pamoja na yote uliyoandika, lakini kwa hili CHADEMA na LISSU wameaibika. maelezo yametolewa vizuri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na yamejitosheleza. pia serikali ya mapinduzi Zanzibar ambayo ni ya ubia baina ya CUF na CCM imekiri kuwa imeshirikishwa na walitoa mchango wao. Ni aibu kwa chama cha upinzani kuumbuliwa hadharani
Kwa wanaomwamini Mwanasheria Mkuu, Lukuvi na maCCM wengine. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Katiba, Sheria na utawala, na nilihudhuria vikao vyote vya Kamati wakati wadau wanatoa maoni yao mbele ya Kamati. In fact, niliondoka kwenda kwenye mikutano ya rasimu ya Katiba baada ya Kamati kukamilisha kazi ya kupokea maoni ya wadau na pia kuridhika kwamba Safari ya Zanzibar ilikuwa haiwezekani tena.
Kwa kifupi, Kamati ilitengeneza orodha ya wadau wa Zanzibar ambao tulitaka kuonana nao. Wadau hao ni hawa wafuatao:
1) Zanzibar Law Society
2) Zanzibar Female Lawyers Association
3) State University of Zanzibar
4) University of Zanzibar Tunguu
5) Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA)
6) Umoja wa Walemavu Zanzibar
7) Profesa Abdul Sheriff
8) Association of NGOs in Zanzibar (ANGOZA)
Ratiba ya Kamati ilikuwa inaonyesha kwamba Kamati ingeonana na wadau hawa Zanzibar Kati ya tarehe 14-16 Agosti. Kamati ilizuiliwa kwenda Zanzibar na kwa hiyo hakuna mdau hata mmoja wa Zanzibar aliyeonana na Kamati.
Mwanasheria Mkuu Werema amedai kwamba chama cha Jahazi Asilia walikuja kutoa maoni yao kwenye Kamati. Swali ni je, chama cha jahazi asilia ni chama cha Wazanzibari peke yao? Kwa kadri ninavyojua, Jahazi Asilia ni chama kilichosajiliwa Dar es Salaam sawa na CUF, CCM, CHADEMA, n.k. Hakuna chama cha siasa cha upande mmoja wa Muungano kwa maana ya kisheria. Vyama vyote vinatakiwa na Sheria ya Vyama Siasa kuwa vya Muungano. Notebook yangu ya kikao cha Kamati cha tarehe 30 Julai inaonyesha kwamba vyama vyote vya siasa, Jahazi Asilia included, vilitoa maoni siku hiyo. Hakuna hata kimoja kilichokuja kwa niaba ya Wazanzibari.
Kuhusu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikishwa kwenye maandalizi ya Muswada, hiyo vile vile ni ngonjera ya maCCM. Sisi kama Kamati hatukukutana na mwakilishi yeyote wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kipindi chote cha Muswada kuwa kwenye Kamati. Ukweli ni kwamba hata SMZ hawakushirikishwa mpaka Jumatatu ya wiki walipom-summon AG na Lukuvi Zanzibar baada ya Kamati kuhojinushirikishwaji wa Zanzibar katika Miswada yote miwili. Ndio maana ilibidi Muswada wa Sheria ya kura ya maoni uondolewe kwenye orodha ya shughuli za Bunge za wiki hii kwa sababu SMZ iliwaambia haiko tayari kutoa ridhaa yake. Huyo Mzee Iddi Sefu ametumiwa kuokoa jahazi la CCM Bungeni. Tutafahamu vizuri juu ya ukweli wa jambo hili very soon.
In fine, mimi sikudanganya chochote Bungeni. Ndio maana hao wanaodai nimedanganya hakuna hata mmoja aliyethubutu kuniambia nithibitishe kauli yangu vinginevyo niifute Kama inavyotakiwa na kanuni za Bunge. Na Kama nilikuwa nimekosa kweli, mimi ni Mtu wa kusamehewa na watu hawa kirahisi hivyo? Si ningefukuzwa Bungeni Kama Zitto mwaka fulani kwa jinsi walivyo na hasira na mimi?
All the best,
Tundu