Kwa nini kingunge aligoma kumushukuru jk baada ya kuhutubia wazee dsm!!???????????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini kingunge aligoma kumushukuru jk baada ya kuhutubia wazee dsm!!????????????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Nov 20, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Baada Ya Hotuba kwa Wazee wa CCM Mwenyekiti wa Wazee Brigedia Mbita alimwita Kingunge Kuja kuwashukuru Hotuba ya Jk Lakini ghafla Mwenyekiti huyo akasikika akisema Kingunge amekataa na kuendelea na Mambo mengine.

  Wadau wanasema huenda aliogopa kwa kuwa Wazee wa Kigoda cha Mwalimu wakiwemo Jaji Warioba, na Mh Salimu walitaka hekima itumike ili kuondoa machafuko nchini!!!

  Angalia tukio hilo katika picha hizi!!
  :juggle:
   
 2. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #2
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  kazi ipo
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mods msitoe hii maana hamkawii
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Kingunge ashindwa kumshukuru Kikwete
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 20 November 2011 09:12 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] Leon Bahati
  KADA Mkongwe wa CCM, Kingune Ngombale Mwiru alishindwa kuzungumza "neno la shukurani" baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia taifa kupitia mkutano wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam.

  Mzee Kingune ambaye alikaa upande wa kushoto wa Rais Jakaya Kikwete wakati akihutubia Taifa juzi, alionekana kutokuwa tayari kusema neno hilo la shukrani licha ya Kaimu Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Dar es Salaam, Brigedia Jenerali Hashim Mbita, kumsihi afanye hivyo.

  Mbita aliyekuwa upande wa kulia wa Rais Kikwete , alisikika mara kadhaa kwenye kipaza sauti akimkaribisha Mwasisi huyo wa Chama , bila ya mafanikio .

  Hata hivyo haikufahamika sababu za Kingunge kushindwa kutii ombi hilo ingawa alionyesha ishara ya kutokuwa tayari kufanya hivyo licha ya Mbita kuendelea kumsihi bila mafanikio.

  Tukio hilo lilitokea wakati Brigedia Mbita alipokuwa akizingatia taratibu za kiitifaki za kutoa neno la shukrani baada ya Rais Kikwete kutoa hotuba.

  Baada ya kitendo hicho kulionekana kuwepo kwa miguno kutoka kwa baadhi ya wazee waliohudhuria mkutano huo wakishindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea kwenye meza kuu.

  Hatimaye baada ya jitihada za ushawishi kushindikana Mbita aliamua kutoa neno la shukrani kwa Rais Kikwete akibainisha kuwa .hotuba yake imejaa nasaha nzuri na muhimu kwa Watanzania wote.

  Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alizungumzia mambo ambayo katika kipindi cha karibuni yamekuwa yanawagusa Watanzania wengi, yakiwemo yanayohusu matatizo ya kiuchumi na uundwaji wa katiba mpya.

  Kuhusu uchumi, Kikwete aliwataka Watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho Tanzania na mataifa mengine duniani yanakabiliwa na athari za kiuchumi.

  Miongoni mwa athari hizo alizozitaja ni pamoja na kasi ya mfumuko wa bei ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya nchi, kushuka kwa thamani ya shilingi, kupanda kwa bei ya mafuta na kuadimika kwa sukari inayozalishwa nchini kutokana na kuuzwa kimagendo kwa nchi jirani.

  Alisema serikali yake iko mbioni kukabiliana na baadhi ya matatizo na moja wapo ni kuagiza sukari kutoka nje.

  Lakini tatizo kama vile kupanda kwa bei ya mafuta na kushuka thamani ya sarafu huku dola ya kimarekani ikipaa, alisema ni tatizo kwa nchi nyingi duniani.


  Kuhusu Katiba, Kikwete alipinga hoja zilizokuwa zikitolewa na Chadema pamoja na wanaharakati wa mabadiliko ya katiba.

  Mojawapo ya hoja hizo, alisema wanapotosha kuwa suala la muungano limekatazwa kujadiliwa.

  Ukweli alisema wanapinga kwenye mchakato wa kuandaa rasimu kujadili juu ya kuvunja muungano lakini wanaruhusu maoni ya namna ya kuuboresha.

  Aliwahakikishia Watanzania kuwa katika mchakato wa kuandaa katiba hiyo, watakuwa huru katika kutoa maoni yao.

  Lakini akaonyesha wasiwasi wake kuwa kuna makundi ya watu yanayoweza kuhamasisha watu juu ya mambo yenye maslahi kwao hivyo akaonya:

  "Ninataka wananchi wawe huru. Mtu asilazimishwe la kusema."

  Akijua wazi kuwa Chadema wamekuwa wakishinikiza mambo mbalimbali kwa maandamano kwa hoja ya kutumia nguvu ya umma, Kikwete akaonya:

  "Jambo hili halihitaji maandamano… Vurugu hazina faida bali kuwaongezea machungu Watanzania. Hivyo naomba wawe na busara. Tuchague njia ya faraja. Tusichague njia ya machungu."
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Nov 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hali ya uchumi ya sasa ni global trend lakini hapa kwetu tatizo ni yeye
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,817
  Likes Received: 36,921
  Trophy Points: 280
  Kingunge aliona atajichoresha kutoa shukrani kwa hotuba ile ya JK.
   
 7. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #7
  Nov 20, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]SAKATA LA KATIBA Dk Salim: CCM kaeni na Chadema
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 17 November 2011 21:36 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  ANONYA BILA MARIDHIANO NCHI ITAELEKEA KUBAYA, KITINE ADAI SERIKALI 'INATUPELEKAPEKA'
  Boniface Meena
  MJADALA wa Muswada wa Katiba Mpya umechukua sura mpya baada ya viongozi waandamizi wa Serikali wakiwamo wastaafu, kutaka upatikane mwafaka wa kitaifa kuhusu suala hilo vinginevyo taifa litaelekea kubaya.Onyo la viongozi hao akiwamo Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa , Dk Hassy Kitine, linakuja ikiwa ni siku chache baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kutaka mwafaka huo wa kitaifa.

  Jana, viongozi wakichangia maoni yao katika mdahalo uliondaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF), kuhusu nafasi na umuhimu wa katiba katika maisha ya Watanzania, kwa sehemu kubwa walipaza sauti kutaka mwafaka huo ili kunusuru taifa.

  Kauli ya Dk Salim
  Dk Salim ambaye ni mwenyekiti wa MNH, alisema ni muhimu kuwe na makubaliano na maafikiano katika suala la Katiba Mpya kwa CCM na Chadema.

  Alisema, "Chama tawala na chama kikuu cha upinzani vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo".
  Dk Salim alisema kwamba malumbano si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe yakasababisha nchi ikafika pabaya.
  "Ninachoomba chama tawala na Chadema wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si jambo zuri kwa taifa,"alisema Dk Salim ambaye ana uzoefu na utatuzi wa migogoro ya kimataifa.
  Alisema zoezi la Katiba ni zito na linatakiwa kufanyika kwa busara na kuwahusisha Watanzania wote.
  "Kwa hali ya kisiasa hivi sasa ni lazima mjadala uwe wa nia njema lengo ni kuendeleza makubaliano na si kuhitilafiana. Tujenge na kuimarisha undugu na mishikamano wetu na kuonyesha uzalendo na uongozi madhubuti wa taifa letu,"alisema Dk Salim.
  Kitine aionya Serikali
  Kwa upande wake, Dk Kitine, alisema ni vizuri Serikali ikasoma alama za nyakati kutokana na hoja iliyoko bungeni kwa kuangalia suala hilo la katiba.

  Dk Kitine alisema Serikali haitakiwi kuruhusu Muswada huo wa Marekebisho ya Katiba ukasomwa kwa mara ya pili, kwani tayari upinzani bungeni umekwishapinga.

  "Serikali iutoe na kusoma upya, nchi haiko tayari kuona Serikali inavyotupeleka. Sasa ndiyo maana kuna matatizo kila sehemu,"alisema Dk Kitine.

  Jaji Samatta
  Kwa upande wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta alisema kuna baadhi ya wanasiasa hawaelewi maana ya katiba na kupotosha kuwa ni mapatano kati ya wananchi na viongozi."Katiba ikifutwa viongozi hakuna, hivyo Katiba ni moyo wa taifa,"alisema.

  Jaji Samatta alisema kutunga Katiba ni kazi nzito na haiwezekani kila kitu anachokihitaji au kitu kinachohitajiwa na kundi fulani, kiwepo katika Katiba."Katiba ni makubaliano, lakini muda uliowekewa suala hili ni mchache,"alisema.

  Alisema Katiba ya mwaka 1977 imefanya kazi nzuri, lakini ina matatizo mengi ndani yake, moja ikiwa ni dhana ya mfumo wa chama kimoja.

  "Mfano Spika wa Bunge kuwa sehemu ya Halmashauri Kuu ya chama tawala, hapa atasababisha mgongano wa maslahi kwa kutetea chama chake,"alitoa kasoro hiyo.

  Alisema kutokana na hali hiyo, Katiba Mpya ni lazima iwe na chachu ya upanuzi wa demokrasia na uboreshaji wa utawala wa sheria."Iwe ya mfumo wa vyama vingi na kuondokana na mfumo wa chama kimoja na iwe, inayoongozwa na wananchi,"alisema Jaji Samatta.

  Dk Slaa atabiri Katiba mbovu
  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema mchakato wa Katiba uikiwa mbovu Katiba yenyewe itakuwa mbovu.

  "Wenzetu kule Dodoma wanapotosha kwamba kilichopo ni mchakato wanafikiri mchakato ni kitu kidogo, katiba ndiyo mzazi wa kila kitu hivyo kwa hali ilivyo katiba hii haiwezi kuwa ni ya wananchi badala yake Rais anajitengenezea Katiba yake,"alisema Dk Slaa.

  Dk Bilal
  Awali, akifungua mdahalo huo baada ya wachangiaji hao kutoa maoni yao, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal alisema nchi haiwezi kuwa na katiba nzuri ambayo itapatikana kwa kuliacha taifa likiwa vipande.

  Alisema, ni muhimu kuhakikisha kunakuwepo majadiliano kuhusu kupata Katiba kukiwa na dhamira ya pekee ya kuhakikisha umoja, mshikamano na muunganmo vinabakia na kuimarika zaidi.

  Dk Bilal alisema Serikali imejipanga vizuri na itahakikisha zoezi hilo linafanyika vema bila bughudha yoyote na kila mwananchi anapata haki ya kutoa maoni yake, kwa uwazi bila vizingiti vyovyote.

  "Tunataka kubakia taifa ambalo linasimamia uhuru, haki na misingi ya kutafuta usawa kwa kila mwananchi. Tunataka kubakia taifa linaloheshimu utu, kuenzi ubinadamu na kuthamini ujenzi wa taifa lisilofungamana na matabaka,"alisema Dk Bilal.

  Makamu wa Rais alisema kazi ya kuandika Katiba mpya ni lazima ifanyike kwa umakini, kwa uangalifu na kwa weledi mkubwa kwa kuwa taifa linapaswa kubaki linalokuwa kisiasa, kijamii na kiuchumi.
  Tangu kuanza kwa mjadala kuhusu muswada huo, wabunge wote wa Chadema akiungwa mkono na baadhi ya wabunge wa NCCR- Mageuizi hawakuwahi kushiriki kutokana na kile wanachodai kwamba kuingizwa kwake bungeni kulikiuka kanuni za Bunge na Sheria za nchi.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,076
  Likes Received: 7,566
  Trophy Points: 280
  Umenena vyema mkubwa, maana JF siku hizi inatulazimisha ku-think shallow Mods hawataki tena maandiko yenye muelekeo wa kuipinga serikali. Niliwahi tuma andiko lilihusiana na TISS wakali close mapema. siku nyingine niliandika kwa staili ya kuuliza andiko moja kuhusiana na Aboud Jumbe hilo ndiyo halikuonekana kabisa hapa. Nimeamua kutumia muda wangu mwingi kuchangia Post za watu na muda mwingine kwenye Chit-Chat. Kuliko kulazimishwa kufikiri au kuandiko nje ya upeo na uelewa wangu. Au kuandika vitu sare sare kama zombies.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wanabembeleza gazeti lao lisajiliwe labda ndo maana wanamtumikia kafiri
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Hahahahaha, kama hapa ni yeye na huko kwingine ni yeye pia, au sio?
   
 11. M-pesa

  M-pesa JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama uliifuatilia vyema hotuba ya JK, kuna upuuzi mwingi kaongea na hasa pale alipoamua kuanika wazi imani ya mzee kingunge kwamba mpaka leo hayupo kwenye dini yeyote. Ukizingatia ya kwamba huyu jamaa ndio charger ya kikwete kwenye masuala ya nguvu za giza.
   
 12. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nakubaliana na wewe kwa hoja zako lakini ukumbuke hata sisi tulioko huku mashenzini hatujauona huo muswada na wala hatujui umeandikwa nini maana hao watu wamegeuza tanzania ni dodoma, dar na zanzibar poleni sana
   
Loading...