Makonda, William Malecela wadaiwa kupanga njama za kumchafua aliyewashitaki kwa utapeli wa gari

Kosinde

Member
Jun 7, 2018
49
60
Makonda, Lemutuzi wapanga njama kumchafua PCK Kisutu leo

WAKATI kesi ya madai namba 234/2022, iliyofunguliwa na Mfanyabiashara Patrick Christopher Kamwelewe ‘PCK’ dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mwanamitandao William Malecela ‘Le Mutuz’, ikitarajiwa kuanza kusikilizwa leo tarehe 13 Oktoba 2022, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imebainika kwamba watuhumiwa hao wawili wamepanga kundi la kwenda kumchafua mfanyabiashara huyo nje ya viunga vya mahakama hiyo.

Inaelezwa kuwa Makonda na Lemutuz wamepanga kundi hilo ili kumchafua PCK na kuuaminisha umma kuwa kesi hiyo haina mashiko.

Kesi hiyo inasikilizwa leo mchana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Richard Kabate ambapo mfanyabiashata huyo anawataka Makonda na Malecela wamlipe fidia ya kiasi cha Sh. 247.2 milioni;

Katika kesi hiyo, Kamwelwe anaiomba mahakama imuamuru Makonda na mwenzake, kumlipa kiasi hicho cha fedha kama fidia anayodai kuwa, imetokana na hatua ya wadaiwa hao kumdhulumu gari lake jeusi aina ya Toyota Rand Rover/Range Rover Range Sport, yenye namba 20153.

Katika mchanganuo wa fedha hizo, Sh. 247,243,750, ambazo ni sawa na dola za Marekani 106,250, Kamwelwe anamtaka Makonda na mwenzake, walimpe dola 11,250, kama gharama ya kodi ya kuliingiza gari hilo. Dola 50,000, fidia ya kutwaa gari, pamoja na dola 45,000, ambayo ni thamani ya gari.

Makonda anadaiwa kuwa ameendelea kuitumia gari hiyo hata baada ya kuondolewa madarakani licha ya kwamba si mali yake halali.

SOMENI HII HABARI RAIA MWEMA WALIVYOANDIKA NAMNA GARI ILIVYOKWAPULIWA

Kamwelwe ambaye awali alikuwa mfanyabiashara wa magari, msanii wa Bongofleva na promota wa muziki, alisema mwaka 2017 alifuatwa na Staa wa mitandaoni ambaye pia ni mtoto wa Waziri Mkuu mstaafu, Samwel Malecela, William Malecela maarufu kwa jina la Lemutuz na kumueleza kuwa Makonda anaomba amuazime gari aina ya Range Rover.

Alisema Lemutuz alimfuata katika Yard yake ya magari iliyokuwepo katika eneo la Magomeni Mikumi jijini Dar es salaam.

“Sikuwa na urafiki wowote na Makonda wala Lemutuz hivyo nilipata wasiwasi licha ya kufahamu kwamba kweli Lemutuz ni rafiki wa karibu wa Makonda. Lakini kama unavyofahamu Lemutuz ni mtu wa sifa kwa hiyo akatoa simu na kumpigia video call Makonda ambaye baada ya kusalimiana akanihakikishia kweli amemtuma Lemutuzi.

“Nikampatia gari, lakini bado wakawa wanaendelea kuja kuchukua hela kwangu, kwa kuwa kipindi kile hali ilikuwa tete na mimi ninakwa nawapo chochote nilichonacho,” alisema.

Alisema kilichomshtua ni pale alipoanza kuona gari yake imebandikwa kibao kwenye namba za usajili jina la RC DSM.

“Hapo niliona sasa niache unyonge, nikamtafute Lemutuz ili nirejeshwe gari yangu, lakini kumbe ndio kama niliuchokoza moto, na wala sikufanikiwa, nikawa napigwa chenga leo kesho na kupewa vitisho vya hapa na pale,” alisema.

Alisema cha ajabu katika kipindi Makonda anataja orodha ya watuhumiwa wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya, nay eye alitajwa kwa kuwa mmoja wa watuhumiwa wanaomiliki mali kirahamu ndipo akafunguliwa kesi katika mahakama hiyo ya Kisutu.

Juni 2017, vyombo vya habari viliripoti kesi hiyo yenye namba CC 247/2017 iliyokuwa inaendeshwa katika Mahakama ya Kisutu chini ya Hakimu Susan Kihawa.

Kwa mujibu wa Musa Ngonyani mwanasheria aliyekuwa akimuwakilisha Kamwelwe wakati huo, alisema mteja wake huyo alishtakiwa kwa kumiliki mali haramu.

Aidha, Kamwelwe alilieleza Raia Mwema kwamba wakili aliyekuwa akiendelea na kesi hiyo katika siku za karibuni, alifahamika kwa jina la Rashdu, alipoteza maisha wiki iliyopita, hivyo anaendelea na harakati za kumtafuta wakili mwingine.

Mali za Kamwelwe zilizoshikiliwa wakati huo hadi sasa amedai magari matatu, Toyota Prado (shilingi milioni 60), Nissan Murano (shilingi milioni 45) na Toyota V-Mark (shilingi milioni 32) na nyumba ya ghorofa ya kifahari iliyopo maeneo ya Kigamboni (Dar) jirani kabisa na Ufukwe wa Bahari ya Hindi huku akaunti zake zote za benki zikifungwa kutokana na kuwa kiasi kikubwa cha fedha hadi kesi yake itakapomalizika kwa sababu inasemekana mali hizo siyo za halali.
 
Kwahiyo huyo PCK akichafuliwa mitandaoni ndio Mhakama itamuhukumu yeye kisa kachafuliwa mitandaoni? Mahakama huhitaji vivid evidence ili kutoa hukumu na sio kwa kusoma kwenye mitandao ya kijamii.
 
Kutokana na mtiririko wa maelezo hapo, inavoonekana kuna vitu vinafichwa haswaa kumhusu huyo PCK...nini chanzo cha hizo pesa zake hadi kumiliki hio Yard ya magari??? Je, sio utakatishaji wa pesa huo uliotokana na pesa haramu za ngada??? Maana kumpa Makonda gari kirahisi hivyo just kwa kuongea nae video call tu na Le mutuz pembeni ndio kweli unaweza kuachia Range Rover kiujinga ujinga tu??? Kuna makubaliano ya hao watu nyuma ya pazia, ila sasa kwa vile kesi ipo mahakamani ukweli utajulikana tu....kwa ujasusi wangu nilionao mdogo tu ni kua hio gari kuna makubaliano mengine kati ya PCK na Makonda yapo chini ya kapeti ili kuuziba uharamia wa wakati ule. Time will tell.
 
Ishu hapa ni kudhulumiwa gari. Jinsi alivyopata pesa nyingi hilo ni shauri jingine....
 
Pck kama ni huyu mrundi basi hata yeye hana usafi kivile
Na tatizo la makonda kuna baadhi ya watu wachafu aliambatana nao
Hii itamsumbua sana
Ngoja tusubirie maamuzi ya mahakama...

Ova
 
Hii nchi kila mtu ni mjanja janja na mwizi kwa tafsiri ya haraka haraka sheria zetu ni mbovu au vyombo vyetu vya mahakama kumejaa rushwaa...
 
Kutokana na mtiririko wa maelezo hapo, inavoonekana kuna vitu vinafichwa haswaa kumhusu huyo PCK...nini chanzo cha hizo pesa zake hadi kumiliki hio Yard ya magari??? Je, sio utakatishaji wa pesa huo uliotokana na pesa haramu za ngada??? Maana kumpa Makonda gari kirahisi hivyo just kwa kuongea nae video call tu na Le mutuz pembeni ndio kweli unaweza kuachia Range Rover kiujinga ujinga tu??? Kuna makubaliano ya hao watu nyuma ya pazia, ila sasa kwa vile kesi ipo mahakamani ukweli utajulikana tu....kwa ujasusi wangu nilionao mdogo tu ni kua hio gari kuna makubaliano mengine kati ya PCK na Makonda yapo chini ya kapeti ili kuuziba uharamia wa wakati ule. Time will tell.
Pia haihalalishi makonda kulichukua.
Hoja unayojenga unalenga kuwa jamaa ni mhalifu so alitoa gari asishtakiwe au kuchukuliwa hatua?

Ndivyo sheria inavyotaka?

Huoni mhalifu zaidi ni huyu Makonda?

Kwanini akubali kuhongwa?
 
Ishu hapa ni kudhulumiwa gari. Jinsi alivyopata pesa nyingi hilo ni shauri jingine....
Issue ni kudhulumiwa sawa, Lakini je kwa akili yako kweli mtu unaweza toa gari kirahisi rahisi hivyo tena gari yenyewe Range kwa video call tu ya Le Mutuz?????? Kwamba alimpa Makonda ili iweje?? Ndio maana nasema muda utaeleza hayo yote yatajulikana.
 
Hilo tutalifungulia shauri baadaye baada ya upelelezi kukamilika. Hivi sasa ngoja tu deal na udhulumaji...
 
Issue ni kudhulumiwa sawa, Lakini je kwa akili yako kweli mtu unaweza toa gari kirahisi rahisi hivyo tena gari yenyewe Range kwa video call tu ya Le Mutuz?????? Kwamba alimpa Makonda ili iweje?? Ndio maana nasema muda utaeleza hayo yote yatajulikana.
Amefungua kesi ya kudhulumiwa gari,namna gani amedhulumiwa hiyo haina maana,wangapi wanaazimana magari mjini hapa?? Wangapi wanaendesha magari siyo yao?? Kwahiyo namna ya kupeana siyo issue,issue ni kutokurudisha baada ya kuazimwa au kupewa,arudishe gari
 
Huyo jamaa akifwatiliwa ataoneka kwa nini alitoa hilo gari na kukaa kimya ameona jamaa hana Rungu anataka gari lake pana kitu kipo hapo jamaa ajazurumiwa gari ila alihonga ili mazambi yake yasifumuke ndio maana kaona hiki kipindi adai gari lake...hawezi kukaa kimya miaka yote hiyo kama kweli palikua na biashara harali hapo ...na Makonda hawezi kuongea kitu maana ataulizwa ukiruhusu kazi haramu ifanyike kwa kuhongwa gari...
 
Huyo mshamba wa kirundi hana uwezo kuwa na hilo gari wala biashara ya uhakika.
Katumwa tu kuna watu behind hiyo yard.
Ni bwege mmoja hivi alikua anazurula huko dubai na waarabu.
Kazi yake haieleweki.
Ndio kaibuka tu na hili la kudai range..
Le mutuz kasema hamjui hata kumuona.
 
Wote wale wale

Huwezi ukawa unapiga vita mambo fulani,alafu bado kuna watu fulani wanaojihusisha na mambo fulani
We unaambatana nao?

Ova
 
Back
Top Bottom