Ni kwa nini CCM wanahofu ya JK kuzomewa bungeni ijumaa?

Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,438
3,458
Nimewasikia wajumbe mbalimbali wa CCM akiwemo pia Mwenyekiti Samwel Sita wakijitahidi kutoa tahadhari zenye sura za vitisho kwa wajumbe wanaowahisi watamzomea Mh Rais JK atakapohutubia bunge siku ya ijumaa. Sita kadai kuna kamera zaidi ya 13 ndani ya bunge kwa ajili ya kuwanasa wajumbe watakaofanya fujo na kwamba wataangalia uwezekano wa kuwatoa kwenye public media.

Baada ya hoja zilizoshiba za Mh Warioba, inaonekana CCM wanajua JK hatakuwa na hoja yeyote ya maana kumpinga Warioba na tume yake, na kwa sababu hiyo wameshikwa na hofu kuwa akijifanya kukosoa tume tu anaweza kuambulia aibu ya kuzomewa. sasa wanajipanga kuwatisha wajumbe wasiexpress hisia zao zidi ya mipasho badala ya kujibu hoja zitakapoanza dhidi ya tume ya warioba.

Tunamsihi Mh Rais kama ijumaa atapenda kumjibu Warioba na tume yake, basi ajikite kwenye hoja alizozitoa Mh Jaji Warioba.
 
kazi ya jk ijumaa ni kufungua bunge la katiba tu , wala hana hata mamlaka ya kumjibu warioba , akithubutu tu amekwisha ! Tena siyo kuzomewa bali hata kupishana na wajumbe mlangoni .
 
Akija na hoja za maCCM azomewe tu tumechoka na hotuba za Mipasho ambazo hazijengi zinazidi kuturudisha nyuma.
 
Kikwete ninayemjua mimi hatabiriki.yule ------ ana maneno matamu ya kuzima moto,wala hana presha saa hzi.chamsingi Tuombe Mungu wetu mwema atujalie katiba itakayokidhi matakwa yetu watanzania
 
Bado ninajiuliza kuwa nini kingeanza kati ya Mkuu wa Nchi kuzindua Bunge rasmi na Mwenyekiti wa tume kuwasilisha rasimu ya Katiba? Kwa kuwa sasa inakuwa kama Raisi anakuja kuchangia hoja badala ya kuzindua Bunge. Nini nia hasa ya kufanya mageuzi hayo? Waliopanga hivyo wanamdhalilisha mkuu wa nchi bila kutambua. Nadhani wala Rais hatagusia hotuba ya Waryoba kama ambavyo angeanza yeye angefanya!
 
hoja kuu ya kila mchangia hoja ni kuhusu tabia ya raisi wetu wa jumhuri kupenda sana mipasho hahahahha nimependa sana hiyo taswira ya mzee wa mipasho anapenda kuwapasha upinzani sana
 
Kama atajifanyakujadili hoja za walioba hata wananchi tumzomee tu. Kazi yake ni kuzindua bunge ili rasimu ijadiliwe na si vinginenyo.
 
Jk akijichanganya na kuanza kuwa sehemu ya wajumbe tu kwa kumjibu warioba badala ya kuzindua bunge maalumu la katiba azomewe tu! Kazi ya mijadala awaachie wajumbe wenyewe!
 
akiongea kitu ambacho watanzania hawataki kukisikia lazima atazomewa tu.
 
Nimewasikia wajumbe mbalimbali wa CCM akiwemo pia Mwenyekiti Samwel Sita wakijitahidi kutoa tahadhari zenye sura za vitisho kwa wajumbe wanaowahisi watamzomea Mh Rais JK atakapohutubia bunge siku ya ijumaa. Sita kadai kuna kamera zaidi ya 13 ndani ya bunge kwa ajili ya kuwanasa wajumbe watakaofanya fujo na kwamba wataangalia uwezekano wa kuwatoa kwenye public media.
Baada ya hoja zilizoshiba za Mh Warioba, inaonekana CCM wanajua JK hatakuwa na hoja yeyote ya maana kumpinga Warioba na tume yake, na kwa sababu hiyo wameshikwa na hofu kuwa akijifanya kukosoa tume tu anaweza kuambulia aibu ya kuzomewa. sasa wanajipanga kuwatisha wajumbe wasiexpress hisia zao zidi ya mipasho badala ya kujibu hoja zitakapoanza dhidi ya tume ya warioba.
Tunamsihi Mh Rais kama ijumaa atapenda kumjibu Warioba na tume yake, basi ajikite kwenye hoja alizozitoa Mh Jaji Warioba.

Pyuu! Kama bata kanya,
Gongo ya asbuhi usipokunywa supu unaweza ukajikuta unaota huku unatembea.
 
Nimewasikia wajumbe mbalimbali wa CCM akiwemo pia Mwenyekiti Samwel Sita wakijitahidi kutoa tahadhari zenye sura za vitisho kwa wajumbe wanaowahisi watamzomea Mh Rais JK atakapohutubia bunge siku ya ijumaa. Sita kadai kuna kamera zaidi ya 13 ndani ya bunge kwa ajili ya kuwanasa wajumbe watakaofanya fujo na kwamba wataangalia uwezekano wa kuwatoa kwenye public media.
Baada ya hoja zilizoshiba za Mh Warioba, inaonekana CCM wanajua JK hatakuwa na hoja yeyote ya maana kumpinga Warioba na tume yake, na kwa sababu hiyo wameshikwa na hofu kuwa akijifanya kukosoa tume tu anaweza kuambulia aibu ya kuzomewa. sasa wanajipanga kuwatisha wajumbe wasiexpress hisia zao zidi ya mipasho badala ya kujibu hoja zitakapoanza dhidi ya tume ya warioba.
Tunamsihi Mh Rais kama ijumaa atapenda kumjibu Warioba na tume yake, basi ajikite kwenye hoja alizozitoa Mh Jaji Warioba.
TBC sasa hivi asubuhi wako na Lipumba na Mzanzibar na wanazungumzia kuhusu serikali 2 au 3 kwa nini wanashindwa kusema vipi tuwe na serikali ya zanzibar na tusiwe na serikali ya tanganyika? kuna ulazima gani wa kuwa na serikali ya Zanzibar wakati tuna serikali ya muungano? hilo ndilo tatizo kubwa, na kama hilo sio suala la msingi kupita yote kwa nini ccm wameliwekea msimamo?mbona hawajawekea msimamo hayo masuala mengine wanayosema ni ya msingi kama Ardhi, elimu,na mshikamano. kiukweli la msingi kupita zote ni hili la haina ya muundo wa serikali
 
Sijui kwanini tanzania masiki,nawajua wauza madawa ya kulevya,nawajua majangili wapo,ni kiherehere chao teh teh kwanini usizomewe
 
Back
Top Bottom