Kwa nini uwekezaji/biashara mara nyingi hufa pindi mwanzilishi akifariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini uwekezaji/biashara mara nyingi hufa pindi mwanzilishi akifariki

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by ommy15, Apr 7, 2012.

 1. o

  ommy15 Senior Member

  #1
  Apr 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Habari wana jf,kwanza nawatakia sikukuu njema ya Pasaka,Mimi bainafsi napenda kuwa mfanyabiashara au muwekezaji na sio mfanyakazi(kuajiriwa). kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia sana historia za makampuni na bidhaa mbali mbali duniani na hasa hasa hapo wetu Tanzania. Lakini nimeona biashara nyingi sana huku kwetu zinatoweka pale mwenyewe akishafariki.

  Mfano naweza sema nimeona kwetu mbeya,kuna wazee walikuwa na hela na vitega uchumi vingi sana,lakini baada ya kufariki hizo biashara,mashamba na vitu vingine vyote huwa havidumu sana. Pia hii ipo hata kwenye biashara zetu hapa Tanzania kwa kweli kukuta biashara ya mswahili ina miaka 15 au 20 na zaidi ni mara chache kama sio hakuna.

  So najiuliza tunakosea wapi sisi na tulekebishe wapi? Kwani napenda kama natafuta mali au na wekeza sasa hiyo juhudi yote hata wajukuu zangu ambao siwafahamu kwa sasa wajewaufaike na jasho langu. Angalia wakina Mc Donalds tangu 1940,Unilevel na bidhaa nyingine kama Lux,lifebuoy sabuni ambazo za zamani lakini utazani ndio zinaingia sokoni
  .
   
 2. Red Giant

  Red Giant JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 9,485
  Likes Received: 5,953
  Trophy Points: 280
  hata mi hilo jambo huwa linanitatiza sana, halafu nahisi nikiwa na mali nyingi nikizeka ntakuwa na stress juu ya mali nilioacha, ila nna mpango wa kufanya lifuatalo
  1. ninapowekeza ntahakikisha nimetafuta wenzangu kama wawili tufanye pamoja na kuwa na share sawasawa hamuwezi kufa kwa pamoja!
  2. halafu kama mtaji mkubwa mnauza hisa (japo huko mbali sana)
  3.halafu kitu kingine ni kuwa transparent na kazi zako na kuwaandaa vizuri wale unaohisi utawaachia biashara
  nilikuwa nasoma kampuni ya kilimo cargill nilishangaa sana ilivyo survive au ile kampuni ya wal mart
   
 3. CONSULT

  CONSULT JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Nijambo la muhimu sana katika jamii yetu, ukipata muda tafuta vitabu vya entrepreneurship, pana topic/course iitwayo FAMILY BUSINESS SUCCESSION PLAN(Transfer Wealth to next generation), Ni nzuri sana factors mojawapo ni culture, early preparation to involve your successor in the business at least 10 yrs handover, lack of motivation, secret, lack of plan. etc bahati mbaya sijajua namna ya kua attach materials hapa ningewapeni -its a process not an envent.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  Nilkweli Biashara nyingi sana huwa zinakufa baada ya wamiliki wake kufariki, But kwa uchunguzi wangu ni zile zinazo milikiwa single, soleproprietorship ndo huwa zinakufa sana na si hapa Tanzania tu, make ukiwa wewe ndo mmiliki pekee ukifa maana yake Biashara lazima fe make sheria haziruhusu mwingine kuimiliki papo kwa hapo

  SABABU ZA KWA NINI ZINAKUFA

  1. Wamiliki wengi kuto kuweka msingi mzuri wa Biashara zao base kiasi kwamba hata akifa au akiugua muda mrefu ziendelee kuwepo,

  2. Kwa wamiliki mmoja mmoja kuto kuandaa warithi mapema sana, hapa ndo kuna shida kubwa sana,
  - MMILIKI KUWA MSIMAMIZI WA KILA KITU
  - KUTUMIA WAKE ZAKE/WATOTO/NDUGU NA JAMAA KUSIMAMIA BILA KUWAJENGEA UWEZO
  - kUSHINDWA KUANDAA SUCCESSION PLAN YA NANI ATAKUWA KIONGOZI WA HII BIASHARA PINDI NIKIFARIKI
  - Kuachia kikao cha mirathi kuamua nani wa kusimamia biashara ya marehemu bila kuangalia uwezo wa mteuliwa nayo factor kubwa sana
  - Mmiliki kuto kuwaendeleza watoto wake/mke/ndugu katika elimu ya biashara ili kuwajengea uwezo wa kibiashara wa kusimamia baishara na hivyo kuaha wasimamie kimazoea tu
  - Kutumia uchawi katika biashara inyo pelekea ukifa na nguvu za giza za biashara yako zinafikia tamati

  SULUHISHO NI NINI?

  1. Tujitahidi kuwa na makampuni na si kuendesha individual hii inaweza kuwa suluhisho


  2. Kuwajengea uwezo wasimamizi wa biashara yako tangia mwanzo na kuwaelimisha mambo mbalimbali yahusuyo biashara yako

  3. Kuandaa succession plan mapema sana ya nani atasimamia hii biashara pindi nikifa, na huyo aliyoko kwenye plan aandaliwe mapema kielimu na si mtu aliendaliwa aachwe akasomee kosi zingine tofauti na za biashara, hapa mmiliki ahakikishe mtoto wake atakaye mrithi anakua na mwelekeo wa masomo ya biashara sana na si mtoto anatazamiwa kurithi biashara za baba huku yeye achukua Degree ya KISWAHILI AU KITU KINGINE KISICHO ENDANA NA BIASHARA

  4. Kuwapa wasimamizi wako mazoezi ya vitendo means wawe wasimamizi kuanzia ukiwa bado hai na uwe mshauri wao tu, MFANO WAHINDI, VITOTO VYA WAHINDI VINAJUA BIASHARA VIKIWA BADO VIDOGO SANA TENA PRACTICALLY SIO THORETICALY
   
 5. Chipukizi

  Chipukizi JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 1,970
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wazazi wengi wa kiTZ awawikaribu na watoto wao katika biashara,so akifa baba ndo kwishney
   
 6. o

  ommy15 Senior Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Naomba jitahidi mkuu ufanye kuattach hizo copy ilinasisi tupate kuongeza uelewa,kwani hii kitu muhimu sana. Asante
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Watanzania wengi wanaona kuandaa mirathi (will) ni kujichulia. Kwa hiyo unakuta mtu ana fariki basi ndugu wanaishia kugombana. Hata kama ndugu wa nje wasipo gombania unakuta mtu kaacha watoto wa kiume kadhaa na wote hao wana gombania umiliki wa biashara zote bila kuangalia uwezo. Matokeo yake miradi inabidi igawanywe kila mtu achukue "ng'ombe wake. When that happens biashara lazima itakufa.

  Mtu unatakiwa kuandaa mrithi/warithi mapema. Una waingiza kwenye uongozi wa miradi. Kwa hiyo ukiondoka mtoto anaerithi uongozi ni yule mwenye cheo kikubwa zaidi ya wenzie. So mfano una mtoto mmoja ni deputy managing director na mwingine ni marketing manager inajulikana kabisa yule ambae ni deputy managing directo ndiyo next in line kuchukua uongozi na una liweka hili wazi ili pindi ukifa hamna power struggle. Pia hapa kuandika urithi ya nani achukue cheo kipi itasaidia.

  Cha mwisho kama tulivyo sema ni maandalizi. Unakuta baba ni msiri na biashara zake au watoto wanajua mzee ana biashara gani lakini hajui the ins and out ya hiyo business. So una kuta mfano mtoto ana kazi yake kwingine ghafla baba ana kufa anapewa biashara but hajui chochote.

  Cha mwisho ni bahati mbaya mkuu. Kwenye nchi kama za kwetu unakuta baba haishi muda mrefu na anakufa kutokana na sababu yoyote (ajali, magojwa ya kuepukika, kuuliwa). Sasa unakuta marehemu kaacha mtoto mdogo ambae obviously hawezi kutake over. Sawa anaweza akawa na mke but ni mara chache mtu hufanya biashara na mke au mumewe. Mama anakua na yeye na kazi zake. Sasa unakuta anaachiwa biashara hawezi iendeleza.

  Kwa hiyo mimi niseme kikubwa kinacho tuponza sisi ni utamaduni. Tuna utamaduni wa kuficha mali zetu, kwa maana mtu ana miradi yake lakini hata familia yake mwenyewe (mke, watoto) hawajui undani wa hizo biashara. Hii inaweza kutokana na mila za wanaume wa Kiafrika kuto kupenda au kuthamini ushauri wa mke au watoto kwa hiyo haoni maana ya kuwa shirikisha. Sababu nyingine ya kuto kushirikisha familia ni unakuta mtu anaendesha miradi yake kwa njia zisizo nzuri kama uchawi, ujambazi, ufisadi nk kwa hiyo hapo inakua ngumu kushirikisha familia. Cha mwisho ni utamaduni wetu wa kuona kujiandaa na kifo ni kama kujichulia. Kwa mtu anaona kuandika urithi au kuwa andaa warithi ni kama vile anajichulia kifo.
   
 8. nyatofundi

  nyatofundi Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Biashara za watanzania zina asili ya ubinafsi, kwa maana ya mmiliki kuivaa biashara kama nguo "that is PERSONALIZED" Biashara haipaswi kuwa hivyo. Biashara kama biashara ni mtu/binafsi/-"entity" kwa hiyo inapaswa kuendeshwa kwa misingi ya kitu kinachojitegemea, kiwe na usimamizi wanaoweza kumkemea hata mmiliki akitaka kutumia vibaya raslimali zake.

  Maana yake ni nini? biashara ina miiko yake " Business ethics code of conduct" Nenda kwenye search engines- iwe YAHOO/GOOGLE search for BUSINESS DICTIONARY/INVESTORS DICTIONARY YOU WILL LEARN A LOT THERE.

  Ili Biashara iwe endelevu(sustainable) inataka kuwe na "succession plan" wahindi, wachaga, waibo -nigeria, wayahudi middle east hufanya hivyo na wengi wao wamefaulu kwa kiwango cha juu wote tunaona na kusoma kwenye uzoefu wa "Entrepreneurship development". "Succession Plan" maana yake nikumwandaa mrithi wa shughuli ya sasa ili kusiwe na "gap" pindi mtenda shughuli hiyo atakapo staafu, kufa, kuacha kazi, kujiuzulu, kufukuzwa n.k. Watanzania wengi hasa wanaume huanza na kufanya biashara kwa kificho.

  Yaani, inashangaza familia yake haishirikishwi kuanzia mke na watoto hata ndugu wengine katika mchakato mzima wa kutafuta kuumba wazo la biashara(business idea formulation), uendeshaji wabiashara wenyewe, matumizi ya faida huwa ni siri ya mtu moja katika familia. Mmiliki wa biashara akijitahidi sana atashirikisha familia katika ngazi ya uendeshaji nayo kwa asilimia kidogo sana.

  Akipata mauzo mazuri atanunua vitu vya anasa/ visivyo vya lazima katika biashara bila kujali gharama za uendeshaji wa biashara yake- kama vile gari la kifahari. Wakati alipaswa kuvinunua kwa fedha ya gawiwo au mshahara wake anaojilipa ndani ya biashara. HIVI NI VIDODOKEZO VIDOGO NADHANI VITAKUONESHA NJIA -UNDANI ZAIDI SOMA KATIKA MTANDAO
   
 9. o

  ommy15 Senior Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  kwenye bluu,sisi watanzania wengi tukiwa na biashara faida/mauzo tunaiona kama ni mali yako. Mfano kuna kaka yangu alikuwa dereva taxi dar yeye alikuwa anaendesha gari yake na gari ya pili akampa dereva. sasa alichokuwa anafanya yeye ni kwamba alikuwa anajilipa kama anavyomlipa derava wake na alikuwa anaishi kwa kutegemea pesa hiyo hiyo bila kugusa yale mauzo. Nimeona imemsaidia kwani amep[iga hatua sana
   
Loading...