa sababu sikupendi, nikalipiga teke, basi litanivunja dole japo ningekuwa nani. Ukweli haupendi kupuuzwapuuzwa”.

Rais Samia kwa sasa hakubaliki nchini lakini kibaya zaidi hakubaliki ndani ya kundi kubwa la watu wenye maisha ya chini ambao ni wengi nchini na hutumiwa kama “kete” ya CCM katika chaguzi.

Rais Samia amebandika mabango ya kujitangaza nchi nzima lakini kinyume chake watu wakiyaona wanaanza kuyatukana!

Sakata la kuwapa DP-World bandari zetu limekuwa ndio msumari wa mwisho katika kaburi lake la kisiasa baada ya kuwabambikia wananchi tozo mbalimbali.

Ndani ya CCM wameanza kukubali kuwa hali ni mbaya sana mpaka wameamua kuanza ziara za “kuwatongoza” wananchi hasa wa kupato cha chini huku wakisema eti Rais hawezi “kuiuza” nchi.

Katika hali ya kutapatapa wameanza kutumia mbinu ya udini ili kugusa hisia za imani ya dini angalau kundi la watu lenye mlengo wa dini yake lianze kumuunga mkono hasa kundi la watu wa kipato cha chini ambalo halitaki hata kumsikia.

Kinachowashitua zaidi ndani ya CCM ni kuona kuwa juhudi zote za kuwaleta ndani ya utawala wake wapinzani hasa CHADEMA katika “dhana ya kujenga umoja” haijazaa matunda endelevu na badala yake wananchi wa kipato cha chini hawataki hata kumsikiliza achilia mbali kumuona.

Ukiwauliza wananchi wengi kama wanakumbukumbu ya jambo lolote ambalo Rais Samia amelifanya na hawawezi kumsahau watakuambia ni tozo na kugawa bure raslimali zetu za Taifa.

Hotuba zake husahaulika pindi anapomaliza kutoa hotuba. Nadhani hata mawaziri wake ukiwauliza baada ya hotuba yake hawawezi kukumbuka alichokisema! Garbage in, garbage out.

Mikutano yake ya barabarani kwa sasa inakuwa na magari mengi zaidi ya wananchi ukiondoa wale wanaovalishwa nguo za CCM!

Historia nchini huonyesha kuwa Rais huanza kuchokwa na kuchukiwa katika kipindi cha pili cha utawala wake lakini Rais Samia imemchukua miaka miwili tu kuchukiwa na wananchi wengi.

Kwa jinsi hali ilivyo mbaya kuna uwezekano mkubwa Rais Samia akawa ni Rais wa kipindi kimoja katika historia ya Tanzania kwa sababu katika nchi yoyote wanaoleta mabadiliko ni watu wa kipato cha chini ambao kwa sasa hawataki hata kumsikia.
 
Mimi ni CCM lakini siwezi kumpa Mama kura yangu! HATOSHI!
Mwenyewe yeye CCM? Watanganyika hamutujuwi Wazanzibari. Huyo ni mtoto wa Amani Karume, muanzilishi wa UAMSHO avunjie muungano, alosema nyie CCM vichwa vya Samaki. Je unamkumbuka Muwenyekiti wa chama gani alosema mwaka juzi baada ya kupata Uwenyekiti kuwa "Adui yako ni shati la kijani".

Inawezekana nakosea, lakini tukistaafu utatafuta andiko hili.

Wazanzibari wanavaa kijani lakini kwenye sanduku wanapigia kura Zanzibar yao kwenye chama kileeee cha Mamlaka Kamili.

ZAMBARAU COLOUR ndio meseji sent kwa Wazenj kati yetu wenyetu
 
Back
Top Bottom