Kwa nini hata ndoa ikivunjwa na mwanamume lawama zinaenda kwa mwanamke? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini hata ndoa ikivunjwa na mwanamume lawama zinaenda kwa mwanamke?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nazjaz, Aug 22, 2011.

 1. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Jamani hebu pata picha, nimetolewa kijijini nimeletwa mjini kuolewa na mtu ambaye hata sijawahi kumuona na simfahamu kabisa. Mtu huyu ni mlevi kupindukia, haachi matumizi nyumbani, tunadaiwa madeni chungu nzima. Pia nasikia eti huwa nasikia akilewa hujidondosha makusudi ili watoto wabaya wammpasulie mayai.

  Jamani kwenye ndoa kama hii najaribu kujinasua lakini naitwa eti mi ni mpumbavu na ninaivunja nyumba yangu kwa mikono yangu mwenyewe. Huyu mwanaume hashauriki, na ukijaribu kumwelekeza naishia kupigwa na matusi juu. Kwanini yeye ndio asiitwe mpumbavu na aliyeivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe?

  Naomba tujadili.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Aug 22, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote utaolewaje na mtu ambaye hujawahi kumuona na usiyemfahamu? Sasa kwa nini usiitwe mpumbavu kama ulikubali kufanya hivyo? Fikiria.
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Hivi we ndio yule ambrosi tuliye msoma kwenye kitabu cha hawala ya fedha tulipokuwa wadogo?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Aug 22, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Yule ni Ambrosi na mimi ni Kevin Ambrose.
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Hapo kuna utata kidogo
  Wewe unakubalije kuuziwa mbuzi kweney gunia mtu humjui wala hujawahi kumuona unakubali tuu kupelekwa kama mbuzi machinjioni bana
  Haiji wewe nafikiri ndo unatakiwa uitwe hilo jina
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mbona na wewe ushachaguliwa mke?!Usitukane wakunga uzazi ungalipo!!
   
 7. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Hebu jua kula na kipofu hujui?
  Jifunze kula na kipofu kamwe nyumba hutoiona chungu na wala haitovunjika.
   
 8. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Vitu vingi vinavyopelekea mtu aolewe na mtu asiye mjua. Nazjaz suo wa kwanza, hali ngumu ya maisha jumlisha uelewa mdogo wa wazazi na binti mwenyewe ndivyo vinavyo pelekea hali kama hii kutokea
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Aug 22, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Lizzy Ambrose?
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu sawa nakubaliana na wewe kuwa kuna mambo yanachangia kwa binti kuolewa na mtu ambaye hamjui
  Ila mkuu ukishakutana na hali kama hiyo kinachotakiwa ni wewe kucope na mazingira husika na mume uliyechaguliwa
  Sidhani kama kuanzia asubuhi anakuwa emelewa
  Amvizie asubuhi akiwa mzima na aeleze matatizo yake
   
 11. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Ndoa ni makubaliano ya Watu Wawili waliopendana na ambao wako tayari kuishi kwa Shida na Raha.
  Kosa lako, hakukuwa na makubaliano na huyo mtu wako, na wala ulikuwa humjui, ulikurupushwa kijijini ukaja mjini ukapewa hilo jumba bovu ambalo linakuangukia sasa. kama ni kuishi kwa Shida basi hizo zimezidi.
  Cha msingi hapo nakushauri UVUE GAMBA tu, kwa sababu yatakupata makubwa zaidi ya hayo, anaweza kukutia kilema kwa vipigo. Pole
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Enhee!!Una mpango wa kumkataa?!Au unamshauri yeye akukatae?!
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  mkuu umesema acope sasa kwa hiyo itabidi nae aanze kula kitungi ili waende sawa..

  kuhusu mambo kama haya yakitokea inabidi uwe mvumilivu na mwenye subiri na isitoshe chumba inawezekana mshua kala kodi kwa hiyo taraka haina nafasi..
   
 14. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Yaani mpaka leo kuna wabongo wanaolewa bila kujua nani anayemuoa? Au kwa sababu uliambiwa unakwenda kuishi mjini? Ha ha ha, MOD tunaomba uturuhusu tumchape vibao kwa kudhalilisha wanawake wenzake
   
 15. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Mkuu sikumaanisha acope na yeye aaanze kupiga tungi ila acope kwa kuyakubali mazingira alimojikuta maana yameshakuwa hayo hana ujanja na ameshakubali kuwa huyo ndie mume wake na mahari ishapokelewa
   
 16. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,999
  Trophy Points: 280
  Jifunze kufunga, kusali kuomba na kushukuru, ni Mungu tu atakaye mbadili huyo mumeo.
   
 17. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  sasa inaonekana hata kwao hawamuelewi ndio maana iko hivyo..

  ushauri mwingine aanze kupiga mazoezi ya kareti ili jamaa akianzisha songombingo anatulizwa kiulaini..
   
 18. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hapo Inabidi urudi kwa yule aliyekutoa kijijini kwenu kukupeleka kwa huyo mwanaume umwambie mzigo aliokutwisha umekushinda.
   
 19. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ndio zigo lako hilo huna budi kulibeba
   
 20. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,313
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  raha ya mlevi kubali mabaya yake yote yawe yako! umekubali kuja mjini kutka kijijini kwenu kumjia mlevi,, pata raha yake na ukifurukuta tu WE MBAAAAAAAAAAYA!!!
   
Loading...