Maswali yako yote yanajibiwa na kitu kinaitwa gravitational force , nguvu inayovuta kila kitu kuelekea centre ya dunia , hili halina ubishi maana tunajionea wenyewe hii force ipo na ukiikwepa basi unaelea juu juu bila direction , ndege huruka kwa njia ya kuondoa force hii, unapokunywa soda kwa mrija ile soda inapanda kwenye mrija kwa kuodoa gravitational force upande mmoja ndo maana ukiweka mrija na ukaziba mdomo wa soda vizuri soda haipandi kwa hiyo hii force ipo. Hujaelewa niulize nikupe mifano mingine mirahisi utaelewa tu.
Kwa nini ndege zikiruka hazipotei ? Hizi ndge za kawaida haziwezi kuruka nje ya dunia (dunia ni anga , ardhi na bahari) hivi vyote ni physical materials yan anga lina hewa ambayo tunai feel na ina uzito kwa hiyo nayo ni sehem ya dunia, kumbuka dunia inazunguka na anga lake yan hewa ya mbeya huwezi ikuta iko ulaya itaendelea kuwa mbeya hapo hapo ni kama uko kwenye gari hewa ya ndani inatembea na gari labda ufungue madirisha. Ndege zinatembea kwa urefu toka ardhini na iki maintain urefu ule ule itajikuta inazunguka dunia hivyo kutua sehem husika (ndege zinafuata mdura wa dunia hazinyooshi nje ya dunia) na ndo maana ukiingalia kwa mda mrefu inakuwa kama inazama na kupotea kwa maana kwamba imeenda upande mwingine wa duara/dunia. pia ndege zinatumia mda na mawasiliano mda wote na rubani anafanya adjustment accordingly. Kifupi ndege hainyooshi bali inazunguka sema huwezi kuona maana dunia ni kubwa sana kiasi kwamba ukubwa wake hauingii hata akilini.
Issue nyingine ni kwamba tunaelewa vitu kwa kitu kinaitwa relativity yan kulinganisha, mfano huwezi sema hili jiwe ni kubwa bila kuona mengine madogo , huwezi kusema kule ni juu bila chini kuwepo , huwezi kusema uko ndani ya gari bila kuona au kutambua nje ya gari , huwezi kusema gari linatembea bila kuangalia nje , ukiangalia ndani mwende wa gari hutauona , mfano magari mawili yanayoenda direction moja yakitembea kwa mwendo sawa abiria wa magari hayo watajiona wamesimama nafikiri hii ishawahi kukutokea , sasa kwa upande wa dunia hatuna cha kulinganisha nayo ndo maana huwezi kuona ukubwa wake au umbile lake kwa macho .
Maji hayawezi kumwagika, sasa yatamwagika wapi ? Kumbuka nimekwambia kila kitu kinavutwa kwa huyo maji nayo nayavutwa hapa nimeweka vidoe ya watu waliosehem isiyo na gravity uone maji yanavyokuwa
Hamna upande wa dunia ulio juu wala chini , hizi ni assumption zetu tu lakini kisayansi hamna hicho kitu , vitabu vyote huwezi kukuta eti upande huu ni juu , hiyo tumetengenza sisi tu kwa kuangalia angani ila amini hamna juu wala chini