Kwa nini wanawake hutoka nje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wanawake hutoka nje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Aug 21, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Wanawake wengi walioolewa hutoka nje ya ndoa kwa sababu mbalimbali lakini nyingi zikiwa ni kutafuta ridhiko la kihisia.

  Dr. Ralph Meyering na Profesa Emeritus wa chuo kikuu cha Illinois huko Marekani wanasema inaonekana wanawake hutazama tendo la ndoa nje ya ndoa zao kama jambo tofauti na lile wanalofanya na waume zao.
  Kwao kUtoka nje sio kufuata tendo la ndoa hasa. Ni vyema hata hivyo kabla sijazitaja baadhi ya sababu nikasema kwamba hatupaswi kuzichukulia sababu hizo kama msahafu , hapana. Binadamu hubadilika kila siku na suala la hisia na uamuzi wa binadamu nalo limejaa utata pia.

  tu mmoja anaweza kutoka nje ya ndoa kwa sababu ambayo mwingine wala asingehisi kuwepo kwake lakini pia zile sababu ambazo zimebainishwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni chanzo cha wanandoa kutoka nje zInaweza zisiwe ndizo hizo ambazo zimemfanya mwanandoa fulani kutoka nje.

  Sababu zenyewe ni hizi hapa:

  1. Kutafuta kusikilizwa- kuna idadi kubwa a wanawake ambao hutoka nje ya ndoa zao kutafuta kuziba pengo la kihisia. Kwa kawaida mwanamke hupenda kuona mwanaume akimjali, akimsikiliza na kuwa karibu naye kihisia, na kama jambo hili halitimizwi na mumewe, basi atatafuta mtu wa kuziba pengo hilo huko nje. Kuna wakati unaweza kumsikia mwanaume akilalamika, "nimeamua kuachana na mwanamke yule. Nilikuwa nampa kila kitu lakini bado akawa anatoka nje ya ndoa." Ndio inawezekana alikuwa anampa mkewe kila kitu, lakini alisahau kuwa mwanamke ni zaidi ya mali.

  2. Kutafuta kukamilishwa- kuna wanawake hudhani kwamba umri wao umekuwa mkubwa na hawana thamani tena, yaani hawawezi kupendwa. Hofu ya kwamba wamezeeka au hawapendeki inaweza kuwafanya kuwa wepesi na kukubali kutoka nje ya ndoa ili kujithibitishia kwamba hawajachuja au kupoteza thamani zao. Sababu hii pia huwaangukia pia wale wanawake ambao hawajaolewa lakini wanatembea na vijana wadogo waliowazidi umri.

  3. Kulipa kisasi- Ingawa sio wanawake wengi wanaolipa visasi kufuatia waume au wapenzi wao kuwa na uhusiano nje, bado kuna idadi a kutosha ya wanawake wanaofanya hivyo. Mara nyingi hutokea kwa wale ambao walikuwa na hisia ya kutoka nje lakini walikuwa anazikandamiza hisia hizo, hivyo inapotokea kupata sababu, ni rahisi sana kwao kutoka nje.


  4. Kuwa huru katika mapenzi- kuna wakati tendo la ndoa kwa wandoa au wapenzi linakuwa ni tendo la mwanaume zaidi. Yeye ndiye anayeamua lifanyike vipi na wakati gani.
  Mwanamke anakuwa hana kauli kabisa kwenye jambo hili. Mwanamke anayeishi kwenye ndoa au uhusiano wa aina hii hufikia mahali tendo la ndoa na mumewe au mpenzi wake linakuwa ni aina ya utumwa. Ni rahisi sana kwa manamke anayeishi kwenye husiano wa aina hii kutoka nje ya ndoa ili kutafuta ule uhuru ambao haupati kwa mumewe.


  5. Matatizo ya kipato- hili linafahamika kwa wengi kati yetu. Mwanamke anatoka nje ya ndoa yake ili amudu kujikimu kutokana na ugumu wa hali ya kimapato. Kuna wanawake ambao wametelekezwa au waume waume zao hawana kipato. Baada ya kuhangaika sana hulazimika kuutoa mwili wake kwa walichonacho ili mkupata fedha au kazi. Maofisini kuna waawake wengi ambao wanaishi kwenye kazi zao kwa kutoa miili yao kwa mabosi au wamiliki wa ofisi hizo kwa sababu wanataka kuendelea kuwa kazini.

  6. Kutoridhishwa katika tendo- Kabla ya miaka ya Sabini tafiti zinaoneshwa kwamba tendo la ndoa halikuwa linahesabika kwa ridhiko la mwili bali zaidi lilikuwa ni ishara ya kupendana na kutafuta watoto. Lakini leo hii tendo la ndoa limekuwa ni burudani, lenyewe kama lilivyo. Kwa hiyo mpenzi anapokuwa na udhaifu hata kidogo, sio ajabu mwenzake kuhisi kwamba anakosa jambo kubwa na muhimu kuliko hata uhusiano wenyewe. Katika hali kama hiyo anaweza kuanza kutafuta mtu ambaye anaamini atamfanya ahisi ridhiko. TV na mikanda michafu ya video imeongeza uongo kuhusu ridhiko la tendo la ndoa, kiasi kwamba yule ambaye mpenzi wake ana udhaifu huamini kwamba anakosa kikubwa kama kinavyoonekana kwenye TV na mikanda michafu ya video.

  7. Tamaa ya kipato- Inashauriwa kwamba mwanaume anapokwenda kuoa inabidi aende kama yeye, yaani akionesha na kusema kuhusu alivyo, bila kuongeza chumvi. Wanashauri pia kwamba mwanaume anapokwenda kuoa akague namna msichana alivyolelewa yaani aina ya malezi ya wazazi wa mwanamke. Kuna wanawake ambao hawako tayari kukosa kile wanachokitaka maishani. Wanapokikosa wanakuwa tayari kufanya lolote, ikiwa ni pamoa na kuuza miili yao.

  Kwenye utafiti wake alioufanya, Dk. Lynn Atwater anaonesha kwamba nusu ya wanawake wanaotoka nje ya ndoa zao wanakuwa wamewajua hawara zao miezi kadhaa kabla hawajafanya nao tendo la ndoa.
  Nusu waliobaki wanakuwa wamewafahamu angalau kwa katika kipindi cha mwaka mmoja kabla hajaama kufanya nao mapenzi. Kabla mwanamke hajakubali kufanya nmapenzi na hawara huwa ameshafanya uamuzi huo sio chini ya mwezi mmoja kabla.

  Kwa hiyo unapokuta umehangaika kumpata mke wa mtu kwa muda mrefu, unapokuja kumpata, basi jua kwamba Alisha kukubalia mwezi mmoja au zaidi kabla ya siku hiyo.

  Mara nyingi mwanamke akikubali, kabla hajamjulisha rasmi hawara yake kwamba yuko tayari, ni lazima pia apate ushauri au azungumze na rafiki yake wa karibu sana. Unapofanya mapenzi na mke wa mtu ambaye umemhangaikia kwa muda mrefu, usidhani hiyo ni siri yenu, kuna mwingine amejulishwa.

  Ni wanawake wachache sana wanaobaki na siri hiyo wenyewe.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Haya mambo haya....mhhhhhhhh!!

  Hata sijui yataishia wapi!!
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kwa hisia zangu tu ninakubaliana na mada kwa kiasi kikubwa sana. Lakini ninachojiluiza kila linapokuja suala la mwanamke tu au mwanmme tu, kwa nini hatuyazungumzii masual haya katika umoja wake?

  Kwa nini Mwanamke anatoka nje ya ndoa? Kwa nini wanaume wanahiari wasichana wa chini ya umri wao? Kwa nini wanaume hawaridhiki na wapenzi wao?...na masuala mwngi kama haya, jawabu zake hazikamiliki mpaka kuwepo na wa jinsia ya pili.

  Kwa hivyo kwenye mada hii, isipokuwa kwa sababu ya 5 na 7 ambazo zote zinazungumzia kipato, lakini sababu nyengine zote nahisi ndio hizo hizo zinazowafanya wanaume watoke nje ya ndoa zao, yaani kusikilizwa, kukamilishwa, kulipa kisasi, kutafuta uhuru au jambo jipya katika tendo la ndoa na kutoridhishwa kwenye tendo la ndoa...

  Hata hiyo sababu ya kipato, kuna baadhi ya wanaume (ingawaje wameoa) huenda kwa mashuga mami ambako hulipwa kwa kungonoka kwao. Kwa ufupi, "ukofi haupigwi kwa mkono mmoja", nikimaanisha kuwa kila alipomwanamke, kuna mwanamume nyuma na kinyume chake.
   
 4. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono hoja, kwa maelezo uliyotoa upo sahihi. mia
   
 5. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ahsante kwa thread nzuri!
   
 6. Kibirizi

  Kibirizi JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 602
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wanawake wengi huiingia kwenye ndoa ili kufuata ndoa na sio mapenzi hivyo basi kuna wakati huolewa na mwanamme ambaye hampendi ila kwa sababu amemtangazia ndoa huamua kuolewa naye, pindi anapokuwa kwenye ndoa huanza kutafuta anaowapenda au kuwakumbuka alikuwa anawapenda. Kwa mtizamo wangu hiyo ndio sababu ya wanawake kutoka nje ya ndoa.
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhh
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  sababu zote zinaweza kuhusika, except for #2. kama mwanamke anasikilizwa na kuheshimiwa hawezi kamwe kujiskia kuwa amezeeka. mwanamke hazeeki,anazeeshwa! na hata issue ya kutoridhika na tendo la ndoa nalo limekaa kihisia zaidi. if u make her feel u like her man, yaani nadhani ni mteremko tu!sasa kama ni serial cheater,u dont spend time together, anakuwa anajiskia kama hgeli,hakuna heshima wala nini! unategemea nini?
  turejee maandiko ya dini: wanaume wapendeni wake zenu, na wanawake watiini waume zenu! mwanamke akioneshwa kupendwa, yaani ni automatically atakutii na kukutumikia kwa uaminifu! lakini lazma mapenzi yaanze kwanza,ndo utii ufuate. mimi naamini wanawake ni waaminifu sana,lakini frustration ndo zinapelekea going astray! kuna watu ni serial cheaters,lakini mkewe humuambii kitu!of coz kuna black sheep kwenye kila jamii,na hapa ndipo sababu hizo hapo juu zinakuwa na maana
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  Wanawake ni waaminifu sana? Haya bana...wewe wasema hivyo!!
   
 10. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Hiyo sababu ya "kulipiza kisasi" imetulia. Wanaume wakware wakisoma hapo lazima pressure ipande.
   
 11. tatizomuda

  tatizomuda Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kweli mapenzi yanarun dunia.................
   
 12. M

  Mkumbo2011 New Member

  #12
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Duh jaman mambo haya ni magumu sana pia unpredictable
  Mungu tusaidie kwa kweli hali si shwari hasa kizazi hiki chetu a.k.a the papcorn generation
   
 13. caven dish

  caven dish Senior Member

  #13
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kama mambo yenyewe ndio hivi ...bado nipo nipo mwaya!
   
 14. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #14
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hapa naona niishie tu kutoa "LIKE"
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wacha watoke, huwa insaidia ku-balance mambo ndani, wasipotoka utaona watoto wanavyopata makonzi
   
 16. b

  babaubayaz New Member

  #16
  Sep 16, 2011
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanaume wengine wakuwa wapo kikazi zaidi kuliko mapenzi
   
 17. K

  Kikambala Senior Member

  #17
  Sep 16, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni kwelllllllllllllllllllllll
   
 18. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  umenena vyema
   
 19. C

  Capitani Member

  #19
  Sep 16, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushauri huo mimi naupa100% saafi sana ,muelewa na achote hazina nzuri hii ya ushauri endeleeeeaaaa tena na tena Bravooooo
   
 20. Noor

  Noor Senior Member

  #20
  Jan 12, 2013
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 145
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Let's discuss and mention reasons why women cheat. Je kwa sababu ya maudhi ya ndani ikiwemo kutoridhishwa au wewe unaonaje mdau?
   
Loading...