Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Bunge linaweza kumwondoa madarakani Rais

2. Bunge.

Katiba No. 46A

(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais

(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama

(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bungelilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
mkuu mchakato huu ni mrefu sana ,wakati wanafanya huu mchakato mpaka wapige kula ,yeye ambaye anauwezo wa kulivunja bunge bila kuwasiliana atakuwa anawasubili wamtoe,
 
Katiba No. 116
Mada nzuri sana kiongozi hii, endelea kushusha nondo maana wananchi wengi wanakuwa wavivu sana wa kusoma Katiba. Naomba nikusahihishe kidogo hapo uliposema "Katiba No. 116" sema "Ibara ya 116".
 
mkuu mchakato huu ni mrefu sana ,wakati wanafanya huu mchakato mpaka wapige kula ,yeye ambaye anauwezo wa kulivunja bunge bila kuwasiliana atakuwa anawasubili wamtoe,
Mkuu wala usiseme eti muda ni mrefu. Hapo nafikri hata mahakama huwa zinatakiwa kusimama imara kama Malawi walivyomfanyia yule mama aliyetaka kubaka demokrasia. Haiwezekani alivunje bunge wakati mchakato wa kumjadili ukiendelea. Wabuge wetu wanatakiwa kuwa imara sana na kusahau tofauti zao za kiitikadi watusaidie kutuondolea huyu mgonjwa hapo alipo, na hapa chama lazima kituombe radhi kwamba kilichemka kutuletea mgonjwa wa akili! Yote haya ni shauri ya Kikwete, hakika mimi nitamsamehe lakini sitamsahau!! Nafasi ilikuwa ya Mzee Lowassa hii kwa kila namna (iwe alivyokuwa CCM au alivyoenda UKAWA). Tumedhurumu haki ya mtu ngoja cha moto tukione!!
 
Kifungu 90 (d) cha katiba kinachompa madaraka rais kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu pale ambapo ataona bunge linapinga kile ambacho serikali yake inakifanya.
Mkuu jishughulishe kujisomea...hizi situations ni mbili tofauti kabisa.
 
Kujua sheria si kujua kifungu kimoja moja. Unabidi ujuwe ibara na vifungu vyote. Kwa mfano ibara ya 90(d) ya Katiba inampa madaraka rais kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu upya pale rais atakapoona halikubaliani na kile serikali yake inakifanya. Kwa maneno mepesi ni kuwa pale bunge likianza kufanya fyoko fyoko ya kupinga sera zake anazotekeleza na ambazo yeye kwake ni za msingi, basi atavunja bunge hilo na kuitisha uchaguzi mkuu ambapo wananchi ndiyo watakaoamua nani arudi bungeni na nani awe rais wao.

Kwa hiyo mchakato wa bunge ulioko kwenye ibara ya 46A wa kutaka kumu impeach rais ukianza utamaanisha ibara hii ya 90(d) ifanye kazi maana utadhihilisha wazi kuwa sasa bunge linazipinga sera za msingi za serikali iliyo madarakani. Hivyo huo mchakato wa ibara ya 46A hautafika mwisho bali mwisho wake utakuwa ni ule wa ibara 90(d).

Kwa hiyo msitake kuwadanganya wabunge eti kuna njia rahisi tu ya kumuondoa rais madarakani. Never on earth. Hata huko kwenye nchi zilizoendelea si rahisi kumuondoa rais aliyeshinda uchaguzi mkuu. La sivyo ingekuwa vurugu tupu maana kila mtu anapenda kuwa rais. Tuheshimu kile ambacho wananchi walichagua. Baada ya uchaguzi tufanye kazi. Na bahati nzuri uchaguzi ni kila baada ya miaka 5 tu na sasa imebaki mitatu tu na kaushee wananchi wataamua tena.
Hivi hujasoma kuwa pindi bunge linapounda kamati ya uchunguzi tayari RAIS HATAKUWA KAZINI?jishughulishe kidogo kuelewa mada.
 
Mkuu Ngosha hajashindwa kazi. Sema wengi hatukubaliani na maamuzi yake. Lakini hilo halimfanyi kuonekana kwamba kashindwa kazi. Ukweli mchungu huo.
 
2. Bunge.

Katiba No. 46A

(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais

(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba, au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.

(3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama

(a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya
Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;
(b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge waiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

(4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani

(a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
(b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
(c) Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa
uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.

(5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashataka yaliyotolewa dhidi yake.

(6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

(8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

(9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

(10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bungelilipopitisha azimio hilo.

(11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
Aiseee, hivi Wabunge wa Tanzania wanajua power waliyonayo?
 
Mbona huo utaratibu tayari umewekwa wazi kwenye Katiba? Kwanza matendo tu na kauli anazozitoa zinaonesha anayo matatizo makubwa ambayo mtu asiye na maradhi kama hayo katu hawezi kuzitoa. Muangalie hata uso wakati anaongea, je ni picha gani unatoka nayo?
Kumbe katiba imeeleza hayo !!!!yaan mpaka vipimo vyakuangalia kwa macho tu!!Aisee!!!
 
sio kweli...akivunja uchaguzi wa wabunge unafanyika...aipopata majority hawezi kuunda serikali . ..na atapigiwa vote of no confidence
Aisee!!!Atapigiwa vote of no confidence akiwa kama nani?Si lazima uonekane nawe umechangia.
 
Hivi hujasoma kuwa pindi bunge linapounda kamati ya uchunguzi tayari RAIS HATAKUWA KAZINI?jishughulishe kidogo kuelewa mada.
Soma ibara 90(d) inasema nini. Kujua katiba unapaswa kuzijua ibara zote, siyo ibara moja tu, maana zinakwenda pamoja. Unaweza kukuta ibara moja inatoa haki fulani lakini haki hiyo inanyang'anyanywa na ibara fulani. Hayo ndiyo mambo ya sheria. Usiisome katiba kama novel fulani ya penguin, utapotea.
 
Hivi hujasoma kuwa pindi bunge linapounda kamati ya uchunguzi tayari RAIS HATAKUWA KAZINI?jishughulishe kidogo kuelewa mada.
Huo mchakato hautafikia hatua hiyo maana rais kwa mamlaka aliyonayo chini kifungu 90(d) atakuwa ameshalivunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu upya.
 
Nawaza tu kwa MFANO hiki kinachosemwa ya KUWA bunge LIMEJIPANGA kumwondoa RAIS madarakani ni cha kweli na ikatokea imefanikiwa.....ni yapi yatakuwa ni madhara kupitia CCM...
Hopefully tutafanya UCHAGUZI mkuu....sasa hofu yangu juu ya hili LA KUMWONDOA RAIS NI NDOTO na halitokujafanikiwa KAMWE ni hii...
Ni nani hasa ni MBADALA WA MAGUFULI ndani ya CCM???.....na ambae hatauzika vizuri huku nje bila tatzo???Kidogo Unaweza sema ni MEMBE but huyu MEMBE ana makando kando yake pia NA PIA si MEMBE tu wapo pia HAZINA KUBWA YA VIJANA kama MWIGULU..JANUARY na wengine but tukumbuke mpaka sasa HUYU RAIS aliyepo MADARAKANI tayari ana watiifu wake MWISHO wa siku ITATOKEA MIFARAKANO YA SISI WENYE KWA WENYEWE NA kuwafaidisha WAPINZANI....kupitia HILI HAKUNA MBUNGE WA CCM anaeweza kuruhusu huu UPUUZI hata kama ana mchukia JPM....sisi NDANI ya CCM tuna kauli ifuatayo 'CHAMA KWANZA MTU BAADAE"....
Na je kupitia upinzani ni nani hasa NI MSAFI zaidi ya MAGUFULI???....ni jibu ni hakuna hata kidogo maana so far UPINZANI unategemea wafuatao NI LOWASSA na LISSU...but kuna wafia chama kamwe hawamkubali MZEE hata kidogo na MZEE hayupo tayari kukaa pembeni kwenye SUALA LA URAIS....mwisho wa siku ni CHADEMA vipande vipande......
Ndio maana tunasema IMPEACHMENT KWA JPM NI NDOTO........sasa ebu mwacheni RAIS wetu atutumikie sisi tusiokuwa MAJIZI,,MAGAIDI,..WAVIVU..MAFISADI...TUSIOPENDA MAISHA YA MTEREMKO atutumikie tutamuhukumu 2020......
 
Back
Top Bottom