Kwa nini plate number hazijirudii na zipo 3 tu?

Wewe ndio ulie muelewesha huyo ndg kiufasaha, ninaimani km atasoma hii ameshaelimika

Ni hivi,
Gari za mwanzo kabisa kwenye huu mfumo zitakuwa zilianza na
T 001 AAA hadi T 999 AAA
then
T 001 AAB hadi T 999 AAB
zikaendelea
T 001 AAC hadi T 999 AAC
hizo herufi zikaendelea mpaka zikafika AAZ
zilivyofika AAZ zikaanza tena kama ifuatavyo
T 001 ABA hadi T 999 ABA
T 001 ABB hadi T 999 ABB
T 001 ABC hadi T 999 ABC
.
.
.
T 001 ABZ hadi 999 ABZ

ikaanza tena
T 001 ACA hadi 999 ACA

ukiendelea na huo mtiririko baadae utakuja kufikia mahali ukute namba T 999 AZZ
ambapo itabidi gari linalofuatia lianze na namba zenye herufi zinazoanzia na B yaani
T 001 BAA.
kwa hiyo kwa hii system mpaka magari yajaze hiyo combination ya namba na herufi sio leo wa la kesho ndo maana mpaka leo magari yaliyopo Tanzania yamefikia herufi D tu
huwezi kukuta gari lenye namba kwa mfano
T 345 EAA kwa sasa ila baada ya muda yataanza kuwepo.

namba zinaanzia 101 wakuu hadi 999. herufi A mpk Z bila kujumuisha I na O. sasa hisabati ndio inaanzia hapo
 
naomba kuuliza wakuu, kwa uelewa wangu ni kwamba plate number za gari hazipaswi kujirudia na ikitokea huwa ni kosa tu la kibinaadam, gari zote na pikipiki nyingi ambazo nimeshaziona mpaka sasa huwa number ni 3 mfano t 111 agg namba tatu ina maana ni kuanzia 100 mpaka 999 sasa inakuaje hizo namba tatu za hapo hazijirudii? Sidhani kama number ya kati ya 100 mpaka 999 ndo idadi ya gari zote tz pamoja na pikipiki. Nini huwa kinafanyika kwenye utoaji wa hizo namba naomba kufahamishwa kwa mwenye uelewa.

haziwezi kujirudia namba na herufi kwa gari moja, namba zikijirudia basi herufi hazitajirudia, na herufi zikijirudia namba unakuta ni tofauti, ukipiga hesabu (zinaitwa permutations unapata namba jumla zinazoweza kuandikwa bila kujirudi ni
10x9x8=720{kuanzia 0 mpaka 9}
herufi jumla ni
24x23x22x21=255,024(kuanzia a mpaka d}
asa jumla ya herufi na namba ukizichanganya
255,024x720=183617280
 
T 999 ZZZ itakuwa gari ya mwisho kabisa ni maoni yangu ya kimtazamo tu.
 
Umekosea mkuu kukokotoa,kwa hesabu yako,mfano namba T111 AAA isingekuwa inatumika
 
Hizo namba na alphabet zinaruhusu mpangilio 9*10*10*27*27*27= 17,714,700 tofaut, kwa hiyo idadi ya magari yenye namba tofaut ndo hiyo! Bado sana mpaka namba hizo ziishe zikiisha ndo tutatafuta mpangilio tofaut wa hizo namba
 
Mchango wako umeishia hapo mkuu? Kwamba ni shule za kata?

Unakumbana na hoja kama hizi kwa kuwa Huonyeshi kuelewa pamoja na jitihada za wadau kukujibu kwa njia nyepesi na rahisi.

Je, sasa Umepata jibu la swali lako na kulielewa?
 
T 472 AVH......inaweza ikawa T 742 HAV, T 427 AHV, T 247 VHA, T 274 AVH, T 724 HVA

Kwa maana hii number hujirudia karika set ila kwa mpangilio tofauti.
 
T 999 ZZZ itakuwa gari ya mwisho kabisa ni maoni yangu ya kimtazamo tu.

Itakua gari ya mwisho kivipi? Ina maana baada ya hapo watu hawatoruhusiwa kuingiza gari upya/mpya?? Wewe labda useme itakua ndio namba ya mwisho kwa mfumo huu, sio gari ya mwisho
 
Itakua gari ya mwisho kivipi? Ina maana baada ya hapo watu hawatoruhusiwa kuingiza gari upya/mpya?? Wewe labda useme itakua ndio namba ya mwisho kwa mfumo huu, sio gari ya mwisho

Ndicho nikimaanishacho na ndicho tunachokizungumzia hapa boss
 
Nimeziona gari strabag zinazojirudia namba, so concept ni hiyo tu namba zinajirudia isipokuwa herufi hakuna complications nyingine, shukrani kwa wote waliochangia wengine hawakuwa wanajua ingawa walidhani wanafahamu so hopefully ujinga umetoka
 
Vile vle mbal na probability kuna software ya microsoft office hutumika kupanga no randomly bila kujirdia
 
Hili swali limesaidia kuona jinsi gani watanzania wengi wanakariri masomo na sio kuelewa, kila mtu kakaa tu kusema mara probability mara permutations alafu kusolve zero, swali rahisi tu hata bila kusoma hizo hesabu unaweza jiongeza tu na kupata majibu.

T 111 AAA
Hapo kwenye namba 111 kuna uwezekano wa kua na namba 0-9 maana yake jumla unaweza kua na namba
Code:
9x10x10= 900
sababu namba zinajirudia alafu note nimeanza na 9 kwa assumption kua namba hazianzii zero, kama zinaweza anzia zero itakua 10x10x10, hapo mbele kwenye AAA kwa kua herufi zipo 26, kuna uwezekano wa kuwepo
Code:
[COLOR=#ff0000]26x26x26[/COLOR] = 17,576.
Jumla ya uwezekano wa namba zote ni
Code:
900x17576 = 15,818,400.

Kwa hiyo kuna uwezekano wa magari milioni 15 kupewa namba unique. Sidhani kama Tanzania kuna magari mengi kiasi hicho.

Wewe pekee mpaka muda huu ndo umefafanua ipasavyo, point ya kunote hapo kwenye red ni kwamba herufi I na O hazitumiki kwenye plate numbers, hivyo tunabaki na 24, hesabu itabadilika kuwa 9x10x10x24x24x24.

Asante.
 
duuuuh kweli mimi sijawahi ona namba zifanane ni ngumu kwanza kosa kisheria HERUFI HIZO SAWA
 
Naomba kuuliza wakuu, kwa uelewa wangu ni kwamba plate number za gari hazipaswi kujirudia na ikitokea huwa ni kosa tu la kibinaadam, gari zote na pikipiki nyingi ambazo nimeshaziona mpaka sasa huwa number ni 3 mfano T 111 AGG Namba tatu ina maana ni kuanzia 100 mpaka 999 sasa inakuaje hizo namba tatu za hapo hazijirudii? Sidhani kama number ya kati ya 100 mpaka 999 ndo idadi ya gari zote tz pamoja na pikipiki. Nini huwa kinafanyika kwenye utoaji wa hizo namba naomba kufahamishwa kwa mwenye uelewa.

Ni hivi,
Gari za mwanzo kabisa kwenye huu mfumo zitakuwa zilianza na
T 001 AAA hadi T 999 AAA
then
T 001 AAB hadi T 999 AAB
zikaendelea
T 001 AAC hadi T 999 AAC
hizo herufi zikaendelea mpaka zikafika AAZ
zilivyofika AAZ zikaanza tena kama ifuatavyo
T 001 ABA hadi T 999 ABA
T 001 ABB hadi T 999 ABB
T 001 ABC hadi T 999 ABC
.
.
.
T 001 ABZ hadi 999 ABZ

ikaanza tena
T 001 ACA hadi 999 ACA

ukiendelea na huo mtiririko baadae utakuja kufikia mahali ukute namba T 999 AZZ
ambapo itabidi gari linalofuatia lianze na namba zenye herufi zinazoanzia na B yaani
T 001 BAA.
kwa hiyo kwa hii system mpaka magari yajaze hiyo combination ya namba na herufi sio leo wa la kesho ndo maana mpaka leo magari yaliyopo Tanzania yamefikia herufi D tu
huwezi kukuta gari lenye namba kwa mfano
T 345 EAA kwa sasa ila baada ya muda yataanza kuwepo.
Hili swali limesaidia kuona jinsi gani watanzania wengi wanakariri masomo na sio kuelewa, kila mtu kakaa tu kusema mara probability mara permutations alafu kusolve zero, swali rahisi tu hata bila kusoma hizo hesabu unaweza jiongeza tu na kupata majibu.

T 111 AAA
Hapo kwenye namba 111 kuna uwezekano wa kua na namba 0-9 maana yake jumla unaweza kua na namba
Code:
9x10x10= 900
sababu namba zinajirudia alafu note nimeanza na 9 kwa assumption kua namba hazianzii zero, kama zinaweza anzia zero itakua 10x10x10, hapo mbele kwenye AAA kwa kua herufi zipo 26, kuna uwezekano wa kuwepo
Code:
26x26x26 =  17,576.
Jumla ya uwezekano wa namba zote ni
Code:
900x17576 = 15,818,400.

Kwa hiyo kuna uwezekano wa magari milioni 15 kupewa namba unique. Sidhani kama Tanzania kuna magari mengi kiasi hicho.
Sikumbuki kuwahi kuona magari ambayo namba zake zinaanza na tarkimu ya sifuri (0), ila kama yapo basi idadi ya magari yatakayoweza kusajiliwa kwa kufuata mfumo huu tulionao (na unaoendelea kusajili) yatakuwa kama ifuatavyo:

1. Kesi ya kwanza:
Kama kuna namba ambazo zinaanza na herufi ya sifuri (0), yaani T0... mfano T001, T002, ...:, basi idadi ya tarakimu za T(numba ya kwanza) (nama ya pili)(namba ya tatu), mfano T001, T002, .... na kuendelea ( kwa zile zitakazoanza na sifuri peke yake) zitakuwa:

10x10x9=900 (Hapa hatuna T000 kama ilivyo kwa zingine kama T111, T222,... na kuendelea, sifuri haiwezi kuwa mwisho).

Hivyo namba ya MWISHO ya zile zinazoanza na 0 inabidi iwe kati ya 1 na 9 TU na siyo kati ya 0 na 9 (SIFURI HAITUMIKI KAMA TARAKIMU YA MWISHO HAPA) na hivyo kupunguza idadi ya uwezekano wa kupata tarakimu ya MWISHO kutoka 10 hadi 9. Kumbuka kuwa tarakimu ya kwanza na ya pili zenyewe zitaendelea kubaki na idadi ile ile ya "kumi kumi" kwa sababu zenyewe zaweza kuwa yoyote kati ya 0 na 9.

Kufuatia maelezo haya hapa juu hii ina maana kuwa kuna namna 9 TU ambavyo tarakimu ya MWISHO inaweza kupatikana, kwa zile zenye mfumo wa T0.. , na vile vile namna 10 kwa tarakimu ya KWANZA na ya PILI.

Kwa zile zenye mfumo kuanzia T1... mpaka T9..., zina namna 9x10x10 kwa kila mfumo (Hapa tarakimu yoyote inaweza kuwa namba ya kwanza kati ya 1 mpaka 9, na ya pili na ya tatu inaweza kuwa yoyote kati ya 0 na 9)

Kwa hiyo kesi hii, jumla ya namba zote kuanzia T0... mpaka T9.. itakuwa (9x10x10)x10=9000

Lakini pia vile vile kuna herufi 26 kuanzia A mpaka Z. Lakimi ni MUHIMU sana tukakumbuka kuwa katika herufi hizi, mbili hazitumiki ambazo ni O (ambayo inafanana na sifuri) na I (ambayo inafanana na moja). Tunabaki na herufi 24 ambazo kwa mpangilio wa herufi "tatu tatu", zina namna

24x24x24= 13824. Hapa herufi inaweza kujirudia mfano AAA, BBB, CCC, .... Kwa hali hiyo magari yanayoweza kusajiliwa kwa

mfumo huu wa T0... mapaka T9... na A mpaka Z (bila ya herufi I na O) ni magari

13824x(10x10x10)-1=13,823,999 (tunatoa moja ile T000 ambayo haipo)

Kesi ya pili:

Kama hakuna magari yaliyosajiliwa kwa namba zinazoanza na T0... (yaani kwa mfano hakuna T001, T002, ...) basi magari yanayoweza kusajiliwa kwa mfumo huu ni 13824x(9x10x10)-1=12,441,599

Mbarikiwe wasomaji.
 
Back
Top Bottom