kwa nini wanaume.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini wanaume....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nailyne, Sep 22, 2011.

 1. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi kwa nini wanaume wengi ni wagumu kukiri udhaifu, makosa au kukabali kuwa kuna vitu hawavijui mbele ya mwanawake?, nimeona kwenye mahusiano huko ndio balaa,inahitaji hekima kumwambia mwanaume amekosea, au hicho anachokifahamu hakipo kama anavyodhania,na kama amekosea ndio kabisa hadi aje akubali kosa itachukua karne...,is it about man's ego ama? ( sio wote lakini)
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Pole sana Nailyne, unaonekana katika maisha yako una bahati mbaya ya kuwa na mahusiano na madikiteta tu. Ndiyo maana ukafikia mahali ukadhani wanaume wote wako hivyo!!
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sometimes ni mans ego
  Ila inategemea umeniambiaje bana
  Ukija na mkwara wako sitakiri kosa wala kukubali nimekosea ila ukija taratibu tutaelewana
  Na kukiri sio kule kusema eehh nimekosa ila ni ile kiaina "haya yaishe "
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Sep 22, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nailyne umenikumbusha mbali sana mydia.
  Kwetu sie wa 47 tulifundishwa kuwa Mwanaume hakosei!! Mwanaume ANAKUMBUSHWA hata kile ambacho hakijui unamfundisha kwa KUMKUMBUSHA .....yaani ile ya hajui mwanae anadaiwa ada (kwa kuwa hajawahi kumlipia) we unamkumbusha tena kwa sauti ya upole na kumpetipeti mgongoni....Hun, umesahau kuwa ULITOA NUSU na sasa bado anadaiwa ile nusu ilobaki 50,000? ........lol kwa vizazi vya sasa hivi hata si rahisi kuishi kwa namna hii. Lakini sie wengine imetusaidia sana kuepusha migogoro ya hapa na pale.

  Lakini ukianza kumsema, hujui moja mbili, tatu, umekosea a, be, che na kelele nyiiiingi haisaidii. KWanza anaona unamgeuza mtoto na kumsema kama mtoto.

  Eh I wish ningekuwa sawa jioni hii, mada hii mh!
   
 5. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nimeweka angalizo sio wote,..niliyenaye anajitahidi sana n nampongeza kwa hilo.
   
 6. RR

  RR JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  yaani huyo wa kwako anaweza kukiri makosa na kuomba radhi?
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Barikiwa sana mpendwa. Napenda sana coments zako, zina mafundisho sana kwa aliye tayari kujifunza.. Una hazina kubwa ya "hekima" na "busara"... Mungu akulinde wakati wote!
   
 8. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  MMJ1 umesema
  Bahati mbaya natumia kamchina hakana sehem ya like wala thanks.
  Wanakosea anapokujia na mishutuma kuwa unajua hapa na hapa ulikosea au hiki na hiki ni makosa
  Ofcourse hata kama ni mimi niapply uanaume wangu sitakubali kukiri kosa
   
 9. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Inaonekana wewe mgumu eeh?
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  nadhani timing ni kitu muhimu. manipulation haizai matunda. usipomuibia mmeo, majirani watakusaidia. im sorry to say this, bt men shld be handled like kids ili maisha yawe rahisi. u let him feel like ndo kila kitu, ndo anajua, anaamua na kuongoza. na akishaleta hereni ama uturi ndo keshaomba radhi, just accept kama sio issue kubwa.
   
 11. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  of coz kwa uzoefu kangu kadogo, hakuna mwanaume atakiri kosa kama utamwambia as if unamwambia mtoto wako, au mdogo wako but hata ukitumia hiyo hekima mara nyingi huwa inakuwa ni ile ya kubali ya ishe ndio maana nikauliza why?
   
 12. mdeki

  mdeki JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 3,303
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  kwahiyo unatka tuanze kukiri kosa tu kizembezembe?
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hili tatizo limechangiwa na mambo mengi saana.... ikiwa tamaduni zetu ambazo pia zimesukwa na mfumo dume... Mtoto wa kiume/wanaume walijengewa saana confidence tokana na wanavokua treated kwa upendeleo katika familia.... hio system humvua confidence mwanamke na kumvisha confidence mwanaume.... Hivo basi pale ambao mwanaume akikosea anashindwa kabisa kutaka kubali na kuonesha kwa mwanamke wake kua yeye kweli kakosea... lazima ata manipulate na kukuambia "oh Mpenzi utaona kama nimekosea lakin wee ulipo fanya hivi ndo umesababisha yoote haya" lol (kwa mjuvi unaelewa hapo ndo kisha omba msamaha na kamaliza....)

  Kuna pia tatizo upande wa wadada/mama... sababu mwanaume ni adimu saana kuomba msamaha - anapopata mwanaume ambae kwake ni rahisi kuomba samahani... kwa kukosa busara ndo sasa inakua shida... ataongea maneno hapo weeee mpaka kuchwe!! Atataka mashoga woooote wajue kua jamaa kaomba msamaha.... kwa maneno kuongezea kama "alijifanya mjanja... mie mwisho wa reli bana".... Sasa vitu kama hivo - hubomoa kabisa na kusababisha next time huyo mwanaume asikuombe msamaha hata kama anastahili... hivo na kwa wanawake wengine woote atakao kua nao....
   
 14. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe kabisa, natamani wa dada wa leo wangeelewa usemacho MJI, lakini kumwambia kwa kumbembeleza na kumpetipeti inaondoa kosa alilofanya? au ni katika hali ya kufunika kombe mwanaharamu apite?
   
 15. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo MR. Rocky ukiambiwa makosa yako kwa kubembelezwa, bila shutma na makelele utakiri kosa lako?
   
 16. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  so sote tunakubali hawa viumbe ni wagumu kukubali ukweli esp kama ni makosa, na ili kuweka mambo sawa nilazima kuwapambapamba wakati unadress hiyo mada.
   
 17. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye blue hapo sina cha kuongeza, na ndicho ninachojiuliza kwa nini afikie kusema '...wewe ndio umesababisha yote hayo' instead of admiting alichokifanya sio sahihi? au kukosea anakosea mwanamke tuu akikosea mwanaume ni dhaifu?
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa, sie wa 47 kuna kakitu kama ka mama zetu bado tunako, kunyeyekea, na ukifanikiwa hii utakaa ujue ubishi wa mwanaume wako
   
 19. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Nakuingiza kwenye kundi la MJ1..kwa hii useful coment..mwambie paw aweke kitufe cha like kwenye cm bana..au arudishe thanks jamani!
   
 20. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #20
  Sep 22, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  No Nailyne.. akikosea mwanaume sio kwamba ni dhaifu (in fact ni wakosaji wakubwa saaana) ila tu hivo ndio walikua programmed... With time mambo yanabadilika taratibu for kuna changes nyingi saana katika jamii dhidi ya mahusiano kati ya wanaume na wanawake... Hivo basi saizi idadi ya kuomba msamaha walau ni kubwa ukilinganisha na enzi za baba/babu zetu.... Mwingine kuweza anasema kwa kidhungu... "I am Sorry" na kukwepa sema "Nimekosa" kwa ile tu anaona kama kwa kiswahili ina uzito zaidi (observe this)
   
Loading...