Uchambuzi wa kauli ya raisi Magufuli kwa viongozi wa Dini katika muktadha wa COVID-19

Dseni

Member
Aug 13, 2012
33
125
UCHAMBUZI WA KAULI YA RAIS MAGUFULI KUHUSU VIONGOZI WA DINI KATIKA MUKTADHA WA COVID-19

Na: Mchungaji Daniel Seni

Tarehe 3/5/2020 raisi John Joseph Pombe katika hafla ya kuapishwa kwa waziri mpya wa Katiba na Sheria, Dr. Mwigulu Nchemba, aliyeteuliwa kutokana na kufariki kwa aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo ndugu Agostino Mahiga. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine mengi, aliwanyooshea kidole baadhi ya viongozi wa dini kwa ajili ya misimamo yao kuhusu korona na ibada kanisani au misikitini.
Baada ya kusikiliza kwa makini hotuba yake, hasa kipengele cha viongozi wa dini, nimeona nichambue ili tujiridhishe uhalali wa malalamiko yake.
Ningependa ninukuu maneno haya;

“…lakini pia tuendelee kumwomba Mungu wetu, Mungu yupo. Wapo hata viongozi wa dini wengine wamemsahau Mungu ambaye kila siku wamekuwa wakituhubiria; wanashika vitabu wanafahamu juu wa akina Daniel walivyokaa kwenye matumbo ya samaki (ni Daniel?) Daniel ni kwenye moto, wapo wengine walitupwa kwenye moto, wapo wengine walitupwa kwenye simba, simba hakuwala, kwa sababu walimtegemea Mungu. Leo kuna viongozi wa dini wameanza kuyumba na kumsahau Mungu ambaye waliapa, ndio kiapo chao; Biblia au Korani, wameanza kuisahau na kuiweka pembeni na kuweka ubinadamu mbele; acheni kuomba, tunajiokoa, acheni sijui nini nini, ni mambo ya ajabu, lakini ndiyo hivyo, katika kipindi hiki cha mpito tutayasikia mengi, na huu ndio wakati wa kuwapima imani viongozi tulio nao, hata viongozi wa dini. Ukizuia waumini wako wasiende kanisani, ukazuia watu wasiende msikitini, na unaweza kukuta msikiti huo hukuujenga wewe, umejengwa na hao waumini, hili nalo ni suala la ajabu la kujiuliza, si uwaachie hao waumini wafungulie waende wenye nia yao waende wakamwombe Mungu., hata kama wewe hutaenda kuhubiri pale! Ndiyo haya tutayaona, hizi ni changamoto, na mimi nawaomba Watanzania tuendelee kumwomba Mungu, na Mungu atatusaidia kutupitisha katika changamoto hizi…”mwisho wa kunukuu.

Ukiangalia katika nukuu hiyo hapo juu, raisi anaongelea dini mbili; Ukristo na Uislamu, hata hivyo mifano ya Kibiblia aliyoitoa ni kutoka katika Ukristo; labda pengine kwa sababu ni Mkristo. Katika Makala haya, nitajadili kwa upande wa viongozi wa dini wa Kikristo kwa sababu sina uzoefu wa kutosha katika upande wa pili wa dini. Napenda kujikita katika hoja ambazo raisi ameziweka kwa ajili ya kuthibitisha lawama zake kwa viongozi wa dini, na je lawama hizo zikoje kwenye muktadha wa Kitheologia.

Mifano kutoka kwenye Biblia; Daniel 6:16-22 (kuna kosa lilifanyika kidogo katika kutamka, raisi alichanganya habari ya Daniel na Yona). Ninachotaka kukichambua mahali hapa ni; je raisi alikuwa sahihi kutumia maandiko hayo katika muktadha wa korona?

Kwa mujibu wa Mch. Edwin Mihigo katika video aliyoiweka kwenye akaunti yake ya facebook tarehe 2/5/2020 siku moja kabla ya hotuba ya raisi yeye anasema hivi “swala la Daniel ni tofauti kabisa na mazingira ya korona, yeye ukiangalia alizuiliwa asiabudu; na alipoamua kumwabudu Mungu, basi ikabidi ahukumiwe. Tukio hili limelenga kumthibitisha Mungu wa Israel.”[1] Ameeleza mambo mengi lakini mwisho akasema tu kwamba; suala la korona si kwa ajili ya wasioamini tu, bali ni kwa watu wote. Suala muhimu ni kujilinda. Unaweza kubonyeza link hiyo kusikiliza mpaka mwisho.

Katika matukio kama haya, Wakristo katika vipindi vyote vya Biblia (Agano la Kale na Agano Jipya) wamekuwa na mitizamo tofauti tofauti. Kila mmoja amekuwa akisisitiza msimamo ambao anaamini ni sahihi kabisa. Tukiachilia masuala ya akina Daniel, Yona na wengineo; tunaweza kuona pia mateso ya kanisa la kwanza.

Je ni sahihi kutumia vifungu hivyo katika muktadha huu wa Korona? Nitaeleza kwa kuzingatia pande zote mbili; upande wa kwanza ni sawa (kwa kuzingatia muktadha wa msemaji) na upande wa pili si sawa (kwa kuzingatia muktadha wa Kitheologia)

UHALALI WA KUTUMIA VIFUNGU HIVYO KATIKA KUPAMBANA NA KORONA

a) Kwa kuzingatia muktadha wa msemaji (ambaye ni raisi Magufuli) lengo lake hawa siyo kuwaambia watu waache kujikinga na ugonjwa wa korona; kusudi lake ni kule kuonyesha kwamba Mungu anaweza kuwatoa hata katika janga hili kubwa la Corona. Na ndiyo maana anaanza kwa kusema “lakini pia tuendelee kumwomba Mungu wetu,” na anamalizia kwa kusema “tuendelee kumwomba Mungu, na Mungu atatusaidia kutupitisha katika changamoto hizi.”

Kwa muktadha huohuo, unaweza kugundua kwamba rais Magufuli ametumia habari za Daniel na Yona si kwa kuwazuia watu kujikinga au kutozingatia taratibu za kiafya, bali ni kwamba Mungu yupo, na kwamba anaweza kutusaidia.

b) Kwa kawaida tunapokuwa kwenye maombi mara nyingi huwa tunarejelea vifungu mbalimbali vya Biblia. Hivyo basi si kosa kwa raisi Magufuli kurejelea vifungu hivyo; hata kama alikosea kosea lakini dhana inabaki palepale kwamba lengo lake ilikuwa ni kuonyesha watu “Umuhimu wa kumtegemea Mungu.” Swali la kujiuliza labda je vifungu hivi hatuvitumii kwenye kuombea watu wanapokuwa kwenye shida? Je vifungu vya Zaburi 118:17 kwamba “sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana” huwa mnavirejelea kwenye maombi mkimaanisha kwamba kweli hamtakufa? Ni dhahiri kwamba huwa tunarejelea vifungu mbalimbali vya Biblia tunapokuwa kwenye maombi au kwenye changamoto zozote katika maisha yetu.

c) Kuhusu kwamba ugonjwa huu unaua watu wote; nakubali 100% kabisa lakini lazima kuna kitu cha kusema. Ukisikia watu walifunga siku 40 kavu wakafa kwa njaa; haimaanishi kwamba usifunge. Kama ukisikia kwamba kuna taifa fulani wamekufa watu laki 1 leo haimaanishi kwamba hata nchini kwako wanaenda kufa hao laki 1. Wakati wa magonjwa, watu wa aina zote wanakufa; uwe mpagani, mkristo, mwislamu, nk…lakini hii haimaanishi kwamba mtu aache imani yake kwa Mungu. Hii inamaanisha kwamba wakati unamtegemea Mungu ni lazima pia unahitaji kuzingatia kanuni hizo. Mkristo unapaswa kuomba mpaka usikie sauti “Neema yangu yakutosha” (kama Paulo alivyosikia)…bila kusahau kwamba unahitaji kutumia mbinu/dawa zilizopo kwa wakati huo. Paulo alimwambia Timotheo “atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake;” hapa Paulo alikuwa ana uwezo wa kumwambia afunge, lakini kwa sababu ya shida ya tumbo, Timotheo alikuwa hawezi kufunga-hata hivyo bado Paulo aliomba kwa ajili ya Timotheo.

d) Katika Maandishi ya Martin Luther, yeye alichukulia “mlipuko wa magonjwa” kama jaribu ambalo linajaribu kuthibitisha imani yetu na upendo kwa Mungu: akasisitiza “Wakristo lazima kwanza wachague kutimiza mapenzi ya mwili au ya Mungu"imani yetu ili tuweze kuona na kuona jinsi tunapaswa kutenda kwa Mungu. Luther aliwaruhusu Wakristo kufanya maamuzi ya kibinafsi kuhusu aidha kukimbia au kukabili kifo.
Hebu kabla hatujaendelea upande wa pili wa makala haya, ningependa kujadili kidogo hoja ya raisi magufuli kwa watumishi wa Mungu hawa. Nimejaribu kuchambua dhamira tano (5) muhimu katika kama kiini cha malalamiko na tuangalie uhalali wake.

a) Viongozi kushindwa kusimamia yale wanayohubiri. Raisi Magufuli anasema “Wapo hata viongozi wa dini wengine wamemsahau Mungu ambaye kila siku wamekuwa wakituhubiria.” Ukiangalia tamko hilo ni dhahiri kwamba wapo watumishi ambao wameshindwa kusimama katika yale wanayosimama nayo. Makanisa ya mitume na Manabii kwa sasa wako kimya kabisa. Lakini kila mara wamekuwa wakihubiri kwamba wao wanaponya HIV, Kansa, na magonjwa mengine sugu..kwa sasa raisi anaona kama wameyumba vile. Nina hakika Tanzania wako watumishi wa Mungu wanaoomba sana usiku na mchana kwa ajili ya korona iondoke; lakini raisi anasema kuna baadhi kumbe wao wanatuambia tutapona—kumbe wanajua hatutapona. Hawaamini kile wanachosema.

b) Wanashindwa Kuamini Yaliyofanyika katika Historia; Raisi Magufuli anasema “Wanashika vitabu wanafahamu juu wa akina Daniel… walimtegemea Mungu.” Hapa kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba matukio yote yaliyofanyika katika historia yanalenga kutufundisha sisi tusimame katika imani. Changamoto ya watumishi wa Mungu wa leo ambao raisi anawasema ni kwamba “wanaogopa kufa.” Hawana uhakika na wokovu wao! Hawana “security.” Hivi unaposoma kitabu cha Waebrania 11 unapata picha gani? Unajua maana ya imani? Imani ni Kumtegemea Mungu. Sasa unaposhindwa kumtegemea Mungu na unakalia kuangalia mazingira yanayokuzunguka, basi kweli wewe huna tofauti na asiyeamini au ni mchanga kiroho.

c) Wanashindwa kusimamia viapo vyao. Raisi Magufuli aliendelea kusema “Viongozi wa dini wameanza kuyumba na kumsahau Mungu ambaye waliapa, ndio kiapo chao; Biblia…” Wachungaji wanapoingia rasmi katika utumishi kwa kawaida hupewa viapo (ukiacha utiriri wa watu wanaojiita wachungaji). Katika viapo hivyo, ni lazima ukubali kwamba utashika neno la Mungu sawasawa na imani ya Kikristo. Kuna viapo vingi kwa kutegema na kanisa, lakini kiapo ni kile kile kwamba unakubali kusimama na neno la Mungu. Hivyo basi, raisi anaona watumishi wa Mungu wengi wamekuwa wasaliti kwa viapo vyao. Tena anasema “wameanza kuyumba” kwa maana ya kwamba walikuwa kwenye msimamo mzuri sasa wameanza kutoka kwenye huo msimamo.

d) Ubinadamu umewatawala. Rais Magufuli anasema kwamba viongozi hawa “wameanza kuisahau na kuiweka pembeni na kuweka ubinadamu mbele;” Hapa ndipo penye ile hoja ambayo nimekwisha kusema kwamba viongozi wa siku hizi hawana imani. Wanaogopa kufa, huo ndio ubinadamu wenyewe. Hapa hamaanishi kwamba mtumishi wa Mungu uende kichwa kichwa bila tahadhari-hapana! Kiongozi wa dini anatarajiwa awe mfano wa kuigwa kwa kutoa elimu ya kujikinga huku yeye akionesha kwa vitendo; hata hivyo siku hizi ubinadamu umewatawala viongozi hawa. Labda kuna mtu aliniambia kwamba wachungaji wengi wana vitambi, na hivyo wanaogopa kwamba korona ikiwapata inafuatilia sana wenye mafuta..wanaogopa wataenda mbinguni mapema.

e) Kipimo cha Mtumishi wa Mungu. Kipimo chochote cha mtumishi wa Mungu siyo Yule anayeweza kunena kwa lugha, au yule ambaye ana maneno mengi- ni yule ambaye anastahimili magumu! Ni yule anayemtegemea Mungu na kumwamini kabisa. Rais Magufuli anasema “huu ndio wakati wa kuwapima imani viongozi tulio nao, hata viongozi wa dini.”
Hitimisho: Uchambuzi huu umeegemea kwenye hotuba ya Rais Magufuli kwenye kile kipengele cha viongozi wa dini. Ikumbukwe kwamba hapa sijasema kwamba viongozi wote wa dini wako kama raisi alivyosema, lakini raisi mwenyewe kasema kwamba siyo wote “baadhi yao.” Hivyo basi niungane tena na raisi kwamba;

a) Tuendelee kujikinga na ugonjwa huu kwa sababu ni kweli upo na unaua watu

b) Tusiache kumwomba Mungu na kumtegemea yeye na tukumbuke kwamba yapo magonjwa mengi yamewahi kutokea duniani.

SHIDA YA KUTUMIA VIFUNGU HIVYO

a) Vifungu hivyo vikichukuliwa juu kwa juu vinaweza kuhatarisha usalama wa taifa letu. Kuna watumishi ambao wao wakishasoma mstari mmoja tu, anatoka nao anaimba.
b) Watumishi wengi siku hizi hawana elimu ya kutafsiri maandiko (Hermeneutics) na hivyo wakichukua moja kwa moja na kujifananisha na Yona au Daniel changamoto lazima iwepo.

TUJIFUNZE KUPITIA HISTORIA

c) Katika Historia kanisa milipuko ya magonjwa ilipojitokeza kila kundi la kidini lilikuwa na msimamo wake. Hebu tuangalie ugonjwa uliolipuka miaka ya 1347-1352 ulioitwa “black death”(kabla hata ya matengenezo ya kanisa)

Mtazamo wa Kikristo:

· Wakristo wengi waliamini Pigo hilo lilikuwa adhabu kutoka kwa Mungu kwa dhambi za wanadamu lakini pia lilisababishwa na "hewa mbaya", uchawi na uaguzi, ulozi na maovu ya watu walizidi duniani.
· Wakristo wengi waliweza kuyaacha maeneo ambayo yameambukizwa na kwenda kwenye maeneo ambayo yalikuwa bado hayajaambukizwa. Hivyo walijikuta wamekuwa wakimbizi. Ikumbukwe takribani watu milioni 50 duniani kote walikufa
· Kwa kuwa pigo hilo lilikuwa ni la kuambukizwa, basi wakristo walipaswa kujikinga kwa kufanya toba ya kweli mbele za Mungu kwa makosa waliyofanya.

Mtazamo wa Waislamu

· Pigo hilo lilikuwa zawadi ya rehema kutoka kwa Mungu ambayo ilifanya mauaji kwa waaminifu ambao roho zao zilisafirishwa peponi. Kwa maana ya kwamba vifo hivyo yalikuwa na majaliwa ya Mwenyezi Mungu
· Waislamu hawakupaswa kukimbia pigo hilo na kwenda sehemu nyingine kama walivyofanya Wakristo; kama pigo likija, basi wakati huo ni kusimama katika imani na Alah ili uende peponi
· Hapakuwa na haja ya kutubu, bali kumshukuru Alah kwa kuvuna roho zake kwa mapenzi yake

Je, unaonaje mitazamo hiyo?

Je, unaweza kuilinganisha na mitazamo ya leo kuhusu korona?

Mch. Daniel John Seni
CONTACT WhatApp ONLY: +8210-2159-1980

[1]
IMG_20200504_014423_973.jpg
 
hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
38,353
2,000
Mungu uwepo wake huwa unanifikirisha sana....maaana kuna wakati naona kabisa kuwa anashindwa nguvu na viumbe ambavyo yeye mwenyewe ameviumba... huyu mungu huyu mnaye muhubiri anapaswa kuchunguzwa upya.... huwenda ikawa mmempachika sifa ambazo hana..... 😄 😄 by the way mkuu umenichekesha sana.. yaani hats waumini wanaoamini kuwa ukifa unaenda peponi nao wanaogopa kifo dhidi ya corona ....so hiyo sindio ticket ya kwenda peponi na kuoa mabikira 72 inakuwaje wanaikimbia hiyo opportunity tena !?.... hizi dini hizi ili uziamini yakupasa uwe hauko timamu
 
Dseni

Member
Aug 13, 2012
33
125
Mungu bado ni Mungu na bado Mkuu vile vile, shida ni wanadamu kushindwa kufahamu utendaji kazi wake tu
Mungu uwepo wake huwa unanifikirisha sana....maaana kuna wakati naona kabisa kuwa anashindwa nguvu na viumbe ambavyo yeye mwenyewe ameviumba... huyu mungu huyu mnaye muhubiri anapaswa kuchunguzwa upya.... huwenda ikawa mmempachika sifa ambazo hana..... by the way mkuu umenichekesha sana.. yaani hats waumini wanaoamini kuwa ukifa unaenda peponi nao wanaogopa kifo dhidi ya corona ....so hiyo sindio ticket ya kwenda peponi na kuoa mabikira 72 inakuwaje wanaikimbia hiyo opportunity tena !?.... hizi dini hizi ili uziamini yakupasa uwe hauko timamu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
RANCO TZ

Member
Aug 26, 2014
23
45
Mungu uwepo wake huwa unanifikirisha sana....maaana kuna wakati naona kabisa kuwa anashindwa nguvu na viumbe ambavyo yeye mwenyewe ameviumba... huyu mungu huyu mnaye muhubiri anapaswa kuchunguzwa upya.... huwenda ikawa mmempachika sifa ambazo hana..... 😄 😄 by the way mkuu umenichekesha sana.. yaani hats waumini wanaoamini kuwa ukifa unaenda peponi nao wanaogopa kifo dhidi ya corona ....so hiyo sindio ticket ya kwenda peponi na kuoa mabikira 72 inakuwaje wanaikimbia hiyo opportunity tena !?.... hizi dini hizi ili uziamini yakupasa uwe hauko timamu
ACHA UVIVU WA KUSOMA NA KUTAFAKARI
MTOA MADA AMEZUNGUMZIA TATIZO LA KUCHUA MSTAR MMOJAA NA KUANZA KUIMBA NAO BILA HATA KUUELEWA,UNAITWA UVIVU WA KUSOMA NA UVIVU WA KUTAFAKARI
MTOA MADA KAGUSIA PEPO KWA IMAN YA WAISLAM NA MAFUNDISHO YA DINI YA KIISLAM HAYAFUNDISHI KUA LENGO LA KUKAA HAPO PALIPO NA MLIPUKO NI KUTAKA UFE ILI UENDE PEPON, BALI LENGO KUBWA NI KUEPUKA KUENDEZA MAGONJWA KTK SEHEM ZINGINE.. SIO UNAJUA UNAUKIMWI UNAENDA KUTEMBEA NA WAKE ZA WATU NA KUMKIMBIA MKEO.
NA UNAPOKAA ENEO HILO HAIMANISHI UACHE KUCHUKUA TAHADHAR YA KUEPUKA MARADH, LKN UNAPOACHA KWENDA NJEE NA UKACHUKUA TAHADHAR NA BADO UKAFA NDIO IMAN INASEMA UMETEKELEZA JUKUMU LAKO NA AMRI NJEMA YA MUNGU WAKO< HIVYO UNASTAHIKI PEPO.

ACHA UVIVU WA KUSOMA.. SOMA UTAELEWA .....
 
RANCO TZ

Member
Aug 26, 2014
23
45
UCHAMBUZI WA KAULI YA RAIS MAGUFULI KUHUSU VIONGOZI WA DINI KATIKA MUKTADHA WA COVID-19

Na: Mchungaji Daniel Seni

Tarehe 3/5/2020 raisi John Joseph Pombe katika hafla ya kuapishwa kwa waziri mpya wa Katiba na Sheria, Dr. Mwigulu Nchemba, aliyeteuliwa kutokana na kufariki kwa aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo ndugu Agostino Mahiga. Katika hotuba yake, pamoja na mambo mengine mengi, aliwanyooshea kidole baadhi ya viongozi wa dini kwa ajili ya misimamo yao kuhusu korona na ibada kanisani au misikitini.
Baada ya kusikiliza kwa makini hotuba yake, hasa kipengele cha viongozi wa dini, nimeona nichambue ili tujiridhishe uhalali wa malalamiko yake.
Ningependa ninukuu maneno haya;

“…lakini pia tuendelee kumwomba Mungu wetu, Mungu yupo. Wapo hata viongozi wa dini wengine wamemsahau Mungu ambaye kila siku wamekuwa wakituhubiria; wanashika vitabu wanafahamu juu wa akina Daniel walivyokaa kwenye matumbo ya samaki (ni Daniel?) Daniel ni kwenye moto, wapo wengine walitupwa kwenye moto, wapo wengine walitupwa kwenye simba, simba hakuwala, kwa sababu walimtegemea Mungu. Leo kuna viongozi wa dini wameanza kuyumba na kumsahau Mungu ambaye waliapa, ndio kiapo chao; Biblia au Korani, wameanza kuisahau na kuiweka pembeni na kuweka ubinadamu mbele; acheni kuomba, tunajiokoa, acheni sijui nini nini, ni mambo ya ajabu, lakini ndiyo hivyo, katika kipindi hiki cha mpito tutayasikia mengi, na huu ndio wakati wa kuwapima imani viongozi tulio nao, hata viongozi wa dini. Ukizuia waumini wako wasiende kanisani, ukazuia watu wasiende msikitini, na unaweza kukuta msikiti huo hukuujenga wewe, umejengwa na hao waumini, hili nalo ni suala la ajabu la kujiuliza, si uwaachie hao waumini wafungulie waende wenye nia yao waende wakamwombe Mungu., hata kama wewe hutaenda kuhubiri pale! Ndiyo haya tutayaona, hizi ni changamoto, na mimi nawaomba Watanzania tuendelee kumwomba Mungu, na Mungu atatusaidia kutupitisha katika changamoto hizi…”mwisho wa kunukuu.

Ukiangalia katika nukuu hiyo hapo juu, raisi anaongelea dini mbili; Ukristo na Uislamu, hata hivyo mifano ya Kibiblia aliyoitoa ni kutoka katika Ukristo; labda pengine kwa sababu ni Mkristo. Katika Makala haya, nitajadili kwa upande wa viongozi wa dini wa Kikristo kwa sababu sina uzoefu wa kutosha katika upande wa pili wa dini. Napenda kujikita katika hoja ambazo raisi ameziweka kwa ajili ya kuthibitisha lawama zake kwa viongozi wa dini, na je lawama hizo zikoje kwenye muktadha wa Kitheologia.

Mifano kutoka kwenye Biblia; Daniel 6:16-22 (kuna kosa lilifanyika kidogo katika kutamka, raisi alichanganya habari ya Daniel na Yona). Ninachotaka kukichambua mahali hapa ni; je raisi alikuwa sahihi kutumia maandiko hayo katika muktadha wa korona?

Kwa mujibu wa Mch. Edwin Mihigo katika video aliyoiweka kwenye akaunti yake ya facebook tarehe 2/5/2020 siku moja kabla ya hotuba ya raisi yeye anasema hivi “swala la Daniel ni tofauti kabisa na mazingira ya korona, yeye ukiangalia alizuiliwa asiabudu; na alipoamua kumwabudu Mungu, basi ikabidi ahukumiwe. Tukio hili limelenga kumthibitisha Mungu wa Israel.”[1] Ameeleza mambo mengi lakini mwisho akasema tu kwamba; suala la korona si kwa ajili ya wasioamini tu, bali ni kwa watu wote. Suala muhimu ni kujilinda. Unaweza kubonyeza link hiyo kusikiliza mpaka mwisho.

Katika matukio kama haya, Wakristo katika vipindi vyote vya Biblia (Agano la Kale na Agano Jipya) wamekuwa na mitizamo tofauti tofauti. Kila mmoja amekuwa akisisitiza msimamo ambao anaamini ni sahihi kabisa. Tukiachilia masuala ya akina Daniel, Yona na wengineo; tunaweza kuona pia mateso ya kanisa la kwanza.

Je ni sahihi kutumia vifungu hivyo katika muktadha huu wa Korona? Nitaeleza kwa kuzingatia pande zote mbili; upande wa kwanza ni sawa (kwa kuzingatia muktadha wa msemaji) na upande wa pili si sawa (kwa kuzingatia muktadha wa Kitheologia)

UHALALI WA KUTUMIA VIFUNGU HIVYO KATIKA KUPAMBANA NA KORONA

a) Kwa kuzingatia muktadha wa msemaji (ambaye ni raisi Magufuli) lengo lake hawa siyo kuwaambia watu waache kujikinga na ugonjwa wa korona; kusudi lake ni kule kuonyesha kwamba Mungu anaweza kuwatoa hata katika janga hili kubwa la Corona. Na ndiyo maana anaanza kwa kusema “lakini pia tuendelee kumwomba Mungu wetu,” na anamalizia kwa kusema “tuendelee kumwomba Mungu, na Mungu atatusaidia kutupitisha katika changamoto hizi.”

Kwa muktadha huohuo, unaweza kugundua kwamba rais Magufuli ametumia habari za Daniel na Yona si kwa kuwazuia watu kujikinga au kutozingatia taratibu za kiafya, bali ni kwamba Mungu yupo, na kwamba anaweza kutusaidia.

b) Kwa kawaida tunapokuwa kwenye maombi mara nyingi huwa tunarejelea vifungu mbalimbali vya Biblia. Hivyo basi si kosa kwa raisi Magufuli kurejelea vifungu hivyo; hata kama alikosea kosea lakini dhana inabaki palepale kwamba lengo lake ilikuwa ni kuonyesha watu “Umuhimu wa kumtegemea Mungu.” Swali la kujiuliza labda je vifungu hivi hatuvitumii kwenye kuombea watu wanapokuwa kwenye shida? Je vifungu vya Zaburi 118:17 kwamba “sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana” huwa mnavirejelea kwenye maombi mkimaanisha kwamba kweli hamtakufa? Ni dhahiri kwamba huwa tunarejelea vifungu mbalimbali vya Biblia tunapokuwa kwenye maombi au kwenye changamoto zozote katika maisha yetu.

c) Kuhusu kwamba ugonjwa huu unaua watu wote; nakubali 100% kabisa lakini lazima kuna kitu cha kusema. Ukisikia watu walifunga siku 40 kavu wakafa kwa njaa; haimaanishi kwamba usifunge. Kama ukisikia kwamba kuna taifa fulani wamekufa watu laki 1 leo haimaanishi kwamba hata nchini kwako wanaenda kufa hao laki 1. Wakati wa magonjwa, watu wa aina zote wanakufa; uwe mpagani, mkristo, mwislamu, nk…lakini hii haimaanishi kwamba mtu aache imani yake kwa Mungu. Hii inamaanisha kwamba wakati unamtegemea Mungu ni lazima pia unahitaji kuzingatia kanuni hizo. Mkristo unapaswa kuomba mpaka usikie sauti “Neema yangu yakutosha” (kama Paulo alivyosikia)…bila kusahau kwamba unahitaji kutumia mbinu/dawa zilizopo kwa wakati huo. Paulo alimwambia Timotheo “atumie mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lake;” hapa Paulo alikuwa ana uwezo wa kumwambia afunge, lakini kwa sababu ya shida ya tumbo, Timotheo alikuwa hawezi kufunga-hata hivyo bado Paulo aliomba kwa ajili ya Timotheo.

d) Katika Maandishi ya Martin Luther, yeye alichukulia “mlipuko wa magonjwa” kama jaribu ambalo linajaribu kuthibitisha imani yetu na upendo kwa Mungu: akasisitiza “Wakristo lazima kwanza wachague kutimiza mapenzi ya mwili au ya Mungu"imani yetu ili tuweze kuona na kuona jinsi tunapaswa kutenda kwa Mungu. Luther aliwaruhusu Wakristo kufanya maamuzi ya kibinafsi kuhusu aidha kukimbia au kukabili kifo.
Hebu kabla hatujaendelea upande wa pili wa makala haya, ningependa kujadili kidogo hoja ya raisi magufuli kwa watumishi wa Mungu hawa. Nimejaribu kuchambua dhamira tano (5) muhimu katika kama kiini cha malalamiko na tuangalie uhalali wake.

a) Viongozi kushindwa kusimamia yale wanayohubiri. Raisi Magufuli anasema “Wapo hata viongozi wa dini wengine wamemsahau Mungu ambaye kila siku wamekuwa wakituhubiria.” Ukiangalia tamko hilo ni dhahiri kwamba wapo watumishi ambao wameshindwa kusimama katika yale wanayosimama nayo. Makanisa ya mitume na Manabii kwa sasa wako kimya kabisa. Lakini kila mara wamekuwa wakihubiri kwamba wao wanaponya HIV, Kansa, na magonjwa mengine sugu..kwa sasa raisi anaona kama wameyumba vile. Nina hakika Tanzania wako watumishi wa Mungu wanaoomba sana usiku na mchana kwa ajili ya korona iondoke; lakini raisi anasema kuna baadhi kumbe wao wanatuambia tutapona—kumbe wanajua hatutapona. Hawaamini kile wanachosema.

b) Wanashindwa Kuamini Yaliyofanyika katika Historia; Raisi Magufuli anasema “Wanashika vitabu wanafahamu juu wa akina Daniel… walimtegemea Mungu.” Hapa kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba matukio yote yaliyofanyika katika historia yanalenga kutufundisha sisi tusimame katika imani. Changamoto ya watumishi wa Mungu wa leo ambao raisi anawasema ni kwamba “wanaogopa kufa.” Hawana uhakika na wokovu wao! Hawana “security.” Hivi unaposoma kitabu cha Waebrania 11 unapata picha gani? Unajua maana ya imani? Imani ni Kumtegemea Mungu. Sasa unaposhindwa kumtegemea Mungu na unakalia kuangalia mazingira yanayokuzunguka, basi kweli wewe huna tofauti na asiyeamini au ni mchanga kiroho.

c) Wanashindwa kusimamia viapo vyao. Raisi Magufuli aliendelea kusema “Viongozi wa dini wameanza kuyumba na kumsahau Mungu ambaye waliapa, ndio kiapo chao; Biblia…” Wachungaji wanapoingia rasmi katika utumishi kwa kawaida hupewa viapo (ukiacha utiriri wa watu wanaojiita wachungaji). Katika viapo hivyo, ni lazima ukubali kwamba utashika neno la Mungu sawasawa na imani ya Kikristo. Kuna viapo vingi kwa kutegema na kanisa, lakini kiapo ni kile kile kwamba unakubali kusimama na neno la Mungu. Hivyo basi, raisi anaona watumishi wa Mungu wengi wamekuwa wasaliti kwa viapo vyao. Tena anasema “wameanza kuyumba” kwa maana ya kwamba walikuwa kwenye msimamo mzuri sasa wameanza kutoka kwenye huo msimamo.

d) Ubinadamu umewatawala. Rais Magufuli anasema kwamba viongozi hawa “wameanza kuisahau na kuiweka pembeni na kuweka ubinadamu mbele;” Hapa ndipo penye ile hoja ambayo nimekwisha kusema kwamba viongozi wa siku hizi hawana imani. Wanaogopa kufa, huo ndio ubinadamu wenyewe. Hapa hamaanishi kwamba mtumishi wa Mungu uende kichwa kichwa bila tahadhari-hapana! Kiongozi wa dini anatarajiwa awe mfano wa kuigwa kwa kutoa elimu ya kujikinga huku yeye akionesha kwa vitendo; hata hivyo siku hizi ubinadamu umewatawala viongozi hawa. Labda kuna mtu aliniambia kwamba wachungaji wengi wana vitambi, na hivyo wanaogopa kwamba korona ikiwapata inafuatilia sana wenye mafuta..wanaogopa wataenda mbinguni mapema.

e) Kipimo cha Mtumishi wa Mungu. Kipimo chochote cha mtumishi wa Mungu siyo Yule anayeweza kunena kwa lugha, au yule ambaye ana maneno mengi- ni yule ambaye anastahimili magumu! Ni yule anayemtegemea Mungu na kumwamini kabisa. Rais Magufuli anasema “huu ndio wakati wa kuwapima imani viongozi tulio nao, hata viongozi wa dini.”
Hitimisho: Uchambuzi huu umeegemea kwenye hotuba ya Rais Magufuli kwenye kile kipengele cha viongozi wa dini. Ikumbukwe kwamba hapa sijasema kwamba viongozi wote wa dini wako kama raisi alivyosema, lakini raisi mwenyewe kasema kwamba siyo wote “baadhi yao.” Hivyo basi niungane tena na raisi kwamba;

a) Tuendelee kujikinga na ugonjwa huu kwa sababu ni kweli upo na unaua watu

b) Tusiache kumwomba Mungu na kumtegemea yeye na tukumbuke kwamba yapo magonjwa mengi yamewahi kutokea duniani.

SHIDA YA KUTUMIA VIFUNGU HIVYO

a) Vifungu hivyo vikichukuliwa juu kwa juu vinaweza kuhatarisha usalama wa taifa letu. Kuna watumishi ambao wao wakishasoma mstari mmoja tu, anatoka nao anaimba.
b) Watumishi wengi siku hizi hawana elimu ya kutafsiri maandiko (Hermeneutics) na hivyo wakichukua moja kwa moja na kujifananisha na Yona au Daniel changamoto lazima iwepo.

TUJIFUNZE KUPITIA HISTORIA

c) Katika Historia kanisa milipuko ya magonjwa ilipojitokeza kila kundi la kidini lilikuwa na msimamo wake. Hebu tuangalie ugonjwa uliolipuka miaka ya 1347-1352 ulioitwa “black death”(kabla hata ya matengenezo ya kanisa)

Mtazamo wa Kikristo:

· Wakristo wengi waliamini Pigo hilo lilikuwa adhabu kutoka kwa Mungu kwa dhambi za wanadamu lakini pia lilisababishwa na "hewa mbaya", uchawi na uaguzi, ulozi na maovu ya watu walizidi duniani.
· Wakristo wengi waliweza kuyaacha maeneo ambayo yameambukizwa na kwenda kwenye maeneo ambayo yalikuwa bado hayajaambukizwa. Hivyo walijikuta wamekuwa wakimbizi. Ikumbukwe takribani watu milioni 50 duniani kote walikufa
· Kwa kuwa pigo hilo lilikuwa ni la kuambukizwa, basi wakristo walipaswa kujikinga kwa kufanya toba ya kweli mbele za Mungu kwa makosa waliyofanya.

Mtazamo wa Waislamu

· Pigo hilo lilikuwa zawadi ya rehema kutoka kwa Mungu ambayo ilifanya mauaji kwa waaminifu ambao roho zao zilisafirishwa peponi. Kwa maana ya kwamba vifo hivyo yalikuwa na majaliwa ya Mwenyezi Mungu
· Waislamu hawakupaswa kukimbia pigo hilo na kwenda sehemu nyingine kama walivyofanya Wakristo; kama pigo likija, basi wakati huo ni kusimama katika imani na Alah ili uende peponi
· Hapakuwa na haja ya kutubu, bali kumshukuru Alah kwa kuvuna roho zake kwa mapenzi yake

Je, unaonaje mitazamo hiyo?

Je, unaweza kuilinganisha na mitazamo ya leo kuhusu korona?

Mch. Daniel John Seni
CONTACT WhatApp ONLY: +8210-2159-1980

Kwasababu sijui utash wa Rais ktk iman ya Mungu wake, Lkn Nafasi ya Mungu Muumba inabaki palepale Muongozaj na Mmiliki wa yote.
Huweza tegemea Mungu pekee kupambana na Corona. Mungu amekupa Nyenzo na vitendea kazi moja wapo akili,na mali, Hivo Lazima uvitumie ktk njia ambazo yeye Muumba anaridhia (kwa wanaomfuata Mungu) kupambana na hali hiyo, Kama vitabu vyake vimetoa solution ya moja kwa moja Apply. Mfano Mwenyezi Mungu amesema Miti inazuwia Mafuriko na kuleta hali ya hewa safi, Wewe ukikata miti na kuharibu mazingira UKIONA MVUA nyingiikasababisha maafa usimlaumu Mungu jichunguze wewe mwenyewe.
Ktk janga hili mkumbe Mungu lkn sio uanche kufanya majukumu yako na kutegemea Mungu atakuja kuzuwia Corona isiingie nyumban kwako hali yakua Njia za kuzuwia maambukizi huzifuati.
 
Gwappo Mwakatobe

Senior Member
Nov 22, 2019
142
250
Umefanya uchambuzi mzuri mno na kujenga hoja kwa umakini mkubwa. Hongera sana!

Sent from my TECNO LC6 using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom