Kwa nini Lissu alidanganya bunge?

Kwa nini Lissu alidanganya bunge?

Atongwele

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2013
Posts
2,470
Reaction score
106
Tundu Lissu alitoa ufafanuzi wakati kuchangia mswada wa marekebisho ya katibu mjini dodoma juzi na kudai kuwa mswada huo umekuwa wa upande mmoja hasa kwa kutoshirikishwa kwa wadau kadhaa.

Lakini Lissu hakuweka wazi hao wadau anaowasema yeye ni akina nani au kunawadau wa chadema au wa lisu pakee ambao hawakushirikishwa?

===========================
UFAFANUZI wa Tundu Lissu
===========================

Kwa wanaomwamini Mwanasheria Mkuu, Lukuvi na maCCM wengine. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na utawala, na nilihudhuria vikao vyote vya Kamati wakati wadau wanatoa maoni yao mbele ya Kamati. In fact, niliondoka kwenda kwenye mikutano ya rasimu ya Katiba baada ya Kamati kukamilisha kazi ya kupokea maoni ya wadau na pia kuridhika kwamba Safari ya Zanzibar ilikuwa haiwezekani tena.

Kwa kifupi, Kamati ilitengeneza orodha ya wadau wa Zanzibar ambao tulitaka kuonana nao. Wadau hao ni hawa wafuatao:
1) Zanzibar Law Society
2) Zanzibar Female Lawyers Association
3) State University of Zanzibar
4) University of Zanzibar Tunguu
5) Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA)
6) Umoja wa Walemavu Zanzibar
7) Profesa Abdul Sheriff
8) Association of NGOs in Zanzibar (ANGOZA)

Ratiba ya Kamati ilikuwa inaonyesha kwamba Kamati ingeonana na wadau hawa Zanzibar Kati ya tarehe 14-16 Agosti. Kamati ilizuiliwa kwenda Zanzibar na kwa hiyo hakuna mdau hata mmoja wa Zanzibar aliyeonana na Kamati.

Mwanasheria Mkuu Werema amedai kwamba chama cha Jahazi Asilia walikuja kutoa maoni yao kwenye Kamati. Swali ni je, chama cha jahazi asilia ni chama cha Wazanzibari peke yao? Kwa kadri ninavyojua, Jahazi Asilia ni chama kilichosajiliwa Dar es Salaam sawa na CUF, CCM, CHADEMA, n.k. Hakuna chama cha siasa cha upande mmoja wa Muungano kwa maana ya kisheria. Vyama vyote vinatakiwa na Sheria ya Vyama Siasa kuwa vya Muungano. Notebook yangu ya kikao cha Kamati cha tarehe 30 Julai inaonyesha kwamba vyama vyote vya siasa, Jahazi Asilia included, vilitoa maoni siku hiyo. Hakuna hata kimoja kilichokuja kwa niaba ya Wazanzibari.

Kuhusu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikishwa kwenye maandalizi ya Muswada, hiyo vile vile ni ngonjera ya maCCM. Sisi kama Kamati hatukukutana na mwakilishi yeyote wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kipindi chote cha Muswada kuwa kwenye Kamati. Ukweli ni kwamba hata SMZ hawakushirikishwa mpaka Jumatatu ya wiki walipom-summon AG na Lukuvi Zanzibar baada ya Kamati kuhojinushirikishwaji wa Zanzibar katika Miswada yote miwili. Ndio maana ilibidi Muswada wa Sheria ya kura ya maoni uondolewe kwenye orodha ya shughuli za Bunge za wiki hii kwa sababu SMZ iliwaambia haiko tayari kutoa ridhaa yake. Huyo Mzee Iddi Sefu ametumiwa kuokoa jahazi la CCM Bungeni. Tutafahamu vizuri juu ya ukweli wa jambo hili very soon.

In fine, mimi sikudanganya chochote Bungeni. Ndio maana hao wanaodai nimedanganya hakuna hata mmoja aliyethubutu kuniambia nithibitishe kauli yangu vinginevyo niifute Kama inavyotakiwa na kanuni za Bunge. Na Kama nilikuwa nimekosa kweli, mimi ni Mtu wa kusamehewa na watu hawa kirahisi hivyo? Si ningefukuzwa Bungeni Kama Zitto mwaka fulani kwa jinsi walivyo na hasira na mimi?

All the best,

Tundu
 
zanzibar walishirikishwa viongozi wachache wa juu wa CCM walioko serikalini ..... kama hao ndio zanzibar lissu amekosea ila tunavyofahamu zanzibar ni zaidi ya viongozi wachache wa CCM serikalini
 
lissu hawajawai sema uongo ni wazi makundi yote hayakushirikishwa. walio shirikishwa ni wana ccm.

ilibidi na jahazi halisia waokoe jahazi kwa kusema wame shirikishwA lakini kama ilivyo kawaida ccm waligeuza mchakato huu ni wa kwao na ndio maana hatA kwenye kukusanya maoni ya wananchi na wanachama wao,walijifungia ndani ya chumba wao na viongozi wao wa juu wakabishana humo alAf wakasema wamekusanya maoni ya wanachama wao.

Na hata kwenye hili wanachama wao wa kiulizwa itabidi wa okoe jahazi kwa kusema wameshirikiswa lakuni hakuna.

Ccm wamegeuza swala la katiba kama ni la chama chao. wawashukuru jahazi hasilia walio hamuA kuokoa jahAzi la ccm.
 
Tundu lisu alitoa ufafanuzi wakati kuchangia mswada wa marekebisho ya katibu mjini dodoma juzi na kudai kuwa mswada huo umekuwa wa upande mmoja hasa kwa kutoshirikishwa kwa wadau kadhaa,
Lakini lisu hakuweka wazi hao wadau anaowasema yeye ni akina nani au kunawadau wa chadema au wa lisu pakee ambao hawakushirikishwa?

Uncle Deo
Umekuwa na hulka ya kujidhalilisha na kulidhaliisha jukwaa hili kwa post zako nyingi zinazoenda kwa ushabiki, umbumbumbu na sitofahau....., Tafadhali azima busara na hekima toka kwa mungu ujivishe utanzania sio ushabiki wa kwa ccm na kufanya mambo kama mfungwa akili huru.

a) Unauhakikagani kwamba data na maelezo ya ccm na pindi chana siyo ya kupindapinda na kuwahadaa watanzania?

b) Nani amethibitisha kwamba kati ya CCM, Pindi Chana na Lukuvi sio waongo? Uncle Deo umefanya utafiti wowote? thibitisha....

Marangapi CCM na dola yake imewahaada watanzania kupitia viongozi wake wa juu? mfano:-

1. Pinda Kulidanya bunge na watanzania kuhusu mgogoro wa vurugu za Arusha Polisi na chadema.....

2. Kikwete maisha bora kwa kila mtanzania ....... yamekuwa maisha duni kwelikweli kwa kila mtanzania...

3. Chagonja mwangosi ameuwawa na wafuasi wa chadema, picha zikamuumbuwa, hakujuwa kama kuna picha za wauwaji....

4. Kikwete, Lowasa na basili mramba ni majembe......Kama ni majembe mbona kavuliwa uwaziri mkuu na maramba anakesi ya uhujumu uchumi????

Nyinyi mliohitimu na kufuzu Elimu chini ya kawambwa na Mulugo mnatuabisha sana watanzania na kutufanya tuonekane

Taifa la mazezeta tusioweza kujipanga kwa lugha moja kutetea maslahi ya Taifa na watanzania kwa kauli moja.
 
zanzibar
walishirikishwa viongozi wachache wa juu wa CCM walioko serikalini .....
kama hao ndio zanzibar lissu amekosea ila tunavyofahamu zanzibar ni
zaidi ya viongozi wachache wa CCM serikalini

hivi tunaposema wadau tuna maana gani? mie nadhan katika hili, wadau muhimu ni serikali zote mbili na bunge pamoja na baraza la wawakilishi. Lisu alijichanganya sana. alijua ni ukusanyaji wa maoni
 
Uncle Deo
Umekuwa na hulka ya kujidhalilisha na kulidhaliisha jukwaa hili kwa post
zako nyingi zinazoenda kwa ushabiki, umbumbumbu na sitofahau.....,
Tafadhali azima busara na hekima toka kwa mungu ujivishe utanzania sio
ushabiki wa kwa ccm na kufanya mambo kama mfungwa akili huru.

a) Unauhakikagani kwamba data na maelezo ya ccm na pindi chana siyo ya
kupindapinda na kuwahadaa watanzania?

b) Nani amethibitisha kwamba kati ya CCM, Pindi Chana na Lukuvi sio
waongo? Uncle Deo umefanya utafiti wowote? thibitisha....

Marangapi CCM na dola yake imewahaada watanzania kupitia viongozi wake
wa juu? mfano:-

1. Pinda Kulidanya bunge na watanzania kuhusu mgogoro wa vurugu za
Arusha Polisi na chadema.....

2. Kikwete maisha bora kwa kila mtanzania ....... yamekuwa maisha duni
kwelikweli kwa kila mtanzania...

3. Chagonja mwangosi ameuwawa na wafuasi wa chadema, picha zikamuumbuwa,
hakujuwa kama kuna picha za wauwaji....

4. Kikwete, Lowasa na basili mramba ni majembe......Kama ni majembe
mbona kavuliwa uwaziri mkuu na maramba anakesi ya uhujumu uchumi????

Nyinyi mliohitimu na kufuzu Elimu chini ya kawambwa na Mulugo
mnatuabisha sana watanzania na kutufanya tuonekane

Taifa la mazezeta tusioweza kujipanga kwa lugha moja kutetea maslahi ya
Taifa na watanzania kwa kauli moja.

pamoja na yote uliyoandika, lakini kwa hili CHADEMA na LISSU wameaibika. maelezo yametolewa vizuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na yamejitosheleza. pia serikali ya mapinduzi Zanzibar ambayo ni ya ubia baina ya CUF na CCM imekiri kuwa imeshirikishwa na walitoa mchango wao. Ni aibu kwa chama cha upinzani kuumbuliwa hadharani
 
ila Wazanzibar wamehadharishwa kuwa makini katika hili. haijapatapo kutokea CHADEMA wakaipenda Zanzibar. pia wameambiwa na wazanzibari wenzao kuwa Lissu ni yule yule na ataendelea kuwa adui wa wazanzibari
 
Dr Kigwangwala anakazi ya ziada na mgonjwa wake bado hajapata nafuu
 
pamoja na yote uliyoandika, lakini kwa hili CHADEMA na LISSU wameaibika. maelezo yametolewa vizuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na yamejitosheleza. pia serikali ya mapinduzi Zanzibar ambayo ni ya ubia baina ya CUF na CCM imekiri kuwa imeshirikishwa na walitoa mchango wao. Ni aibu kwa chama cha upinzani kuumbuliwa hadharani

Lizaboni

Unatakiwa kujibu hoja acha siasa ndo nyinyi mliohitimu kimulugomulugo. Jibu hoja wewe badala ya kujitoa ufahamu wa kwamba hujaona kilichoulizwa?

a) Unauhakikagani kwamba data na maelezo ya ccm na pindi chana siyo ya
kupindapinda na kuwahadaa watanzania?

b) Nani amethibitisha kwamba kati ya CCM, Pindi Chana na Lukuvi sio
waongo? LIZABONI umefanya utafiti wowote? thibitisha....

Marangapi CCM na
dola yake imewahaada watanzania kupitia viongozi wake
wa juu? mfano:-

1. Pinda Kulidanya bunge na watanzania kuhusu mgogoro wa vurugu za
Arusha Polisi na chadema.....

2. Kikwete maisha bora kwa kila mtanzania ....... yamekuwa maisha duni
kwelikweli kwa kila mtanzania...

3. Chagonja mwangosi ameuwawa na wafuasi wa chadema, picha zikamuumbuwa,
hakujuwa kama kuna picha za wauwaji....

4. Kikwete, Lowasa na basili mramba ni majembe......Kama ni majembe
mbona kavuliwa uwaziri mkuu na maramba anakesi ya uhujumu uchumi????

Nyinyi mliohitimu na kufuzu Elimu chini ya kawambwa na Mulugo
mnatuabisha sana watanzania na kutufanya tuonekane

Taifa la mazezeta tusioweza kujipanga kwa lugha moja kutetea maslahi ya
Taifa na watanzania kwa kauli moja.
 
ila Wazanzibar wamehadharishwa kuwa makini katika hili. haijapatapo kutokea CHADEMA wakaipenda Zanzibar. pia wameambiwa na wazanzibari wenzao kuwa Lissu ni yule yule na ataendelea kuwa adui wa wazanzibari

hebu twambie ni kitu gani kibayA ameshawai kufanya au kusema lissu kuhusu zanzibar.

Hebu twambie ni lini na niwapi lissu amewachukia wazanzibari? hivi kweli unaweza ukawa unamchukia mtu alaf upiganie haki yake?

Tatizo hampendi kusikia ukweli na mkihusikia mnauchukulia ni chuki. hata wazanzibar walio wengi muungano hawaupendi lakini ccm wanalazimisha kwa manufaa yao ya kisiasa.

Uzuri wazanzibari wanajuA na wanamuelewa lissu, na ni wazi amewafumbua na wamefurahi.

lissu anaipenda zanzibar na wazanzibari ndio mAana anapigania haki zao kuhakikisha wanAsikilizwa wanachotaka.
 
Uncle Deo
Umekuwa na hulka ya kujidhalilisha na kulidhaliisha jukwaa hili kwa post zako nyingi zinazoenda kwa ushabiki, umbumbumbu na sitofahau....., Tafadhali azima busara na hekima toka kwa mungu ujivishe utanzania sio ushabiki wa kwa ccm na kufanya mambo kama mfungwa akili huru.

a) Unauhakikagani kwamba data na maelezo ya ccm na pindi chana siyo ya kupindapinda na kuwahadaa watanzania?

b) Nani amethibitisha kwamba kati ya CCM, Pindi Chana na Lukuvi sio waongo? Uncle Deo umefanya utafiti wowote? thibitisha....

Marangapi CCM na dola yake imewahaada watanzania kupitia viongozi wake wa juu? mfano:-

1. Pinda Kulidanya bunge na watanzania kuhusu mgogoro wa vurugu za Arusha Polisi na chadema.....

2. Kikwete maisha bora kwa kila mtanzania ....... yamekuwa maisha duni kwelikweli kwa kila mtanzania...

3. Chagonja mwangosi ameuwawa na wafuasi wa chadema, picha zikamuumbuwa, hakujuwa kama kuna picha za wauwaji....

4. Kikwete, Lowasa na basili mramba ni majembe......Kama ni majembe mbona kavuliwa uwaziri mkuu na maramba anakesi ya uhujumu uchumi????

Nyinyi mliohitimu na kufuzu Elimu chini ya kawambwa na Mulugo mnatuabisha sana watanzania na kutufanya tuonekane

Taifa la mazezeta tusioweza kujipanga kwa lugha moja kutetea maslahi ya Taifa na watanzania kwa kauli moja.

hizi ndo hoja brotha wengine wanakurupuka ka wanaishi Rwanda xo Tanzania
 
lissu hawajawai sema uongo ni wazi makundi yote hayakushirikishwa. walio shirikishwa ni wana ccm.

ilibidi na jahazi halisia waokoe jahazi kwa kusema wame shirikishwA lakini kama ilivyo kawaida ccm waligeuza mchakato huu ni wa kwao na ndio maana hatA kwenye kukusanya maoni ya wananchi na wanachama wao,walijifungia ndani ya chumba wao na viongozi wao wa juu wakabishana humo alAf wakasema wamekusanya maoni ya wanachama wao.

Na hata kwenye hili wanachama wao wa kiulizwa itabidi wa okoe jahazi kwa kusema wameshirikiswa lakuni hakuna.

Ccm wamegeuza swala la katiba kama ni la chama chao. wawashukuru jahazi hasilia walio hamuA kuokoa jahAzi la ccm.
Kamanda, unaenda mbali sasa punguza mahaba Tundu Lissu ni binadamu unampa sifa za mitume eti Tundu Lissu, hajawahi kusema uongo, teh teh teh.
 
hebu twambie ni kitu gani kibayA ameshawai kufanya au kusema lissu kuhusu zanzibar.

Hebu twambie ni lini na niwapi lissu amewachukia wazanzibari? hivi kweli unaweza ukawa unamchukia mtu alaf upiganie haki yake?

Tatizo hampendi kusikia ukweli na mkihusikia mnauchukulia ni chuki. hata wazanzibar walio wengi muungano hawaupendi lakini ccm wanalazimisha kwa manufaa yao ya kisiasa.

Uzuri wazanzibari wanajuA na wanamuelewa lissu, na ni wazi amewafumbua na wamefurahi.

lissu anaipenda zanzibar na wazanzibari ndio mAana anapigania haki zao kuhakikisha wanAsikilizwa wanachotaka.
Tundu Lissu, ni mnafiki kila siku anawambia Wazanzibar kuwa Zanzibar siyo nchi dogo hilo, leo anajifanya kuwatetea juzi kawambia CUF ni chama cha Zanzibar tu leo tena anajifanya kuwatetea.

Ndiyo maana CUF na CCM, Zanzibar wamemwambia atujakutuma kutusemea una agenda yako ya siri dhidi ya Zanzibar.
 
EZEKIEL MAIGE; Mbunge wa Msalala CCM, NAIBU Spika,Hakuwa sahihi kutomsikiliza Mbowe!
Baada ya Jauzi jana na leo kuendelea kwa malumbano bungeni kati ya Naibu Spika,wabunge wa CCM kwa upande mmoja na Wabunge wa upinzani kwa upande wa pili wakiongozwa na CDM,wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao juu ya kile kilichojiri jana wakati wa kikao cha bunge la Mchana baada ya Naibu Spika kutumia Askari wa bunge kumtoa nje KUB,hali iliyopelekea tafrani kubwa sana.

Akitoa maoni yake ktk ukurasa wa Facebook,Mh Ezekiel Maige mbunge wa Msalala alisema kuwa hakuona sababu kabisa ya kufikia hapo kwani hali hiyo ingewezwa kuepushwa.

Ingewezekana kabisa kuahirishwa kwa muswada huo na kutoa nafasi kwa kamati ya katiba na sheria kwenda Zanzibar kupata maoni ya wenzetu huko.

Najuwa kuna maelezo mazuri ya kushirikishwa kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,lakini Kikanuni baada ya muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza unakuwa mikononi mwa Bunge.Kamati ndio inayokusanya maoni na sio serikali.

Kwa kuwa hakuna ushahidi wa Public hearing iliyofanyika Zanzibar na kuwasikia Wazanzibari wa kawaida(nje ya serikali) basi kulikuwa na haja kabisa ya kurekebisha kasoro hiyo kwa kutoa nafasi kwa kamati kwenda Zanzibar!!

Swala la katiba ni swala kubwa hivyo ni vema zikafanyika jitihada za kutosha kuhakikisha tunakwenda pamoja(na wenzetu haswa wenye mtazamo tofauti na sisi CCM) badala ya kutumia "Wingi wetu" kwani mwisho wa safari tukienda hivi watakuwepo watakaodai kuwa katiba mpya sio yao na hivyo kuikosesha "Social legitimacy"!!

Kwa kiti (Naibu Spika) kutomsikiliza Mh Mbowe (KUB) nako kulitibua mambo bila sababu ya msingi.
Angepewa nafasi ya kusikilizwa hata kama hoja yake isingekubaliwa bado ingekuwa nafuu sana kuliko shari na aibu ya jana iliyotokea.

Tumesameheana lakini tujifunze na tujitahidi sana kwenda kwa maelewano.

Mungu ibariki Tanzania. By Ezekiel Maige mbunge wa Msalala kupitia CCM.

Ndivyo alivyoandika mh Ezekiel. Binafsi nimependa sana mada yake hii japo siamini kuwa km angekuwepo juzi na jana bungeni nae angeto maoni haya kwa chama chake.!! Nawasilisha.
 
pamoja na yote uliyoandika, lakini kwa hili CHADEMA na LISSU wameaibika. maelezo yametolewa vizuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na yamejitosheleza. pia serikali ya mapinduzi Zanzibar ambayo ni ya ubia baina ya CUF na CCM imekiri kuwa imeshirikishwa na walitoa mchango wao. Ni aibu kwa chama cha upinzani kuumbuliwa hadharani

Unataka kutuaminisha kwamba wabunge wote wa CUF waliotoka nje ya ukumbi wa bunge akili zao haziko sawasawa?je hawana maeasiliano na serikali yao ya ubia?kumbuka maalimu Seif yuko Ikulu ya ZNZ na ni katibu mkuu wa CUF.je unataka kutuaminisha kuwa wabunge hawa hawana maeasiliano?walioshirikishwa ni wana ccm wachache waliko serikalini tu.huo ndio ukweli.
 
EZEKIEL MAIGE; Mbunge wa Msalala CCM, NAIBU Spika,Hakuwa sahihi kutomsikiliza Mbowe!
Baada ya Jauzi jana na leo kuendelea kwa malumbano bungeni kati ya Naibu Spika,wabunge wa CCM kwa upande mmoja na Wabunge wa upinzani kwa upande wa pili wakiongozwa na CDM,wadau mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni yao juu ya kile kilichojiri jana wakati wa kikao cha bunge la Mchana baada ya Naibu Spika kutumia Askari wa bunge kumtoa nje KUB,hali iliyopelekea tafrani kubwa sana.

Akitoa maoni yake ktk ukurasa wa Facebook,Mh Ezekiel Maige mbunge wa Msalala alisema kuwa hakuona sababu kabisa ya kufikia hapo kwani hali hiyo ingewezwa kuepushwa.

Ingewezekana kabisa kuahirishwa kwa muswada huo na kutoa nafasi kwa kamati ya katiba na sheria kwenda Zanzibar kupata maoni ya wenzetu huko.

Najuwa kuna maelezo mazuri ya kushirikishwa kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,lakini Kikanuni baada ya muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza unakuwa mikononi mwa Bunge.Kamati ndio inayokusanya maoni na sio serikali.

Kwa kuwa hakuna ushahidi wa Public hearing iliyofanyika Zanzibar na kuwasikia Wazanzibari wa kawaida(nje ya serikali) basi kulikuwa na haja kabisa ya kurekebisha kasoro hiyo kwa kutoa nafasi kwa kamati kwenda Zanzibar!!

Swala la katiba ni swala kubwa hivyo ni vema zikafanyika jitihada za kutosha kuhakikisha tunakwenda pamoja(na wenzetu haswa wenye mtazamo tofauti na sisi CCM) badala ya kutumia "Wingi wetu" kwani mwisho wa safari tukienda hivi watakuwepo watakaodai kuwa katiba mpya sio yao na hivyo kuikosesha "Social legitimacy"!!

Kwa kiti (Naibu Spika) kutomsikiliza Mh Mbowe (KUB) nako kulitibua mambo bila sababu ya msingi.
Angepewa nafasi ya kusikilizwa hata kama hoja yake isingekubaliwa bado ingekuwa nafuu sana kuliko shari na aibu ya jana iliyotokea.

Tumesameheana lakini tujifunze na tujitahidi sana kwenda kwa maelewano.

Mungu ibariki Tanzania. By Ezekiel Maige mbunge wa Msalala kupitia CCM.

Ndivyo alivyoandika mh Ezekiel. Binafsi nimependa sana mada yake hii japo siamini kuwa km angekuwepo juzi na jana bungeni nae angeto maoni haya kwa chama chake.!! Nawasilisha.
Hayo ni mawazo ya Maige mie hayanihusu kamanda.
 
Tundu lisu alitoa ufafanuzi wakati kuchangia mswada wa marekebisho ya katibu mjini dodoma juzi na kudai kuwa mswada huo umekuwa wa upande mmoja hasa kwa kutoshirikishwa kwa wadau kadhaa,
Lakini lisu hakuweka wazi hao wadau anaowasema yeye ni akina nani au kunawadau wa chadema au wa lisu pakee ambao hawakushirikishwa?

kulidanganya bunge kuna adhabu zake..mbona hakuambiwa hata afute kauli? tafakari...
 
lkwa ccm zanzibar serikali ndio inajulikana lakini kwa bara baraza la maaskofu,asasi za kiraia na vyuo vikuu walitoa maoni lakini cha kujiuliza kwa nini serikali ya muungano na zanzibar hazikukaa kuamua katiba?
 
Back
Top Bottom