gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,274
- 20,673
Mleta mada anaulizia zile dalili za awali kabisa kuwa umepata VVU kabla hata ya CD4 kushuka.Niseme kwa ile miezi ya awali kabisa kabla hata ya magonjwa nyemelezi. Kumbuka magonjwa nyemelezi huanza pale CD4 zinaposhuka!!! Na ukumbuke kuwa kama unakula vizuri CD4 zako zinaweza kudumu hata miaka kumi bila kuonesha dalili kabisa ya ukimwi. Cha msingi kwa wale ambao say jana walipata maambukizi je kuna dalili yoyote atakuwa nayo katika mwili wake hasa katika ku-adopt kuwahifadhi foreign agent katika mwili sasa? Maana wanaingia, sidhani kama wanaingia kimya kimya na wakishaingia wanajiweka sawa wanatulia wanaanza kuzaliana na kushambulia kinga ndiyo CD4 zinahusika sasa. Tafadhali wenye uelewa wa mambo haya hebu wasaidie.
HIV hushambulia seli nyingi sana mwilini soon baada ya mtu kupata infection lkn target yake kubwa ni T cells ambayo hujulikana kama CD4 LYMPHOCYTE ama CD4.
HIV huingia mwilini na kwenda kwenye dendritic cells ambapo husafirishwa hadi maeneo ya matukio kwaajili ya kuzaliana. Virus huyu huzaliana kwa hatua zifuatazo, nazo ni binding and fusion, reverse transcription, transcription na mwisho assembly. Budding ndiyo stage ya mwisho kabisa na toka hapo hapo virus huyu huwa amesha tengeneza seli nyingi na hivyo sasa hutoka na kuanza kushambulia seli nyingine mwilini.
mpaka wakati huu mhusika hawez kuwa na dalili yyte ile na wala hatajiskia kama ni mgonjwa. Mtu huanza kujiskia kuwa na tatizo soon baada ya CD4 kupungua na hivyo magonjwa hata yasiyokuwa na sababu hujitokeza.
dalili ya kwanza kwa alio wengi ambayo nimeona mie ni kwa ngozi kupoteza ubora wake na hapo mtu hupata harara ndogo ndogo sana kama vile vijipele vya joto. hii ni dalili ya kuwa tayari CD4 zimeshaanza kupungua hata kama huumwi chochote na unawez kutumia dawa vikapoa lkn vikajirudia tena.