Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 57,707
- 91,649
Kwa nini Kanisani na misikitini viongozi wakubwa na matajiri hupewa umuhimu, kipaumbele au nafasi za mbele zaidi ikiwa kwa mungu watu wote ni sawa? Mfano RC kuna kitu kinaitwa Wakatoliki wa nguvu.Wiki hii Padri Kitima akiwa Bariadi kwenye shughuli ya kusimikwa Askofu aliwaita jukwaani Wakatoliki wa nguvu, Jenerali Mabeyo, Andrew Chenge(ambaye ni fisadi mmojawapo wa pesa za escrow) na jaji Mihayo wawasalimie maaskofu.
Kwenye Uislamu nako mbinguni au jannah zipo za madaraja tofauti kwa hiyo muislamu usitegemee sana ukifa au baada ya kiama kwamba utaenda kukaa mbingu moja na Nabii Ibrahim au mtume Muhamad, pia hatujui kama ahadi ya idadi mabikira itakuwa sawa mbingu zote, huenda wengine wakapata wachache zaidi.