Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,608
- 1,743
46A.-(1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshitaki rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.
(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba rais-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano.
------------------------------------------
Hicho kifungu C kinaweza kutumika kumuondoa Raisi madarakani.(2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba rais-
(a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;
(b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba au
(c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano.
------------------------------------------
1) Akiwa nchini Ufaransa kwamba hajui umaskini wa Watanzania unatokana na nini.
Akiwa na waandishi wa nje aliamua kuwa wazi na kuwaambia kwamba hata yeye hajui umaskini wa nchi yetu unasababishwa na nini.
Tafsiri yake ni kwamba wakati anagombea urais aliwadanganya Watanzania alipowaambia ataleta neema na maisha bora kwa kila Mtanzania.
2 ) Aliporejea nchini na kutimiza miaka miwili Ikulu, aliwaambia waandishi wa nchini kwamba ahadi zote atazitimiza (ikiwamo ya maisha bora kwa kila Mtanzania, ambayo hajui sababu ya kwa nini Watanzania hawana hayo maisha bora na hivyo kuwa maskini). Huku ndiko kudhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakokataliwa na katiba.
3 ) Rais akilihutubia Bunge Desemba 30 mwaka 2005 alisema: Serikali ya Awamu ya Nne itaendeleza vita dhidi ya umaskini, ujinga na maradhi, tena kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. - Ataendeleza vipi vita wakati haelewi adui umasikini anakujakujaje.
Nimeshangaa kuona kwamba hata pesa ya Rwanda na Burundi, nchi zilizokuwa na vita miaka mingi, ina thamani kuliko shilingi ya Tanzania. Amani tunayodai kuilinda kwa kila hali ni ya nini? Inatusaidia nini?
Kama nchi zinazopigana vita ya wenywe kwa wenyewe baada ya vita watawala wanakuwa na adabu na kuwatumikia wananchi sawa sawa, basi na sisi tupigane.
Baadhi yetu tufe kama kafara ili tuokoe maisha ya vizazi vijavyo, vinginevyo kwa ari hii, nguvu hii na kasi hii, Tanzania ijayo itakuwa maskini sawa na jalala na Watanzania wa kizazi kijacho watakuwa maskini sawa na vichaa na chokoraa wanaokula majalalani.
3 ) Mimi sitembei na fuko la pesa -Kiti Cha Urais kimedhalilishwa
4 ) Anasema serikali hii yenye kitivo cha sheria cha kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki, haina wataalamu wa kujua hilo! Hii ni aibu na kwa kweli kwa mkuu wa nchi kuwatangazia mataifa ya nje kwamba nchi yake haina wanasheria wa kujua mambo madogo kama hayo ni kukidhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Na wanasheria wa nchi hii sijui kwa nini hawajajitokeza kupinga kauli hii ya rais iliyowadhalilisha sana!
Kama nchi zinazopigana vita ya wenywe kwa wenyewe baada ya vita watawala wanakuwa na adabu na kuwatumikia wananchi sawa sawa, basi na sisi tupigane.
Source : Kalamu ya MWIGAMBA