TRA Yaweka rekodi Mpya Kwa Kukusanya Trilioni 16.5 kwa miezi 6. Yavuka Malengo kwa asilimia 103%.

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
68,661
77,094
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeandikisha rekodi Mpya ya Mapato ya nusu mwaka Kwa kukusanya zaidi ya Trilioni 16.5 kwa.kioindi Cha miezi 6 au nusu mwaka ya mwaka wa Fedha 2024/2025.

Kiwango hicho ni Cha Juu zaidi kuwahi kufikiwa na TRA huku ikiwa ni ufanisi wa asilimia 103% yaani imevuka malengo.

Pia soma TRA yaweka rekodi ya kukusanya Trilioni 27.6 kwa mwaka 2023/2024

Aidha mwezi Disemba pekee imekusanya takribani Shilingi Trilioni 3.5 ikiwa ni Juu ya lengo la Trilioni 3.

1735830896350.png

My Take
Hongera sana Kwa TRA na walipakodi wote nimiwemo mimi.

Hongera sana Rais Samia, hongera Kwa Waziri Mwigulu Kwa kukusanya Kodi bila dhuluma na kuvuka malengo , haijawahi tokea tangu TRA kuanzishwa.

Tunatoka wito wa matumizi sahihi ya Kodi zetu na pia juhudi zaidi za kukusanya Mapato,Bado ukwepaji Kodi ni mkubwa na watu hawatoi Wala kudai risiti inavyostahili.
---

TRA YAKUSANYA TRILIONI 16.528 SAWA NA UFANISI WA 104.76% | MATOKEO UTEKELEZAJI AGIZO LA DKT SAMIA KWA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA

Kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amesema katika Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, Mamlaka hiyo imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 16.528, sawa na ufanisi wa asilimia 104.76 katika ukusanyaji wa Trilioni 15.778, ambapo ukuaji wake ukiwa ni asilimia 18.77, ikilinganishwa na kiasi cha Shilingi trilioni 13.917 iliyokusanywa katika mwaka wa Fedha uliopita wa 2023/ 2024.

Kamishna Mkuu Mwenda amebainisha hayo Jijini Dar es Salaam leo Januari 01, 2025, wakati akitoa Taarifa ya Makusanyo ya Kodi kwa Kipindi cha Mwezi Julai hadi Disemba kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Vile vile TRA imefanikiwa kuvuka lengo la Makusanyo ndani ya miezi sita mfululizo katika nusu ya kwanza kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba ya mwaka wa Fedha 2024/2025, huku Wastani wa Kiwango cha Makusanyo kwa mwezi ukiongezeka kwa asilimia 18, kutoka Wastani wa Shilingi Trilioni 2.319 mwaka wa Fedha 2023/ 2024 hadi wastani Trilioni 2.755 kwa Mwezi katika mwaka wa Fedha 2024/2025" amesema Kamishna Mwenda.

Aidha Kamishna Mwenda amesema mafanikio hayo ni kuendelea kutekeleza kwa Vitendo maagizo na Maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Katika moja ya maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Sisi kama TRA tumeendelea kuhamasisha Ulipaji Kodi kwa Hiyari, Kusikiliza na kutatua changamoto za walipakodi wote waliopo nchini, huku tukiimarisha Ushirikiano baina ya TRA na Wizara ikiwemo Taasisi na Ofisi zingine za Serikali katika Usimamizi wa Sera za kodi na Ufanyaji wa Biashara hapa Nchini" amesema Kamishna Yusuph Mwenda.

View: https://www.instagram.com/p/DF4w9MrItP1/?igsh=MTRjb3J3YzFvd3BxYg==
 
Ni nani anafanya verification ya hizi data za TRA?
Au TRA yeye anakusanya ,na eye anatusomea na kutuandikia alichokusanya🥺
Ninashauri next time ,waeleze makusanyo hayo wamekusanya wapi na wapi na kiasi gani
Mzee mwisho wa mwaka Huwa wanaonesha vyanzo vya Mapato baada ya reconciliation,hata Sasa ukita watakupa.

Swala la verification hizo hela zinaingia Hazina
 
Back
Top Bottom