kwa nini wanaume....

Barikiwa sana mpendwa. Napenda sana coments zako, zina mafundisho sana kwa aliye tayari kujifunza.. Una hazina kubwa ya "hekima" na "busara"... Mungu akulinde wakati wote!
Sweetlady, amina. Nashukuru kwa hili. Hapa jamvini tunajifinza kila siku. Mimi personally nimejifunza mengi sana kupitia hapa na katu sijutii muda wangu tangu nimejiunga JF 2009. Sometimes nafikiria ningeigundua mapema pengine ingenisaidia kuepusha mengi yaliyonitokea katika nyanja hii ya Mahusiano na mapenzi, hata hivyo ninaamini yote yaliyotokea yamenitokea kwa sababu maalumu na ni katika kunijenga zaidi. Siyachukulii mapenzi na mahusiano for granted au kijuu juu kama nilivyokuwa ninafanya bali ni sehemu, tena sehemu muhimu ya maisha yangu mimi kama MJ1. Ni wajibu na ningependa kushare na wenzangu juu ya lolote katika kufanikisha sehemu hii muhimu katika maisha yetu inakuwa nzuri na ya kufurahiwa.

Barikiwa sana mpendwa.
 
kwa hiyo MR. Rocky ukiambiwa makosa yako kwa kubembelezwa, bila shutma na makelele utakiri kosa lako?
Nadhani hata mwanamke hapendi kugombeshwa kama mtoto mdogo..... ingawa hawa wenzetu mara nyingi hujiona wanayo haki hiyo. Ajabu haya yote hutokea mkiwa tayari mshaoana. Hebu fikiria ukikosea wakati wa boy/girl friend au uchumba? reaction huwa tofauti sana na wakati mkiwa mshaoana. Huwa ninaangalia wale ambao wakatiu wa urafiki, galfriend ana uwezo wa hata kumwagia maji usoni wakiwa wanazozana na bado ataomba msamaha but ngoja aoe. Mi hata sielewi ni nini labda kwa kuwa sijawahikuexercise hacra (hata sijui kama huwa ninazo ) zangu.

so sote tunakubali hawa viumbe ni wagumu kukubali ukweli esp kama ni makosa, na ili kuweka mambo sawa nilazima kuwapambapamba wakati unadress hiyo mada.

Hata wewe Nailyne bana mtu akikueleza makosa yako wa kubembelezwa ni rahisi kumsikiliza na kumwelewa zaidi ya akikugombeza. Sometimes akikugombeza utakiri na kukubali ili tu ayaache makelele yake. But in general kwa kuwa wanaume ni viumbe ambao toka utotot na katika jamii zilizo nyingi wanalelewa katika hali ya ku'ogopwa' yeye ndo mkuu wa familia e,t.c sasa ukimkaripia ni kama unamwonyesha kuwa haja=fuzu vizuri yale mafunzo yoooote ya kuwa yye ni kichwa cha familia ambacho hakikosei, husahau na kupitiwa tu kutokana na kazi au mambo mengi ya kuitunza familia yake.

Ni sawa na wewe umemkosea mtoto wako kisha mtoto aanze kukugombeza kuwa umekosea. (sisemi kuwa wanawake ni watoto bali kwa akili ya mwanauem na jamii tutokazo wanaume hulelewa katika mtazamo huo.

hapo kwenye blue hapo sina cha kuongeza, na ndicho ninachojiuliza kwa nini afikie kusema '...wewe ndio umesababisha yote hayo' instead of admiting alichokifanya sio sahihi? au kukosea anakosea mwanamke tuu akikosea mwanaume ni dhaifu?

Nailyne.......... concern yako iko sawa kabisa but napenda kusisitiza kama ulivyosema si wote wenye mtazamo huyo. Lakini pia inategemea na unavyomchukulia na jinsi ulivyommould toka mwanzo wa mahusiano yenu (hasa nyie vijana wa kisasa). Sie wa zamani ambao tulibahatika kuwapata waliolelewa kizamani hatuna vudi kuendana nao kama tulivyoanswa na wazee wetu wa zamani. Sio eti kwa kuwa siku hizi kun usawa na kwa kuwa mwanangu anamtreat mwenzi wake namna hii basi na mie Mj1 nakurupika kutaka kuleta revolution nyumbani kwangu, mtu na mvi zake za chuma naanza tu kugomba ume, ume,ume tena ukome sijui nini (kisa Bi kidawa nyumba ya pili anamgombesha mumewe) ntakuwa nakosea. KWanza kikongwe wangu atanshangaa nimevuta cha wapi, Malawi, Msumbiji au Arusha! kabla sijapakilishwa rambo zangu nirudishwe kufunzwa adabu huko kijijini.!!

So mydia, fanya timing, angalia muda muafaka usianze tu, bwana ndo karudi kazini mwali wewe anakukuta mlangoni mikono kiunoni unaanza eh, eh, ehhhhhhhhh katu hatokiri.

(Besides kuna muda mzuri na muafaka wa mwanamke kufikisha malalamiko, grudges zako na zikazikilizwa bila hata swali la nyongeza mpenzi- kula timing tu).
 
Sweetlady, amina. Nashukuru kwa hili. Hapa jamvini tunajifinza kila siku. Mimi personally nimejifunza mengi sana kupitia hapa na katu sijutii muda wangu tangu nimejiunga JF 2009. Sometimes nafikiria ningeigundua mapema pengine ingenisaidia kuepusha mengi yaliyonitokea katika nyanja hii ya Mahusiano na mapenzi, hata hivyo ninaamini yote yaliyotokea yamenitokea kwa sababu maalumu na ni katika kunijenga zaidi. Siyachukulii mapenzi na mahusiano for granted au kijuu juu kama nilivyokuwa ninafanya bali ni sehemu, tena sehemu muhimu ya maisha yangu mimi kama MJ1. Ni wajibu na ningependa kushare na wenzangu juu ya lolote katika kufanikisha sehemu hii muhimu katika maisha yetu inakuwa nzuri na ya kufurahiwa.

Barikiwa sana mpendwa.
Amina!.... Nimeishiwa maneno ya kukuambia! Nakuombea maisha marefu mpendwa...pamoja na familia yako!... Sante sana!
 
Nadhani hata mwanamke hapendi kugombeshwa kama mtoto mdogo..... ingawa hawa wenzetu mara nyingi hujiona wanayo haki hiyo. Ajabu haya yote hutokea mkiwa tayari mshaoana. Hebu fikiria ukikosea wakati wa boy/girl friend au uchumba? reaction huwa tofauti sana na wakati mkiwa mshaoana. Huwa ninaangalia wale ambao wakatiu wa urafiki, galfriend ana uwezo wa hata kumwagia maji usoni wakiwa wanazozana na bado ataomba msamaha but ngoja aoe. Mi hata sielewi ni nini labda kwa kuwa sijawahikuexercise hacra (hata sijui kama huwa ninazo ) zangu.

MJ1 asante sanaaaa, kuna vitu naona umeobserve..
kwanza wanaume wanajiona wanayohaki ya kuwagombeza wanawake zao pindi wanapowakosea na si haki kwa mwanamke kufanya hivyo kwa mumewe, na pia hili ni tatizo zaidi kwa wanandoa so je wanaume wakishaoa huwa wanaamini wameshawamili wanawake zao na wanauwezo kuwatreat kama watoto wao?

Hata wewe Nailyne bana mtu akikueleza makosa yako wa kubembelezwa ni rahisi kumsikiliza na kumwelewa zaidi ya akikugombeza. Sometimes akikugombeza utakiri na kukubali ili tu ayaache makelele yake. But in general kwa kuwa wanaume ni viumbe ambao toka utotot na katika jamii zilizo nyingi wanalelewa katika hali ya ku'ogopwa' yeye ndo mkuu wa familia e,t.c sasa ukimkaripia ni kama unamwonyesha kuwa haja=fuzu vizuri yale mafunzo yoooote ya kuwa yye ni kichwa cha familia ambacho hakikosei, husahau na kupitiwa tu kutokana na kazi au mambo mengi ya kuitunza familia yake.

Ni sawa na wewe umemkosea mtoto wako kisha mtoto aanze kukugombeza kuwa umekosea. (sisemi kuwa wanawake ni watoto bali kwa akili ya mwanauem na jamii tutokazo wanaume hulelewa katika mtazamo huo.

hapo kwenye red....kwa hiyo MJ1 hili nii tatizo ambalo lina shina kwenye mfumo mzima wa maisha ya jamii zetu na malezi ya watoto wa kiume, kuwa watoto wakiume ni wakuogopwa saa zote na kuwa huwa hawakosei na hata wakikosea basi jamii esp wanawake haipaswi kuonyesha kuwa mwanaume amekosea, je huoni ipo haja ya wazazi wa leo kuangalia suala hili katika makuzi ya watoto wao? kuliko kuwatengenezea mazingira ambayo wanaamini wao siku zote huwa hawakosei hata kama in reality wanakosea?

Nailyne.......... concern yako iko sawa kabisa but napenda kusisitiza kama ulivyosema si wote wenye mtazamo huyo. Lakini pia inategemea na unavyomchukulia na jinsi ulivyommould toka mwanzo wa mahusiano yenu (hasa nyie vijana wa kisasa). Sie wa zamani ambao tulibahatika kuwapata waliolelewa kizamani hatuna vudi kuendana nao kama tulivyoanswa na wazee wetu wa zamani. Sio eti kwa kuwa siku hizi kun usawa na kwa kuwa mwanangu anamtreat mwenzi wake namna hii basi na mie Mj1 nakurupika kutaka kuleta revolution nyumbani kwangu, mtu na mvi zake za chuma naanza tu kugomba ume, ume,ume tena ukome sijui nini (kisa Bi kidawa nyumba ya pili anamgombesha mumewe) ntakuwa nakosea. KWanza kikongwe wangu atanshangaa nimevuta cha wapi, Malawi, Msumbiji au Arusha! kabla sijapakilishwa rambo zangu nirudishwe kufunzwa adabu huko kijijini.!!

So mydia, fanya timing, angalia muda muafaka usianze tu, bwana ndo karudi kazini mwali wewe anakukuta mlangoni mikono kiunoni unaanza eh, eh, ehhhhhhhhh katu hatokiri.

(Besides kuna muda mzuri na muafaka wa mwanamke kufikisha malalamiko, grudges zako na zikazikilizwa bila hata swali la nyongeza mpenzi- kula timing tu).[/QUOTE]

hapo kwenye red hapo ndio penyewe haswaaa patakapoonyesha hekima ya mwanamke..,MJ1 ubarikiwe sanaaa naamini wengi wananufaika na mabusara yako,
 
wanawake tuna kazi oh my???........

Chauro umeonaee, si kazi ndogo eti, unaaambiwa wanaume kama watoto shurti kubebelezwa lakini watoto ambao hawakosei ndio uhalisia wa maisha ya jamii yetu leo.
 
wanawake tuna kazi oh my???........

Unafikiri Chauro? wala hakuna kazi yoyote. Ndio maana wanawake tuna sifa ya upekee ya uvumilivu...hivi umeshawahijiuliza visa ambavyo umeshawahi mtendea mama yako akavisamehe?? je umeshajiuliza visa (ambavyo kwa umri wako sasa Chauro unaujua hasa maudhi na undani wake) ambavyo babako ameshawahimfanyia mama yako naye amevumilia tu?
Wanawake tumeumbwa na busara (Ingawa inaitwa busara na ujanja wa nyoka) lakini ni kwa makusudi kabisa tumebarikiwa hilo, uvumilivu, huruma subira you name it. Ingawa kiubinadamu hatutofautiani but tuna ile ziada ya pekee.

Ni namna tu ya kucheza na akili yake.ushapewa utashi wa kujua udhaifu wake, kwa nini utumie nguvu kudeal naye?............
Si vizuri huu usemi lakini si wanasema Mbwa ukimjua jina?......................

Mimi pia ilinichukua miaka kujua namna ya kudeal na mwenzi wangu enzi hizo, nilikuwa sielewi kabisa kwa nini haelewi, hajui na anaignore!! ilinicost ninakiri.
 
Unafikiri Chauro? wala hakuna kazi yoyote. Ndio maana wanawake tuna sifa ya upekee ya uvumilivu...hivi umeshawahijiuliza visa ambavyo umeshawahi mtendea mama yako akavisamehe?? je umeshajiuliza visa (ambavyo kwa umri wako sasa Chauro unaujua hasa maudhi na undani wake) ambavyo babako ameshawahimfanyia mama yako naye amevumilia tu?
Eanawake tumeumwa na busara (Ingawa inaitwa busara na ujanja wa nyoka) lakini ni kwa makusudi kabisa tumebarikiwa hilo, uvumilivu, huruma subra you name it. Ingawa kiubinadamu hatutofautiani but tuna ile ziada ya pekee.

Ni namna tu ya kucheza na akili yake.ushapewa utashi wa kujua udhaifu wake, hwa nini utumie nguvu kudeal naye?............

kweli kabisa, busara zetu ndio zinazoweza kudumisha mahusiano,uvumilivu, kustahimili makubwa, ukishaingia kwenye ndoa bana ina bidi ujizatiti haswa, la sivyo utaona kila siku unaonewa
 
hivi kwa nini wanaume wengi ni wagumu kukiri udhaifu, makosa au kukabali kuwa kuna vitu hawavijui mbele ya mwanawake?, nimeona kwenye mahusiano huko ndio balaa,inahitaji hekima kumwambia mwanaume amekosea, au hicho anachokifahamu hakipo kama anavyodhania,na kama amekosea ndio kabisa hadi aje akubali kosa itachukua karne...,is it about man's ego ama? ( sio wote lakini)

...lol,..hata mimi sikubali kiurahisi namna hiyo,...[inategemeana na kosa]...kama umeona nimekosea nambie nikuelewe kwanini unaamini nimekosea, otherwise ukiwa ni mwepesi wa kujenga hoja, utabakia na msimamo wako nami nitabakia na wangu...
 
Lakini Nailyne ukichunguza vema kuna mabadiliko siku hizi (nadhani imechangiwa na malezi ya wazazi wengi ambao wamegundua kuwa mtoto wa kike na wa kiume anapaswa kulelewa kwa malezi yaliyo sawa.....ile mambo ya Jane, mtengee kaka yako chakula wakati Jane na John wote wametoka shule hakuna tena.......... John akifika anafungua Fridge anawasha Microwave anapasha chakula anakula. Ile hali ya kuogopwa hakuna tena na ndio maana tunashuhudia wanaume wanakiri na kupiga magoti mbele ya wapenzi wao wawapendao, tena wengine na machozi na kamasi juu!

Jamani mbarikiwe na Mwenyezi MUNGU awajaze hekima na maarifa. Tukumbuke wanawake tuna karama ya pekee sana tukitulia na kuivumbua (ndio maana tukaambiwa Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenywe) msemo huu haumaanishi kuwa mwanamke avumilie maovu au mabaya anayofanyiwa na mumewe bali unatoa ujumbe kuwa kama amebarikiwa mume bora, mwema na anayejali basi akitaka kumpoteza atampoteza kwa matendo yake na kukosa kwake maarifa..................... binafsi ninaamini kuwa usemi huu ulimaanisha kubomoa kile kilicho chema na kama tujuavyo si waume wote ni wema so kama MJ1 niliolewa na mume ambaye hakuwa mwema, nina amini kabisa kuwa kama binadamu mwingine awaye yote, nimebarikiwa akili na utashi wa kugundua baya na jema, kuwa hili anifanyialo mwanaume huyu si jema hata kidogo na halivumiliki, nikiamua kuyavunja maagano na mwanaume wa aina hii katu sijichukulii kama ni mpumbavu kama msemo huo unavyomaanisha............kwangu unaapply only and only if nimevunja maagano na mume mwema either kwa tamaa zangu au ujinga mwingine. Wanawake tuko responsible kwa maisha yetu, na ya familia zetu.
 
...lol,..hata mimi sikubali kiurahisi namna hiyo,...[inategemeana na kosa]...kama umeona nimekosea nambie nikuelewe kwanini unaamini nimekosea, otherwise ukiwa ni mwepesi wa kujenga hoja, utabakia na msimamo wako nami nitabakia na wangu...

mbu usiwaogope bwana waambie ukweli wao..
Bottomline wanawake wakishajua wao wako right na wewe uko wrong
mnaweza kuanza mgogoro mwingine kabisaa....hiyo inachangia vidume kuleta ubishi pia..
 
Unafikiri Chauro? wala hakuna kazi yoyote. Ndio maana wanawake tuna sifa ya upekee ya uvumilivu...hivi umeshawahijiuliza visa ambavyo umeshawahi mtendea mama yako akavisamehe?? je umeshajiuliza visa (ambavyo kwa umri wako sasa Chauro unaujua hasa maudhi na undani wake) ambavyo babako ameshawahimfanyia mama yako naye amevumilia tu?
Eanawake tumeumwa na busara (Ingawa inaitwa busara na ujanja wa nyoka) lakini ni kwa makusudi kabisa tumebarikiwa hilo, uvumilivu, huruma subra you name it. Ingawa kiubinadamu hatutofautiani but tuna ile ziada ya pekee.

Ni namna tu ya kucheza na akili yake.ushapewa utashi wa kujua udhaifu wake, hwa nini utumie nguvu kudeal naye?............
Si vizuri huu usemi lakini si wanasema Mbwa ukimjua jina?......................

Mimi pia ilinichukua miaka kujua namna ya kudeal na mwenzi wangu enzi hizo, nilikuwa sielewi kabisa kwa nini haelewi, hajui na anaignore!! ilinicost ninakiri.

MJ1 hakika wastahili pongezi kumbe kuna mapito ulipitia, yaelekea ulipambana.
 
...lol,..hata mimi sikubali kiurahisi namna hiyo,...[inategemeana na kosa]...kama umeona nimekosea nambie nikuelewe kwanini unaamini nimekosea, otherwise ukiwa ni mwepesi wa kujenga hoja, utabakia na msimamo wako nami nitabakia na wangu...
MBU mi naamini kwa mtu uliyekuwa naye katika mahusiano anapokuambia amekosea hana nia ya kukuonyesha kuwa wewe ni mmbaya bali ni kuanisha kitendo kilichofanyika hakijampendeza na labda kinachopelekea akiseme ni kutengeneza mazingira kitendo hicho kisirudiwe so ukiamua kubakiwa na msimamo wako kuwa hujakosea kisa mwenzio ameshindwa kujenga hoja kwa upande mwingine hutasolve tatizo.
 
the boss, unachojaribu kusema wale ambao wanakiri makosa hawaheshimiwi? Kwa hiyo wanaume kutokiri makosa ni katika kulinda heshima yake kwa mkewe?

yaani sijui niseme vipi unielewe...
Sometimes wanakosea tu
but sometimes wanawake,baadhi huwafanya wanaume waliokosea na kukiri kujutia uamuzi wa kukiri...
Inakuwa hayaishi...unakumbushiwa kila siku....
 
Wanaume wamebadilika labda unaongelea wanaume wa zamani sana miaka ya 1980-1990
hivi kwa nini wanaume wengi ni wagumu kukiri udhaifu, makosa au kukabali kuwa kuna vitu hawavijui mbele ya mwanawake?, nimeona kwenye mahusiano huko ndio balaa,inahitaji hekima kumwambia mwanaume amekosea, au hicho anachokifahamu hakipo kama anavyodhania,na kama amekosea ndio kabisa hadi aje akubali kosa itachukua karne...,is it about man's ego ama? ( sio wote lakini)
 
MBU mi naamini kwa mtu uliyekuwa naye katika mahusiano anapokuambia amekosea hana nia ya kukuonyesha kuwa wewe ni mmbaya bali ni kuanisha kitendo kilichofanyika hakijampendeza na labda kinachopelekea akiseme ni kutengeneza mazingira kitendo hicho kisirudiwe so ukiamua kubakiwa na msimamo wako kuwa hujakosea kisa mwenzio ameshindwa kujenga hoja kwa upande mwingine hutasolve tatizo.

...dahhh, umeniambia kwa lugha "laini" mwenyewe nimeelewa...
---it is not what you say, it is how you say it---...ndiyo inayo apply kwangu.
 
yaani sijui niseme vipi unielewe...
Sometimes wanakosea tu
but sometimes wanawake,baadhi huwafanya wanaume waliokosea na kukiri kujutia uamuzi wa kukiri...
Inakuwa hayaishi...unakumbushiwa kila siku....

nimekuelewa there so many factors behind this issues, na inaweza kuwa ni uoga wa wanaume kuamini akikubali kosa mkewe atamuonaje?atamsimanga? au ndo ataibua mgogoro mwingine
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom