Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

Kwa picha: Ufahamu kuhusu Ulimwengu

elimu ya science ya ulimwengu ni elimu ya kusadikika haina ukweli wowote wala haiingii akilini kama tutakuwa na uwezo wa kufikiri,binadamu hatuwezi kuishi kwenye dunia yenye shepu ya chungwa,na kama ingekuwa kweli tungekuwa tunaweza kuishi kwenye milima mikubwa kwa kuganda pembezoni mwa milima bila ya kuanguka.

dunia haiwezi kuwa duara na maji kuganda nje ya dongo la dunia na kisha iwe inaruka angani kwa speed na masafa tunayoambiwa hii haiwezekani kabisa,katika uhalisi wa maji hayawezi kupinda kufata umbo la nje la kitu chochote,maji popote yalipo ni lazima yawe level hio ndio sifa kuu ya maji,na ndio mana tunatumia lever za maji kujengea majumba ili kupata usawa wa nyumba

jua na mwezi ni vitu vipo sawa sawa na umbali wake kutoka ardhini ni sawa sawa kama tunavyoviona,pia kama utaangalia jua na mwezi utakuta vipo ndani ya wingu la blue havipo umbali wanaosema,pia mwezi hauna ardhi ya watu kwenda kutua,tukiwa hapa tunauona kuwa mwezi ni kitu kinapitisha mwangaza(transparent),utazame mwezi mchana utaliona wingu la buluu kwenye mwezi na usiku utaona wingu jeusi kupitia kwenye mwezi.

tumefundishwa gravity ndio inayotuzuia tusipeperushwe na speed ya dunia hiki ni kichekesho kikubwa,kwanini gravity haiwezi kuzuia mabofu na mifuko ya plastic na ni vyepesi sana, kwa ufupi hakuna gravity ni vitu vizito vinabaki ardhini na vyepesi vinakwenda angani

hatuwezi kufahamu kila kitu lakini upo uwezekano kuwa ukubwa wa dunia ndio hauna mwisho(infinity) wala sio duara na haizunguki wala kuruka,uhalisi ni kama tunavyoona kila siku dunia ipo tuli imetulia.
Proof, mkuu,, itapendendeza zaidi
 
Asante Paulo.. Naomba kuuliza, kuna siku niliona Prof Stephen Hawkings akieleza kuhusu black hole, sikumpata vizuri anachomaanisha. Pia Morgan Freeman akawa anafanya narration ya Big bang theory lakini mmmh, nikawa na maswali kuliko majibu. unaweza kudadavua kidogo kuhusu hivi vitu viwili? Mwisho nilifuatilia research zinazoendelea kwenye International space station, naomba kufahamu jinsi iko located na je haiwezekani ikagongwa na meteorites au asteroids?
 

Hii camera imefungwa kwenye moja ya SRB inaonyesha chombo hichi kilivyo na speed ya elfu 28 kwa saa..hichi chombo kina mwendo mkali sana.
 
The fifty likes on this post makes me sick, really sick! It hurts to know the extent of our societies dumbassery!
Eti hata jua liko umbali sawa na mwezi kutoka duniani?!!................argh, naomba nikutukane mkuu! (Naona kinyaa hata kukuita mkuu)
Huyo jamaa sijui amefanya research ipi akagundua kuwa jua na mwezi ziko sawa kwanza jua ni kubwa sana,pia dunia n ndogo sana kwa jua, ndio maana dunia na mwezi zimefungwa eneo moja. Kuna mahesabu ya kimwendo tu yanaweza kugundua kuwa jua lipo mbali.

Mf, kuna chombo kinasafiri kwa miezi 8.5 kufika sayar ya Mars, wataalam wanakwambia chombo hicho kitasafir kilometa kadhaa kwa saa na kitafika mars miezi 8.5 hapo unakuta wameshapiga umbali wa kutoka duniani-mars ni kilometa kadhaa kisha wanachukua mwendo wa kile chombo kwa saa, kisha wana calculate chap wanagundua mpk siku kitakapofika mars. Hivyo hiyo ktk sayari zingine itakuwa ni mahesabu hayohayo.

Hivyo unaposema jua na mwezi ziko sawa kwa umbali si kweli. Fuatilia jifunze zaidi na zaidi.
 
Back
Top Bottom