Never heard that mkuu..km vp tupe elimu kk..
Huyu jamaa walidai alikua kiumbe kutoka venus (alien) aliishi marekani kwa miaka mitatu yeye kaka yake pamoja na mwanamke mmoja mwaka 1957.
Ilijilukana baada ya mwanamke mmoja aliyekua anaitwa Nancy Warren mfanyakazi wa pentagon kumfuata mtunzi wa vitabu na muhubiri aitwaye Dr. Frank E. Stranges na kumpa nafasi ya kumhoji uyo valiant thor kiumbe kutoka Venus.
Maongezi yakawa hivi,
Valiant akasema meli yao ya angani iitwayo Victor one ilitua mnamo March 16th 1957 uko Alexandria, Virginia
Ikiwa na viumbe hao wanne akiwapo Valiant mwenyewe Jill, Donn pamoja na Tanyia walikaribishwa na polisi wawili ambao walipiga simu kwa Neil H. McElroy ambaye alikua secretary of defense kwa kipind icho. Ndipo akaanda mkutano wa dharula pentagon.
Ndipo wakapitishwa kwa njia za chini mpaka ikulu kuonana na Rais wa kipind icho Eisenhower na makamu wake .
Cha ajabu ni kua jamaa aliwaambia amekuja kufundisha Kuhusu Habari za mungu na mwanawe yesu akipinga vikali kua yesu sio mkombozi wa sayari Dunia tu Bali hata venus na kusoma biblia ipo katika sayari zote ambazo Zina maisha kama kitabu au hata kwa mawazo. Lakin Rais akumpa kibali icho na kuamua kufikia makubaliano ya kufanya kazi pentagon kwa hadhi ya VIP.
Na Kuna mashahid wengi walijitokeza baada ya chapisho na kusema walishamuona jamaa pentagon na wengine kusema walishafanya nae kazi Bila kujua. 1960 Val aliondoka duniani na kurudi kwao 1967 chapisho ndo likatoka. Hakuna aliyewahi kumhona tena mpk Leo.
Uhajabu wa uyu mtu ni huu...
1. Alikua na IQ 1200
2. Anaweza kuisoma akili ya kila mtu
3. Hana fingerprint katika vidole vyake
4. Damu yake Ina asilimia kubwa ya copper oxide kama Damu ya pweza
5. Alisema Kaishi miaka 490 ya venus
6. Alikua anaweza kuongea lugha Zaid ya 100 kwa ufasaha
7. Alikua na pafu moja kubwa
8. Moyo mkubwa sana
9. Alisema kuna wageni kutoka galaxy ya mbali ambao upendelea Kuja hapa duniani.
10. Alisema kwao na sayari nying viumbe uishi chini ya ardhi (underground ) ndo maana inakua ngumu kuwaona kwa kutumia satellite mfn. Venus na Mars.
Maombi ya Valiant kwa pentagon, Valiant alimwambia muhubiri Stranges kua
1. Aliwaomba pentagon atufundishe binadamu jinsi ya kuish Bila kuugua au kuumwa na kuyafutilia mbali magonjwa yote.
2. Kuishi Bila kikomo au maisha marefu ambayo hayajawah kutokea duniani.
3. Kupanda mazao au uoto Dunia nzima kusiwe na shida ya chakula.
Lakini pentagon walikataa kwa madai kua uchumi utaporomoka km kutakua hakuna magonjwa, njaa, na kifo.
Madai ya Valiant kutokana na alivyo mwambia mwambia Stranges ni kua serikali ya marekani miaka mingi imekua ikishirikiana na aliens na kuficha au kuteketeza ushahid, anadai kua watu kama wao ndo wamefanya technologia ya duniani kukua.
Kutokana na madai ya Oscar Schneider, Valiant mwenyewe hapo juu kwa mbele, Ukiangalia mkono wake vizuri utauona una uajabu fulani hivi. Nyuma yake ni Oscar Schneider aliyewahi kufanya kazi nae.
Val Jill, Donn katika picha hii
Val Jill, Donn katika picha hii
Val mwenyewe
Oscar Schneider aliyedai amewahi kufanya kazi na Valiant area 51 katika projects nying ikiwapo kujenga underground military base. Na huyu ndo aliyetoa picha Ile ya Kwanza kule juu.
Ref: Stranger at the pentagon 1967 1st edition
Flying Saucerama 1959
Madai au ushahid Oscar Schneider Kuhusu Valiant Thor.
Mwisho nakaribisha mchango, ongezeo na maswali yeyote kuhusiana na hili au alien yeyote maarufu anayesadikika Kuishi duniani.