Kwa nini wanawake wengi wachoyo?

Kwa nini wanawake wengi wachoyo?

Kwenye maisha lazima uanzie mahali fulani. Hapo wanawake wanashindwa kuvumilia kuona watu wakisaidiwa ili wapate nao nguvu ya kuondokea. Wanawazonga wee, kisa katafute na wewe kwako bila kufahamu kuwa hapo jamaa nao wanatafuta mtoko. Unaweza kuta nyumba inavyakula kibao lakini mnachopikiwa ni hatari. Wanaume wengi hawana tabia ya kula na familia ndo maana sio rahisi kujua mateso wanayopewa watu chini ya dari lako. Men wake up. Hakikisha haki inatendeka nyunbani kwako.
 
Ingawa sio wote lakini wengi ni wachoyo sana naona hata wewe unayesoma hii maada kama mwanamke itakuwa inakugusa inawezekana na wewe ni mchoyo.Unakuta nyumbani kuna kila kitu au mumeo amekuachia kila kitu lakini utafanya vijibajeti unavyovijua mwenyewe ili watu wasilizike, muhusika akikuuliza unakuja na majibu yasiyo na kichwa wala miguu yawezekana anayetafuta mwingine sio wewe hii ni kwa nini?


Nafikiri ile hofu ya kusalitiwa na nyumba ndogo inasumbua kina mama wengi. Kwani mwanamme akishakuwa na nyumba ndogo mara nyingi mapenzi nyumbani kunakuwa hakuna na mamaaa naye anataka atimiziwe wajibu wake hivyo kwa hela anazo achiwa ana sevu kidogo ili siku ya siku akija kususwa kimapenzi ajipatie mtu wa kumtunza na kumsitiri kimapenzi. Ni mtizamo wangu tu.
 
ni HE kule kwetu ambako ukituudhi tu tunajinyonga ukiona mwa-gito ujue wa kiume angekuwa wa kike angeitwa se-gito

hee! Shosti kuumbe! Sasa malalamiko ya nini c atafute vyake mweh! Angalia nduguyo asijikomit aisee mana anahasira za mkizi!!! Muwahi!!
 
Hii statement nimeisikia kama ×10 hivi, ndugu wa mume haridhiki, kwa nini awe wa mume tu, wa kwako yeye anaridhika?

wanawivu ndio mana hawaridhiki eti kwakuwa ndugu yao ndo kichwa cha familia thubutuuu!!!
 
sisi wanaume bajeti za ndani huwa hatuzijui na ndiyo maana tunaona wenzetu hivyo , mama akiishiwa limao nayo akuombe hela , huwa wanaweka hela ya dharula yakimkuta awe na uwezo wa kuyatatua haraka na hapo ndiyo sheshe linapoanzia la ubahili, sisi bajeti zetu ni bia nyama choma na washkaji na offer za bar zisizo na kichwa wala mguu

bora yako umelijua hilo wengne ndo hvyo tena et wachoyo embu avae kanga na yeye ckumoja tu ashikilie usukani afu ndo wageni wametinga ukiangalia akaunt haisomi mnajenga huko nanjilinji mkwe anaumwa afu ndo mwezi wa kumi nambili !shauli yake alalame tu!
 
Atakua mkeo tu ndo ana mkono wa birika asa we unamuachia elf2 ya matumiz na unajua mkeo ni kaseja apo anahitaj kufanya marejesho akabunue dera etc unategemea atatoa wap??
Jiangalie ukija na uzi wako apa jf uwe umefanya research sio unajurupuka na kusema wanawake sema mke wangu.
 
halafu ndugu wa mume hawaridhikagi, sijui wapoje?

wewe mwenyewe ni ndugu wa mume upande flani..I hate watu wenye mawazo yako..lini waafrika tutabadilika tuache vimaneno maneno??mara mama mkwe,mara ndugu wa mume..don't you know kuwa kaka au mdogo wako akioa utakua ndugu wa mume??au mama yako atakua mama mkwe??TUBADILIKE!!
 
hivi ni kweli wamama wachoyo, au uchoyo wanatufanyia sisi ndugu wa mume ....!?
 
Hii statement nimeisikia kama ×10 hivi, ndugu wa mume haridhiki, kwa nini awe wa mume tu, wa kwako yeye anaridhika?

mara nyingi ndugu wa mwanamke hawana shida coz wanajua wapo ugenini so hawawezi kuleta controlling ya masuala ya nyumba ya ndugu yao. tatizo ndugu wa mwanaume wakija kwa ndugu yao hujiona kama wao ndio wenye nyumba. watataka wahoji kila kitu, kitu ambacho sio sahihi,
 
Kajitegemee utagombana na shemeji yako buree.......bajet unataka upange wewe kama mama mwenye nyumba.

Unataka nyama kila siku eeeh....eti haturidhiki,kama umetoa hela vile!!!!!

Umesema yote. Mijitu ya namna hii hasara sana. Wakafanye kazi P*mbav zao !!!
 
wewe mwenyewe ni ndugu wa mume upande flani..I hate watu wenye mawazo yako..lini waafrika tutabadilika tuache vimaneno maneno??mara mama mkwe,mara ndugu wa mume..don't you know kuwa kaka au mdogo wako akioa utakua ndugu wa mume??au mama yako atakua mama mkwe??TUBADILIKE!!
haa haaa acha hasira mkuu, mimi kuwa ndugu wa mume hakuwezi kubadili ukweli kuwa kuwa tuna matatizo sana ya kupenda kuingilia masuala ya ndan ya ndugu zetu. mimi nimegundua tatizo lilipo na na naepukana nalo, wewe je chukua hatua mkuu.
NARUDIA TENA NDUGU WA MUME TUBADILIKE MASUALA YA NDANI YA NDUGU ZETU NI YAO NA WAKE ZAO SISI TUFANYE YETU. PERIOD
 
Si uchoyo ni budget maisha magumu haya ujue,hatwez kua tunakula sato kila cku,maharage tembele vyahusika...hauwez kakae kwako c kukaa kwa watu!maana kuna watu wanakula jaman utafikiri hana uhakika km atakula kesho na keshokutwa

Mh! Kuwasema watu wanakula sana ndouchoyo wenyewe wape msosi wenzio washibe waridhike
 
Kajitegemee utagombana na shemeji yako buree.......bajet unataka upange wewe kama mama mwenye nyumba.

Unataka nyama kila siku eeeh....eti haturidhiki,kama umetoa hela vile!!!!!

Bi dada mpe lakini taratibu taratibu keshatibuliwa na shemejiye kisa maandazi ya chai asijemsemea bure kwa mama mkwe ndoa ya kakake iwe ndoano
 
Back
Top Bottom