Kwa nini Gari za Nissan Qashqai siyo maarufu sana Tanzania?

dfreym

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
342
87
Kiukweli katika fuatilia yangu ya magari. Gari za Nissan Maarufu ni Morano, Dualis, X- trail, Nissan Patrol, Juke, na manufacture wengine kama Subaru, Toyota na kadhalika.

Gari za Nissan Qashqai ni nzuri sana kimuomekano na ulaji wa mafuta. Na nimefuatilia hata engine zake nyingi ni 1000+ mpaka 2000.
Kitu ambacho kinafanana na gari nyingi zilizo maarufu. Lakini hizi gari siyo maarufu kabisa.

Sasa nilikuwa najichanga changa ninunue gari hii (Qashqai) ambapo nimejaribu kufuatilia bei zake ni around 25M Mpaka 35M.

Ila ninaingiwa na hofu na mashaka kuhusu mambo makuu yafuatayo.
1. Kwa nini gari hizi siyo nyingi Tz?
2. yaweza kuwa spare zake ni ghali sana kiasi ikizingua utajikuta unapaki.
3. Au siyo imara kama zingine?
4. Spare zake haziingiliani na dualis? (Japo niliambiwa qashqai ni upgrade ya dualis)
5. Au ni vimeo huenda details ninazoziona siyo sahihi?

MSAADA TAFADHALI.


images%20(83).jpg
 
Ni gari ile ile moja wala hakuna upgrade, inasemekana ilianza kuuzwa kwa jina la quashqai jina hili lilsumbua sana baadhi ya nchi kulitumia walishndwa kulitaja mfano Australia. Ndipo wakaipa jina dualis.

Kwa iyo kuna baadhi ya nchi unauzwa kwa jina la hilo na zingne kma Australia nadhan na huk kwetu inauzwa km dualis ila ni gari moja tu mkuu.
 
Ni gari ile ile moja wala hakuna upgrade, inasemekana ilianza kuuzwa kwa jina la quashqai jina hili lilsumbua sana baadhi ya nchi kulitumia walishndwa kulitaja mfano Australia. Ndipo wakaipa jina dualis. Kwa iyo kuna baadhi ya nchi unauzwa kwa jina la hilo na zingne kma Australia nadhan na huk kwetu inauzwa km dualis ila ni gari moja tu mkuu.
Mbona zina pishana muonekano na dualis, kama taa,baadi ya folds za bodi sunroof(baadhi zinazo na baadhi hazina). Pia nimejaribu kufuatilia dualis zinaonekana za miaka ya nyuma. Qashqai zinaonekana ni za miaka ya 2015 na zaidi..
 
Mbona zina pishana muonekano na dualis, kama taa,baadi ya folds za bodi sunroof(baadhi zinazo na baadhi hazina). Pia nimejaribu kufuatilia dualis zinaonekana za miaka ya nyuma. Qashqai zinaonekana ni za miaka ya 2015 na zaidi..
Mkuu zipo kuanzia 2008 mpaka za 2020

Tofauti na dualis ipo inategemea na toleo.

Matoleo ya 2008/9/10 ni kama dualis ila kuanzia 2011 ni tofauti sana.
 
CVT transmission kwa mazingira ya kiafrika sio rafiki, google utapata elimu by the way kwa Bongo Nissan Hapana period.

Kauli yako sio sahihi. CVT africa zinafanya kazi kama kawaida. Gari nyingi tu zinatumia CVT, mojawapo ni Subaru, toyota tav 4, vanguard, honda etc. Labda useme Nissan kama kuna kitu walikosea kwenye baadhi ya model zao.
Na bado sidhani kama tatizo la kila nissan ni gearbox.
 
Jamani ni hiviiii, Qashqai sio Brand kwa Bongo, Msiwe na vichwa vigumu nina examples tatu za jamaa zangu wanalia hadi leo wanaomba tuwatafutie magari huku tunakobeba boksi, Ukishupaza shingo nunua utakuja kunishukuru baadaye, narudia TOYOTA for Tanzania.
Bongo gari yoyote unaendesha mm nina ISUZU Bighorn toka 2009 nabadilisha oil Tu na miguu from time to time! Nina mpango wa kuchukua BMW X5 acheni kututisha. Pesa tuzipate kwa taabu na kutumia muanze tena kuchonga?
 
CVT transmission kwa mazingira ya kiafrika sio rafiki, google utapata elimu by the way kwa Bongo Nissan Hapana period.

CVT transmission kila mahali now. Unless uamue kununua sport car nyingi ndio hazina CVT.

Ila gari nyingi za kuanzia 2014 kuja huku juu hata toyota wanatia CVT.

Japo baadhi ya CVT za Nissan zina shida ila siyo zote. Na hiyo Dualis/Quashqai siyo one of them.
 
tunaogopa jina mkuu,limekaa kichina sana,kutamka tu shida...
Sio jina. Tumia akili kubwa kuwaza zaidi alichokisema mdau.

Anamaanisha kuwa
1. Kanunua hilo gari.
2. Anataka tumjuze kuhusu spare na ulaji wa mafuta.
3. Anaturingishia sisi na vibaby walker zetu jamii ya brevis,crown athlete, probox, alphard n.k
4. Anatuhamasisha tununue gari za kiume kiumeni.

Kijana waza nje ya box tafadhali.

Sogea hapo Bambalaga uone vibwenga vya ubishoo.
 
Sio jina. Tumia akili kubwa kuwaza zaidi alichokisema mdau.

Anamaanisha kuwa
1. Kanunua hilo gari...
Wa bongo tumekalilishwa magari hamna cha utaalamu wowote eti Toyota ndo gari peke, unakuta mtu ana kipato cha 10m kwa mwezi ila anaedesha ist eti spare bei chini, limbukeni wa magari, mimi hapa naendesha chovelete huu ni mwaka wa tatu sijaenda kununua kipuri chochote zaidi ya service ya kawaida hata unywaji wake wa mafuta sioni tofauti yake na vi baby walker vyenu
 
Back
Top Bottom