Kwa nini chuo kikuu muhimbili kinatulazimisha wanafunzi kuunda katiba wanayoitaka wao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini chuo kikuu muhimbili kinatulazimisha wanafunzi kuunda katiba wanayoitaka wao?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by drgeorge, Jun 11, 2011.

 1. d

  drgeorge Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa mujibu wa sheria chama cha wanafunzi kinaweza kufutwa kwa kutumia Government Notice No. 178 of 12 June, 2009? Na inakuwaje juu ya University Act of 2005 section 42 (1)?  Naombeni msaada hapa, maana Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Muhimbili amefuta Chama cha Wanafunzi (MUHASSO) kwa barua yake ya Tarehe 10 Jun, 2009 kwa Rais wa serikali ya wanafunzi yenye kumbukumbu Na. MU/074/1042/206 yenye kichwa cha habari BANNING OG MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES STUDENTS' ORGANISATION (MUHASSO)

  Kisa wanafunzi hatukubaliani na mwongozo wenye upungufu na ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa wanafunzi ikiwemo:-

  1. Mwongozo unatulazimisha kukubaliana (to comply with...) na sera yoyote ya serikali, wizara au chuo
  2. Kila mwanafunzi atakayetaka kugombea nafasi ya uongozi ni lazima awe na GPA ya 3.5 au itakayopangwa na chuo
  3. Mwongozo huo inampa mamlaka makubwa Mlezi wa wanafunzi (Dean of Students) kuwa mkuu katika shughuli za serikali ya wanafunzi (Administrative head)
  4. Mwongozo huo ulipa Baraza la Chuoa au bodi ya chuo kukifuta chama cha wanafunzi ikiwa chama hicho hakitafuata masharti yalioyowekwa na wizara, chuo au baraza/bodi hiyo
  5. Pia ina vipengele ambavyo kwa uelewa wangu ni vipengele dhaifu (Poor provisions) ambavyo vinatoa mwanya mkubwa wa ukandamizaji kwa wanafunzi, kwa mfano; inasema ili mwanafunzi aweze kuogombea uongozi ni lazima awea na high self esteem. sasa mimi nashindwa kuelewa hiyo high self esteem ni kiasi gani, inapimwaje na ni nani anayepima?


  View attachment CHUO KIKUU MUHIMBILI UBABE MTUPU.docx
   
Loading...