Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, Bunge linaweza kumwondoa madarakani Rais

Watu wanataka maendeleo yanayoonekana na unafuu wa ugumu wa maisha sio kiburi,jeuri,ubishi,kuvimba kichwa,kujiona kila taaluma unaiweza. Hata akitolewa wale wateuzi wake wa kanda ya ziwa wote waondolewa.
 
Nawaza tu kwa MFANO hiki kinachosemwa ya KUWA bunge LIMEJIPANGA kumwondoa RAIS madarakani ni cha kweli na ikatokea imefanikiwa.....ni yapi yatakuwa ni madhara kupitia CCM...
Hopefully tutafanya UCHAGUZI mkuu....sasa hofu yangu juu ya hili LA KUMWONDOA RAIS NI NDOTO na halitokujafanikiwa KAMWE ni hii...
Ni nani hasa ni MBADALA WA MAGUFULI ndani ya CCM???.....na ambae hatauzika vizuri huku nje bila tatzo???Kidogo Unaweza sema ni MEMBE but huyu MEMBE ana makando kando yake pia NA PIA si MEMBE tu wapo pia HAZINA KUBWA YA VIJANA kama MWIGULU..JANUARY na wengine but tukumbuke mpaka sasa HUYU RAIS aliyepo MADARAKANI tayari ana watiifu wake MWISHO wa siku ITATOKEA MIFARAKANO YA SISI WENYE KWA WENYEWE NA kuwafaidisha WAPINZANI....kupitia HILI HAKUNA MBUNGE WA CCM anaeweza kuruhusu huu UPUUZI hata kama ana mchukia JPM....sisi NDANI ya CCM tuna kauli ifuatayo 'CHAMA KWANZA MTU BAADAE"....
Na je kupitia upinzani ni nani hasa NI MSAFI zaidi ya MAGUFULI???....ni jibu ni hakuna hata kidogo maana so far UPINZANI unategemea wafuatao NI LOWASSA na LISSU...but kuna wafia chama kamwe hawamkubali MZEE hata kidogo na MZEE hayupo tayari kukaa pembeni kwenye SUALA LA URAIS....mwisho wa siku ni CHADEMA vipande vipande......
Ndio maana tunasema IMPEACHMENT KWA JPM NI NDOTO........sasa ebu mwacheni RAIS wetu atutumikie sisi tusiokuwa MAJIZI,,MAGAIDI,..WAVIVU..MAFISADI...TUSIOPENDA MAISHA YA MTEREMKO atutumikie tutamuhukumu 2020......

Hiyo ni ndoto!
 
Makomeo sio mchafu ni incompetent.
 
Fanya kazi kijana au tafuta hobby acha kupoteza muda na akili yako kwenye ambayo hauna uwezo wa kuyabadilisha, ndiyo maana Wanawake zenu wanawacheat!
 
One day your wish will be granted. Especially if we decide that we have had enough, and take actions. They might be temporarily painful but the result will be lasting. Hakuna atakae dhubutu kuchezea fedha na Haki za umma kiasi hiki tena.

"If we decide...." blah blah blah...you and who/whom????????????? Are you a Member of Parliament??? Au wewe ni mwananchi wa kawaida kama tulivyo wengi na ambao tunaona our President anafanya mazuri???? Kuna tatizo gani la msingi mpaka Rais aondolewe madarakani??? Mnafahamu sharia ya kum-impeach Rais inasemaje? Yaani you want to gang up to remove the President from power???!!!!! God forbid ....Mmepotea njia, hamna mwelekeo, hamna hoja....
 
Nawaza tu kwa MFANO hiki kinachosemwa ya KUWA bunge LIMEJIPANGA kumwondoa RAIS madarakani ni cha kweli na ikatokea imefanikiwa.....ni yapi yatakuwa ni madhara kupitia CCM...
Hopefully tutafanya UCHAGUZI mkuu....sasa hofu yangu juu ya hili LA KUMWONDOA RAIS NI NDOTO na halitokujafanikiwa KAMWE ni hii...
Ni nani hasa ni MBADALA WA MAGUFULI ndani ya CCM???.....na ambae hatauzika vizuri huku nje bila tatzo???Kidogo Unaweza sema ni MEMBE but huyu MEMBE ana makando kando yake pia NA PIA si MEMBE tu wapo pia HAZINA KUBWA YA VIJANA kama MWIGULU..JANUARY na wengine but tukumbuke mpaka sasa HUYU RAIS aliyepo MADARAKANI tayari ana watiifu wake MWISHO wa siku ITATOKEA MIFARAKANO YA SISI WENYE KWA WENYEWE NA kuwafaidisha WAPINZANI....kupitia HILI HAKUNA MBUNGE WA CCM anaeweza kuruhusu huu UPUUZI hata kama ana mchukia JPM....sisi NDANI ya CCM tuna kauli ifuatayo 'CHAMA KWANZA MTU BAADAE"....
Na je kupitia upinzani ni nani hasa NI MSAFI zaidi ya MAGUFULI???....ni jibu ni hakuna hata kidogo maana so far UPINZANI unategemea wafuatao NI LOWASSA na LISSU...but kuna wafia chama kamwe hawamkubali MZEE hata kidogo na MZEE hayupo tayari kukaa pembeni kwenye SUALA LA URAIS....mwisho wa siku ni CHADEMA vipande vipande......
Ndio maana tunasema IMPEACHMENT KWA JPM NI NDOTO........sasa ebu mwacheni RAIS wetu atutumikie sisi tusiokuwa MAJIZI,,MAGAIDI,..WAVIVU..MAFISADI...TUSIOPENDA MAISHA YA MTEREMKO atutumikie tutamuhukumu 2020......
Mkuu hoja yako ungeiweka hivi : baada ya kumng'oa JPM itabidi ufanyike uchaguzi mkuu. Swali ni je, JPM anazuilika kurejea ktk kiti chake?

Ndani ya ccm
Yeye ndiye m/kiti hata baada ya impeachment ataendelea kuwa m/kiti. Hivyo atatumia rungu la uenyekiti kupitishwa kuwa mgombea wa ccm.

Nje ya ccm (serikalini)
Jpm ameteua watu wake kila ngazi ya serikali wakiwemo wakurugenzi wa wilaya. Hawa ndiyo wasimamizi wakuu wa uchaguzi ktk wilaya zao. hawata tafuta namna ya kumtetea bosi wao?

Tume ya uchaguzi
Hii imewekwa na yeye.

Kwa maelezo hayo sioni namna ya kumzuia jpm kurejea kwenye nafasi yake
 
"If we decide...." blah blah blah...you and who/whom????????????? Are you a Member of Parliament??? Au wewe ni mwananchi wa kawaida kama tulivyo wengi na ambao tunaona our President anafanya mazuri???? Kuna tatizo gani la msingi mpaka Rais aondolewe madarakani??? Mnafahamu sharia ya kum-impeach Rais inasemaje? Yaani you want to gang up to remove the President from power???!!!!! God forbid ....Mmepotea njia, hamna mwelekeo, hamna hoja....
Acha kutisha watu wewe
 
Utaratibu wa kumshughulikia ukishaanza tu, Rais hana mamlaka tena ya kuchukua hatua kwa sababu tayari atakuwa benchi akisubiri hatma yake. Mathalani Baraza la mawaziri likishatoa ripoti kwa Jaji Mkuu na uchunguzi ukaanza Rais hana madaraka tena mpaka itakapothibishwa tofauti. Vivyo hivyo, Bunge likishaanza inayoitwa process ya kum-impeach, hawezi kuwa tena na mamlaka ya kulivunja Bunge.

Huo ndio utaratibu wa kawaida kwa mtuhumiwa yeyote yule...isipokuwa kwa Daud Albert Bashite kipenzi cha mkulu.
 
HATUA 12 ZA BUNGE KUMUONDOA RAIS MADARAKANI.

SEHEMU YA I: UTANGULIZI.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kisheria na kikatiba lina mamlaka ya kumuondoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania madarakani. Bunge linapata uwezo wa kumuondoa rais madarakani katika masharti yaliyowekwa na Ibara ya 46 A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ikisomeka pamoja na masharti yaliyowekwa na Sheria ya Kinga, Madaraka na haki za Bunge, 1988 (The Parliamentary Immunities, Powers, Privileges Act, 1988) na Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016. Zipo takrinani hatua 12 katika mchakato wa bunge kumuondoa rais madarakani na kabla ya kuangalia hatua tajwa,yatupasa kuangalia maswala muhimu saba (7) tunayopashwa kuyafahamu katika mchakato huu.

SWALA LA KWANZA,
iwapo bunge litaanzisha mchakato wa kumshtaki rais basi rais anapoteza uwezo wa kuvunja bunge kwa maneno mengine rais hana uwezo wa kuvunja bunge mara baada ya mchakato wa kumshtaki kuanza na mchakato wa kumshita rais unachukuliwa kuwa umeanza baada ya spika kupokea taarifa rasmi kutoka kwa mbunge iliyosainiwa na asilimia 20 ya wabunge wote yenye nia ya kumshita rais na hii ni kwa mujibu wa Ibara ya 90 (2) (a) ya Katiba na Kanuni ya 125 (1) (b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016.

SWALA LA PILI,
Ibara ya 46 A (2) Katiba iweweka sababu tatu zinazolipatia bunge uwezo wa kumuondoa rais madarakani kama ifuatavyo; (1) Iwapo rais atavunja katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; (2) Iwapo rais atakiuka maadili ya uandikishwaji wa vyama vya siasa (3) Iwapo rais amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano. Iwapo sababu mojawapo au zote zitajitokeza basi bunge linaweza kuanzisha mchakato wa kumuondoa rais madarakani unaoitwa “Kumshitaki rais” ambapo mwisho wa mchakato huo ni bunge kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani kutokana na hoja ya kumshtaki rais iliyowasilishwa na mbunge siku 30 kabla ya siku ya kikao cha bunge ambacho hoja ya kumshtaki rais itatolewa bungeni. Bunge halina uwezo wa kumuondoa rais nje ya sababu 3 zilizotajwa hapo juu, hatahivyo sababu zenyewe ni pana sana kuweza kuhusisha mambo mengi.

SWALA LA TATU,
Inabidi izingatiwe kwamba endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashataka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge. Hii inamaanisha kuwa rais atapoteza haki na kinga zote za kisheria na kikatiba ikiwemo kinga ya kutoshtakiwa mahakamani kwa makosa aliyofanya akiwa katika wadhifa wa rais, hivyo basi, baada ya kuondoka madarakani anaweza kupelekwa mahakamani na akikutwa na hatia ya kosa la jina atakwenda gerezani kama raia wengine wote. [Ibira ya 46 A (11) ya Katiba na [Kanuni ya 129 (4) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

SWALA LA NNE,
kura kwa ajiri ya uamuzi wowote utakaofanywa na bunge katika hatua yoyote ya mchakato wa kumuondoa rais madarakani ni lazima kura hizo zipigwe kwa “SIRI” ikiwa pamoja na kura kwa ajiri ya kufanya uamuzi wa kuundwa Kamati Maalum ya Uchunguzi na kura ya kupitisha azimio la kudhibitisha mashtaka ya rais na kupitisha azimio la kumuondoa rais madarakani na hili ni kwa mujibu wa Kanuni ya 125 (3) na 129 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016.

SWALA LA TANO,
ili kuanzisha mchakato wa kumuondoa rais madarakani wanaitajika asilimia 20% ya wabunge wote wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii ni kwa mujibu wa Ibira ya 46 A (3) (a) ya Katiba na Kanuni ya 125 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016. Bunge kwa sasa lina jumla ya wabunge 390, hivyo asilimia 20% ya wabunge wote ni wabunge 78 tu. Hivyo basi kunaitajika saini za wabunge 78 kuanzisha mchakato wa kumuondoa rais madarakani.

SWALA LA SITA,
ili bunge kudhibitisha mashtaka ya rais na kumuondoa madarakani inaitajika mbili ya tatu (2/3) au asilimia takribani 67% ya wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupiga kura kuunga mkono hoja na hii ni kwa mujibu wa Ibira ya 46 A (9) ya Katiba na Kanuni ya 125 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016. Bunge kwa sasa lina jumla ya wabunge 390, hivyo mbili ya tatu au asilimia 67% ya wabunge wote ni wabunge 262 tu. Hivyo basi kunaitajika kura za wabunge 262 kumuondoa rais madarakani.

SWALA LA SABA,
iwapo bunge litamuondoa rais madarakani, Bunge litaendelea kuwepo na wabunge wataendelea na wadhifa wao wa ubunge mpaka 2020 au litakapovunjwa kwa mujibu wa Ibara ya 90 (2) ya Katiba na sio kwa sababu ya kumuondoa rais madarakani. Pia ni muhimu kuzingatia kuwa iwapo rais atavunja bunge pia na rais anapoteza nafasi ya urais na nchi inaenda kwenye uchaguzi mkuu wa rais na wabunge lakini bunge likimuondoa rais madarakani bunge linaendelea kuwepo na wabunge wake wanasaria madarakani.

Madaraka ya rais kulivunja bunge yamewekewa mipaka, rais anaweza kuvunja bunge kutoka na sababu tano (5) tu kwa mujibu wa Ibara ya 90 (2) ya Katiba na sivinginevyo na sababu hizo tano (5) ni kama ifuatavyo.

(i) kama Bunge limemaliza muda wa uhai wake wa miaka mitano (5);
(ii) kama Bunge limekataa kupitisha Bajeti iliyopendekezwa na Serikali;
(iii) kama Bunge limekataa kupitisha Muswada wa sheria;
(iv) kama Bunge limekataa kupitisha hoja ambayo ni ya msingi katika sera za Serikali na
(v) Iwapo chama tawala kina idadi ndogo sana ya wabunge kiasi cha serikali kupoteza uhalali wa kuendelea kutawala nchi.

SEHEMU YA II: UTARATIBU WA KUMUONDOA RAIS MADARAKANI.

Mchakato wa bunge kumshtaki rais kwa lengo la kumuondoa madarakani unafuata utaratibu ufuatao;

HATUA YA 1,
Kuwasilisha taarifa ya mashtaka kwa spika wa bunge. Taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini (20%) ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekezwa kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashataka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais. Bunge kwa sasa lina jumla ya wabunge 390, hivyo asilimia 20% ya wabunge wote ni wabunge 78 tu. Hivyo basi kunaitajika saini za wabunge 78 kuanzisha mchakato wa kumuondoa rais madarakani. [ Ibira ya 46 A (3) (a)] ya Katiba na [Kanuni ya 125 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA YA 2,
mbunge mtoa hoja kuiwasilisha hoja ya kumshtaki rais mbele ya bunge. Wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo Bungeni. [Ibira ya 46 A (3) (b) ya Katiba na Kanuni ya 124 na 125 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA YA 3,
kupiga kura kwa ajiri ya uundwaji wa Kamati Maalum ya Uchunguzi. Baada ya hoja ya kumshtaki rais kutolewa, Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi. [ Ibira ya 46 A (3) (b)] ya Katiba na na Kanuni ya 124 na 126 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA YA 4,
uteuzi wa wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi. Iwapo hoja ya kumshtaki rais itaungwa mkono na Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, spika atateua na kutangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi [Ibira ya 46 A (3) (b) ya Katiba]. Wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi wanapashwa kuwa Jaji Mkuu ambaye ndiye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati, Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na Wajumbe saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa na akidi ya mkutano wowote wa Kamati Maalumu ya Uchunguzi itakuwa ni Mwenyekiti, Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar na Wajumbe wengine wanne kutoka Bungeni. [Ibira ya 46 A (4) (a), (b) na (c) ya Katiba na [Kanuni ya 127 (3), 126 (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA Y 5,
Rais kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atasimamishwa kazi ya urais na kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa na Makamu Rais mpaka pale Spika atakapomtarifu Rais kuwa kuwa Bunge limekataa kupitisha azimio la mashtaka dhidi yake. [Ibira ya 46 A (5) ya Katiba na Kanuni ya 126 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016

HATUA YA 6,
Kamati Maalum ya Uchuguzi kufanya uchunguzi na uchambuzi wa mashtaka dhidi ya rais. Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchuguzi kuundwa, itakaa ichunguze na kuchambua mashataka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge. [Ibira ya 46 A (5) ya Katiba na [Kanuni ya 127 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA YA 7,
Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilisha taarifa yake kwa Spika.Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.[Ibira ya 46 A (5) ya Katiba na Kanuni ya 127 (4) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA YA 8,
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilisha uamuzi wa kamati yake kwenye Kamati ya Bunge Zima. Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa kwenye Kamati ya Bunge Zima ambapo Mwenyekiti na mjumbe mwingine ambaye siyo Mbunge wa Kamati Maalumu
ya Uchunguzi atawasilisha na kuelezea uamuzi wa Kamati yake kwenye Kamati ya Bunge Zima.[Ibira ya 46 A (8)] ya Katiba na Kanuni ya 128 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016] .

HATUA YA 9,
Bunge kujadili taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi. Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa, Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza.[Ibira ya 46 A (9) ya Katiba na Kanuni ya 128 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016] .

HATUA YA 10,
Bunge kufanya uamuzi. Baada ya kusikiliza utetezi wa Rais, Bunge litafanya uamuzi iwapo mashtaka dhidi ya rais yamedhibitika au hayajadhibitika. Bunge litamuondoa rais madarakani kwa kupiga kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote kwa kupitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais vinginevyo rais ataendelea kushika wadhifa wake. Kura zitapigwa kwa siri. [Ibira ya 46 A (9) ya Katiba na Kanuni ya 129 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

HATUA YA 11,
Bunge kupitisha Azimio la kumwondoa Rais madarakani. Baada ya Kamati ya Bunge Zima kukamilisha kazi zake na Bunge kurudia, Mbunge aliyetoa hoja ya kumshtaki Rais atatoa taarifa ya kukamilika kwa shughuli za Kamati ya Bunge Zima na endapo mashtaka dhidi ya Rais yatakuwa yamethibitika, kwa kuungwa mkono na kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, papo hapo atatoa hoja kwamba, Bunge lipitishe Azimio la kumwondoa Rais madarakani, kwa mujibu wa masharti ya Ibara ya 46A (5) ya Katiba. [Ibira ya 46 A (9) ya Katiba na Kanuni ya 129 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016]

HATUA YA 12,
Rais kuondoka madarakani. Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo. [Ibira ya 46 A (10)] ya Katiba na Kanuni ya 129 (3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2016].

SEHEMU III: HITIMISHO.

Huu ni ufupisho (summary) wa mchakato na utaratibu wa bunge kumshtaki rais kwa lengo la kumuondoa madarakani. Hili kupata uelewa wa kina wa swala hili ni vyema kusoma kanuni, sheria na katiba husika hususani ibara, vifungu na kanuni mahususi zilizotajwa kwenye andishi hili. Andishi hili ni mwanzo wa mfululizo wa maandiko nitakayokuwa ninaandika kama sehemu ya elimu ya katiba na sheria kwa umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuisaidia serikali kuwa na raia wanaojua sheria na katiba kwa lengo la kuwawezesha raia kutii na kuheshimu sheria na katiba bila shuruti ikiwemo kuheshimu mamlaka halali ya serikali, viongozi wa umma na watumishi wa umma. Elimu hii kwa umma ina lengo la kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais za kuboresha utawala wa sheria katika Jamhuri ya Muungano waTanzania.

Kutoka; Facebook Attorneys
 
Back
Top Bottom