Kwa mshahara wa Tsh. 765,000/= nikizama benki naweza kopesheka kiasi gani?

Kupitia hiyo salary jibane Sana u save mil 1 then anzisha biashara ya kuwakopa walimu wenzako laki moja kwa elfu 20 na laki mbili 40 Ila ukiwa na muda wekeza katika biashara ya mazao kuwa middle broker .

Katika hizo biashara zako ukiona zinaenda vizuri basi kachukue mkopo bank ambao sio mkubwa na ambao hautaathiri mshahara wako Sana. Then bust biashara yako.

Kuhusu kujenga usijenge kipindi hiki ambacho haujawa na financial freedom , bali anza kujenga kipindi ambacho utakuwa unaingiza hela kila siku. Ila waweza Ku-invest katika viwanja tu.
 
Mimi nina mshahara kama huyo jamaa ninaishi,niko kwangu,nina nyumba mbili, Sijawahi kulala njaa, mwaka huu january napeleka mtoto wangu English medium school,karo 2M,mwaka jana ndani ya miezi miwili nimekamilisha nyumba ya 13M.

Take home yangu ni 270K

Acha kuogopesha watu, jamaa kama anajiweza akope
Unaishi Tanga!?

manake huko kuna nyumba mpaka za laki tano
 
Mnaomshauri akope 25M
Mwambieni pia atalipa 47,318,177.1(47M),
Mwambieni katika hio 25M cash atakayopata ni 22.5M.
Mwambieni atakatwa 438,131.27 kila mwezi kwa miaka 9.
Mwambieni jumla ya riba atakayolipa ni
22,318,177.1.
Mwambie katika 47M atakayolipa,
Yeye atachukua 22.2M na 24.5M anawaachia Bank.
Mwambieni ni sawa kutoa 226,851 kila mwezi kwa miaka 9 kulipa riba tuu.
Mwambie hio pesa Akiamua kujitunzia mwenyewe angetumia miaka 4 kuipata, huku ⅓ ikibaki pale pale.

Akili Kukichwa.
 
Kupitia hiyo salary jibane Sana u save mil 1 then anzisha biashara ya kuwakopa walimu wenzako laki moja kwa elfu 20 na laki mbili 40 Ila ukiwa na muda wekeza katika biashara ya mazao kuwa middle broker .

Katika hizo biashara zako ukiona zinaenda vizuri basi kachukue mkopo bank ambao sio mkubwa na ambao hautaathiri mshahara wako Sana. Then bust biashara yako.

Kuhusu kujenga usijenge kipindi hiki ambacho haujawa na financial freedom , bali anza kujenga kipindi ambacho utakuwa unaingiza hela kila siku. Ila waweza Ku-invest katika viwanja tu.
noted champ, japo sina access na maticha
 
Mimi nina mshahara kama huyo jamaa ninaishi,niko kwangu,nina nyumba mbili, Sijawahi kulala njaa, mwaka huu january napeleka mtoto wangu English medium school,karo 2M,mwaka jana ndani ya miezi miwili nimekamilisha nyumba ya 13M.

Take home yangu ni 270K

Acha kuogopesha watu, jamaa kama anajiweza akope
270k kwa mwezi? Unaweza kutufunza vionjo vya bajeti yako ya siku?
 
Usimdanganye mwenzio. Sababu yake kuu ya kukopa ni NJAA, kasema mwenyewe.
Anataka akope mkopo wa juu zaidi kuweza kukopeshwa kwa sababu ana njaa.

Mtumishi unatakiwa ukope ukiwa na biashara au mradi wako ambao umefanya kwa hela za kudunduliza au hela ya kupata kwenye chanzo kingine ila sio mkopo wa riba. Ufanye kwa muda hata zaidi ya mwaka, uanze kupata faida na hasara uzoee hicho kitu, ukue uache kutumia hadithi na simulizi badala yake utumie uhalisia na uzoefu.
Baada ya hapo ukope ili kuendeleza na kukuza hiyo shughuli. Tena napo haukopi mkopo wa kiasi cha juu kabisa kinachowezekana.

Anza kufuga mbuzi au nguruwe, anza kununua mazao kwenye msimu, anzisha biashara ya miche ya miti na matunda, anzisha duka la spare parts au nguo au viatu au vyombo vya ndani, etc. Fanya kwa muda fulani mpaka uwe na uzoefu kisha ndio ukope benki kuanzia kiasi kidogo na unapanda taratibu.
Miaka kadhaa baadae utakuwa na uwezo wa kukopa hata 70M bila wasiwasi. Sio unapigwa njaa unakopa kujimaliza ili ununue sabufa na pikipiki used ya Sanya, na TV ya Aborder ukutani, hela inayobaki ukarabati nyumba.

mkarimani feki dunia sio mama yako, miaka minne ijayo hakuna atakayekuhurumia leo hii ukikopa kisa una njaa.
Asome vizuri kisha akuelewe
 
Asikope kwasababu ana idea ya biashara .....hapa ndipo watu wengi wanapofeli katika mikopo.Kopa ili kuikuza au kuitanua biashara ambayo tayari unaendelea kuifanya, inakulipa vizuri na una uwezo wa kuzikabili changamoto zake.

Unakopa ili kuongeza uzalishaji au uingizaji wa bidhaa sokoni. Usikope ili kuanzisha biashara utakuja kukutwa na kitu kizito hutoamini.

Mfano labda ulikuwa unaingiza mzigo mchache unauzika kwa wakati na bado kuna demand kubwa ya uhitaji wa bidhaa yako kwa wateja. Hapa unaweza kukopa ili uwe na uwezo wa kuingiza mzigo mkubwa zaidi ili uongeze faida pia.

Ukifanya hivyo fasta utaweza kuulipa mkopo na utaona manufaa ya mkopo. Mwisho kabisa nakushauri uepukane na mikopo yenye Riba.

Kumbuka RIBA sio faida. Riba ni laana . Wengi wamefeli katika biashara kutokana na kujihusisha na mikopo yenye riba.
Mikopo mingi ina riba, ndio faida kwa hiyo kuepuka riba kwenye mikopo ni ngumu sana
 
Back
Top Bottom