Fahamu kuhusu Uwekezaji katika Kilimo Biashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,495
5,531
Habari za wakati huu,

Leo nimeona nilete mjadala mdogo ndani ya mjadala mkubwa unaohusu sekta ya Kilimo.
Kabla ya kuingia katika mjadala niweke wazi kwamba mimi sio mkulima wala sio mfanya biashara inayohusu kilimo.Hata hivyo mimi ni mfuatiliaji wa masuala mbalimbali ya kilimo na Biashara na kwa kipindi cha zaidi ya miaka 15 nimekuwa nikufuatilia kwa karibu mwenendo wa sekta ya kilimo na biashara ya kilimo.Hivyo basi ninapoleta mjada huu nauleta ili tupeane maarifa na taarifa za masingi kuhusu biashara hii,fursa na changamoto.Lakini zaidi nauleta mjada huu kwa lengo la kuwaalika wengine pia ambao wanazao taarifa au uzoefu katika sekta hii ili nao waweze kuchangia maoni yao.

45% ya ardhi ya Tanzania inafaa kwa kilimo na kati ya hizo ni asilimia ndogo inayolimwa kikamilifu.Hii ni matokeo ya uwekezaji mdogo katika eneo hili.Takwimu zisizo rasmi zinaonesha kwamba iwapo kilimo kitafanyika kwa tija na kwa kuzingatia misingi ya kitaalamu na kibiashara kinaweza kuzalisha faida kubwa na kutengeneza ajira nyingi za mojamoja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.Serikali inachukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa ni moja ya sekta mama ambayo inaweza kuwa na TIJA na faida kwa uchumi.Katika mjadala wa leo napenda tuzungmze kuhusu KILIMO cha kibiashara.Napenda tujadili kilimo hiki katika msingi wa UWAZI ili wanaoweza kujifunza waweze kujifunza.Kilimo ninachozungumzia hapa ni KILIMO CHA MKATABA au CONTRACT FARMING.


Kilimo cha mkataba ni aina ya KILIMO ambacho hufanywa kwa makubaliano maalum baina ya Mkulima na mlaji au Mkulima na Mnunuzi.Mnunuzi anaweza kuwa mlaji au akawa ni mtu kati.Ninaposema mtu kati namaanisha kwamba ni wale ambao hununua mazao na kuyaongeza thamani au kuyauza kwa mlaji wa mwisho.Katika miaka ya karibu tumekuwa tukiwasikia watu wanoitwa JATU na MR.KUKU ambao wanafanya aina ya KILIMO ambacho kinaitwa kilimo au ufugaji wa mkataba ingawa serikali kupitia kwa wasimamizi wa sekta husika wameshindwa kutambua namna bora ya kufanya kazi na watu hawa.Hali hii imepelekea kuonekana kwamba KILIMO hiki au ufugaji huu ni utapeli.Lengo langu sio kuwajadili JATU au MR.KUKU na wala slengi kuwakosoa au kuwapigia upatu ila ninahitaji tu kuweka meza nzuri ya kuanzisha mjada huu wa KILIMO cha MKATABA.

Katika shughuli ya kilimo kuna kitu kinaitwa Value Chain.Katika Value Chain ya Kilimo kuna wazalishaji wa pembejeo,Wasambazaji wa pembejeo,Wakulima/Wafugaji,Wasambazaji wa mazao na mifugo,walaji wa ngazi ya kwanza na walaji wa ngazi ya mwisho(Final consumers).Ukitazama mnyororo huu wa thamani utaona kwamba katika kila ngazi ya uzalishaji na ulaji kuna inputs na outputs na hata baada ya kila hatua kuna wastes ambazo zinaweza kutumika katika mnyororo mwingine wa thamani.Swali ambalo watu wengi hujiuliza ni je niingiie katika sehemu fulani au hatua fulani ya mnyororo wa thamani?Je niingie kama afisa ugavi?Niingia kama muwekezaji?Je usalama wa Pesa yangu ukoje?Tukiitazama sekta ya KILIMO katika ukamilifu wake ni rahisi sana kutafuta namna ya kuitumia kikamilifu kuzalisha utajiri na thamani.

Swali la kujiuliza ni je ni kwa kiwango gani wataalamu wa kilimo,wakulima,wasambazaji wa pembejeo wauzaji na wasambazaji wa mazao na wazalishaji wengine katika mnyororo wa thamani katika biashara ya kilimo wamejijenga kitaasisi?Ukitembelea kituo cha UWEKEZAJI TIC au ukatembelea Benki ya Maendeleo ya KILIMO utaona kwamba rasilimali Pesa kwa ajili ya KILIMO na SERA za kusupport kilimo zipo lakini uelewa wa watu wengi na utayari wa watu wengi kuingia katika sekta ya KILIMO ni mdogo hali ambayo inafanya watu kujikuta wakilalamika na kulaumu bila kuchukua hatua.

Katika Kilimo cha Tanzania kuna Kilimo kwa ajili ya soko la ndani na Kilimo kwa ajili ya SOKO la Nje.Soko la Ndani ni soko ambalo ni la hapa Tanzania.Soko la Nje linahusisha soko la Africa Mashariki,Uchina,Ulaya na Sehemu zingine za Dunia.Kulima kwa ajili ya Soko la ndani ni tofauti na kulima kwa ajili ya SOKO la NJE kwani kila SOKO lina kanuni na mahitaji na masharti yake na hivyo basi ni muhimu kwako kufahamu mahitaji ya kila soko.Kwa mfano kulima kwa ajili ya soko la ndani hutahitaji vibali vingi kama vile vya TBS,wizara kilimo au viwanda vya Biashara lakini unaplima kwa ajili ya soko la nje ni lazima ufahamu kuhusu vibali hivyo na upatikanaje wake.Ni lazima ufahamu sheria za kikodi na kibiashara za nchi husika pia.

Mazao ya kilimo ambayo unaweza kulima yako ya aina tofauti unaweza kuchagua kulima mazao ya muda mfupi au mazao ya muda mrefu.Mazao ya muda mfupi ni mazao ya msimu au ya kilimo cha umwagiliaji.Uziri wa mazao ya msimu ni kwamba unaweza kutumia muda mfupi wa kati ya miezi 3 hadi 7 kwa kutegemea aina ya mazao.Unapofikiria mpango wako wa biashara ya kilimo ni lazima uzingatie vigezo na gharama unazotarajia kuziweka katika kilimo chako.Wengi huona kilimo hakina tija kwa sababu ya kufanya kilimo cha SIMU au kilimo cha kufuata mkumbo.matokeo yake watu wengi hujikuta wakipata hasara katika kilimo kwa sababu ya kutokufahamu taratibu na kanuni za Kilimo.Unapofanya kilimo ni lazima ufahamu kwamba KILIMO kinapimwa kwa kutegemea YIELD per hectare yaani kwa kuzingatia ukubwa wa eneo na ubora wa Mbegu.Huwezi kulima eneo dogo na kutumia mbegu zenye ubora mdogo na utarajie kupata mazao bora na ya kutosha kukupa faida.Hapa ndipo kiini cha mjadala wangu kilipo.Je unawezaji kulima kilimo chenye TIJA iwapo una mtaji mdogo na uelewa +uzoefu mdogo kuhusu KILIMO.

Njia Pekee ya kuweza kulima kilimo chenye TIJA hata ukiwa na mtaji mdogo ni kwa kufanya KILIMO cha Mkataba au Kufanya Collective Farming.Katika Kilimo kunakuwa na watu ambao wanamiliki eneo kubwa la kilimo ambao hawana uwezo wa kulima eneo lote na kunakuwa na watu ambao wanayo mitaji au vipato ambavyo vinaweza kuwawezesha kuwekeza katika kilimo katika eneo dogo lakini hakitakuwa na TIJA.Hivyo basi hawa watu wawili wanaweza kukaa mezani na kuingia katika makubaliano maalum ya kibiashara ya kuweza kufanya kilimo.Manweza kujiunga kama Kampuni yenye ukomo wa Hisa au kama JOINT venture Partnership ambapo kwa pamoja mnaweza kuchanganya Financial resources na Physical resources kama ardhi ili kujenga mfumo wa kibaishara ambao unaweza kukopesheka na hata kusimamia biashara.Ni Rahisi sana mkiwa mmejiunga katika aina fulani ya kikundi kuweza kufanya kazi kwa pamoja na kutambulika kitaifa na kimataifa.Jambo la muhimu ni kuendesha shughuli zenu za kilimo kibiashara na kuwa na usimamizi wa kibiashara kwa kuzingatia malengo yenu.Hili linawezekana.Jambo la Kujiuliza Je ni wangapi wanaweza kujiunga na kujitengeneza kama wawekezaji katika kilimo?Ninaelezea katika mfano hapo chini

Unaweza kuwa wewe unamiliki eneo la ardhi kubwa ambalo linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.Kunaweza pia kukawa na watu ambao wanao uwezo wa kifedha wa kuwekeza katika kilimo.Unachopaswa kufanya kwanza ni kufahamu bei ya chini kabisa ya Kitunguu katika SOKO kwa GUNIA.Pili unapaswa kufahamu kiasi ca uzalishaji klwa hectare na kwa eneo lote.Baada ya kuwa na hizo hesabu katika minimum.Unakuja kwenye Gharama za kilimo kuanzia BEI za Mbegu na Gharama nyingine zote mpaka kufika sokoni katika KIWANGO cha JUU.Projection za mavuno na mauzo unatumia Gharama za CHINI na Projection za Gharama unatumia Gharama za JUU kabisa ili upate Profit/Loss margin.Lengo la kupata hii Factor ya profit/Loss Margini ni kufahamu kiwango cha Risk ambacho unajiingiza.Baada ya kupata hii margin basi unaangalia Maximum price na maximu return ili uone kama kiwango cha Faida unayoweza pata kama maximum kinakupa ushawishi wa kuingia ktika KILIMO husika.Hiki tunakiita KILIMO cha kwenye makaratasi SIO kilimo halisia.Ukipata hii maximum yield inabidi uweke factor ya LOSS ambayo ni kawaida katika kilimo.Hapa unaweza tumia 40% kama baseline ambayo utaiapply katika maeneo yote yaani eneo la faida maximu na faida/hasara minimum.

Ukishakuwa na kilimo chako in numbers hatua ya pili ni kuamua cost per hectare ili unapozungumza na wabia wako ujue kabisa unahitaji kiwango gani cha uwekezaji,na unatarajia kiasi gani cha faida.Unapowaeleza waonesha ili maximum bila loss huku ukiwaeleza kuhusu Possible Loss nammna mabavyo utahakikisha unazizuia zisiwe kubwa.Ni lazima uwe na mpango wa kukata Bima ya kilimo kwa kutegemea ama ile maximum yield au minimum yield au gharama zako.Utaangalia ipi ni nafuu kwako.Umuhimu wa bima ni pale ambapo haufikii malengo ya wawekezaji wako unaweza kutumia bima kupunguza Losses zako na zao.Kama wewe ni mgeni katika kilimo husika ni lazima pia ujipe nafasi ya kufanya Pilot farming katika eneo husika kwa kulima eneo dogo ili uweze kuelewa changamoto zilizopo na namna ya kuzikabili hasa kwa kuwa unataka kulima kwa kutumia PESA za watu.

Katika mjada wangu sijagusia suala la masoko lakini ni muhimu ukaanza kuwa na mawasiliano na wanunuzi mapema kabisa.Hii itakuwezesha kuwa na uhakika wa soko.Hakuna kitu kinaumiza mkulima kama mazao yakizaa vizuri akakosa wateja.Inauma kuliko mazao kuharibikia shambani.Wawekezaji wako wakikubali kuwekeza usichukue Pesa zao na kuanza kupeleka shambani.Nenda kwenye taasisi za Fedha kama TADB kwa ajili ya Kupata access ya LOANS huku ukitumia ile back up ya wawekezaji wako kama guarantee ya malipo.Ukipata Access ya Mkopo usichukue Pesa na kuingiza shambani moja kwa moja.Tafuta Pia wauzaji wa Pembejeo ambao unaweza kuwa na makubaliano nao ya CREDIT kwa kutumia Mkopo wa Benki kama Guarantee.Hii yote inakusaidia kuwa na access ya LIQUID funds wakati wote wa KILIMO.Kuwepo kwa cash ya kutosha kunakuhakikishia kwamba unakuwa na STRESS kidogo na unafanya kazi kwa kujiamini na kuelewa kile unachofanya.Faida ya kuwa na hizi arrangements zote ni kwamba unakuwa unafanya kilimo cha kibiashara na sio cha Kibabaishaji.

Kama niliovoeleza Mimi sio mkulima,ila natambua kwamba humu JF wakulima wapo na wengi wanao uzoefu wa kivitendo katika kilimo so kwa kuchokoza mada hii naamni kwamba watakuja na maoni,michango na fursa ambazo zitawezesha wengine kufahamu fursa na changamoto katika kilimo.Hata hivyo kama umependa andiko au ungependa zaidi kufahamu kuhusu namna BORA ya kuingia katika kilimo na kuwa mzalishaji mkubwa unaweza kuwasiliana nasi kwa email masokotz@yahoo.com ili tuweze kushauriana na wewe juu ya namna bora ambavyo tunaweza kuongeza uwekezaji na uzalishaji katika kilimo.

Kuhusu SISI


Masoko Consulting ni Strategic Consulting Firm (Washauri waelekezi wa Kimkakati) ambao tunatumia mbinu za kisasa na utaalam wa kisasa katika kuwasaidia wateja wetu kutambua fursa na kuzitumia kwa ajili ya kukuza biashara zao na kukuza faida.Lengo letu ni kuwasaidi wafanyabiasha wadogo na wakati kubadilisha na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa biashara zao ili ziendane na dunia ya kisasa kwa kuwawezesha kufikia zana za kisasa,utaalamu wa kisasa na teknolojia katika kuendesha biashara zao.

Sisi tunatoa huduma ya usajili wa Majina ya biashara,kampuni,leseni,TIN number NGOs,Taasisi za Kijamii,SACCOS,Taasisi za KIDINI,Taasisi za ELIMU,Viwanda,UWEKEZAJI na pia tunatoa ushauri juu ya namna bora ya kuendesha biashara yako.Unaweza kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.Baadhi ya huduma hizo ni pamoja na:
  1. Kwanza tutakushauri kuhusu muundo wa biashara yako faida na hasara pamoja fursa mbalimbali
  2. Pili tutakufanyia utafiti na ushauri wa Jina la Biashara yako kwa kuzingatia vigezo vya SOKO
  3. Tutakufanyia Taratibu zote za usajili kuanzia Uandaaji wa Nyaraka Mpaka Kukamilika kwa Usajili Kampuni,TRA,Mashine za EFD na VFD,Vibali vya TBS pamoja na leseni
  4. Tutakuandikia Company Profile ya Kisasa kwa Lugha ya Kiingereza na Kiswahili
  5. Kama unahitaji mkopo kutoka katika taasisi za fedha tutakusaidia kufanya mchakato kwa kuzingatia mahitaji yako na vigezo vya taasisi husika.
  6. Tutakutengenezea Website ya kisasa kwa ajili ya Biashara na huduma zako.
  7. Tutakutengenezea, Logo, Business Card,Letter Head pamoja na Nyaraka nyingine za Kibiashara
  8. Tutakupatia Mfumo wa Kutunza kumbukumbu kwa njia ya Mtandao au kwenye Computer yako kwa ajili ya kusimamia Biashara yako
  9. Tutakufanyia Initial Marketing kwa Wateja wako (Inategemea aina ya biashara )wa Mwanzo ili kuwa na customer base ya kuanzia
  10. Pia tutakusaidia Mchakato wa Kufungua Bank Account kwa kutumia jina la Biashara yako (Deposit Ya Kwako)
  11. Tutakuwa nawe katika mchakato mzima wa kuendesha biashara yako mpaka itakapokuwa stable na wewe kupata uzoefu wa kutosha katika biashara yako.
 
Hapana.Huu sio mwaliko wa Jatu ni mwaliko wa Kujifunza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom