Kwa mshahara huu, niwekee bajeti safi ya mwezi ilii niishi bila mikopo umiza

mkarimani feki

JF-Expert Member
Nov 8, 2023
302
1,136
Kwa takehome below 700k ,nifanyeje nisione dunia ni jehanamu wala kuwa ndugu, jamaa na marafiki kuhusu mikopo ama kuenda benki ambao riba zao ziko juu sana.

Wazoefu, wachumi na waatalamu niwekee mgawanyo wa bajeti safi ya mwezi ili niwe debt free.

Maana sukari iko juu, vyakula vikojuu, kodi nk
 
Jitengenezee formula ya matumizi. Mfano 20% saving, 60 % matumizi ya kila siku kama nauli, chakula etc, 10% dharura na iliyobakia 10% ziada mfano kusaidia wazee na vitu kama hivyo.

Punguza kununua vitu ambavyo ni ziada na visivyo lazima mfano nguo sijui viatu vipya kila wakati, kutoka out sijui dinner out, vifaa vya ndani ya nyumba ambavyo vitakugharimu sana, kusaidia sana watu hata kama nj ndugu zako, kunywa pombe sijui kila weekend, kubet etc.

In short ukiweza masta hiyo formula hapo juu utakua unaishi kibahili na hiyo hela itakutosha
 
noted chief
 
Kwanza jifunze kutumia kilichobaki baada ya kuweka akiba, ukipata pesa kwanza weka akiba inayobaki ndio utumie,,

Ili kuweka akiba kwanza uwe unakula nyumbani ikiwa hakuna umbali mkubwa , mfano unaweza toka nyumbani saa 1 mpaka saa1:45 unakuwa umefika kazini , kunywa chai yalo nyumbani kabisaaaa.

Nani yupo nyumbani na ana umri gani ? Ikiwa upo na mti mwenye miaka 20 na kuendelea hakikisha hawi tegemezi mtafutie shuguli ya kufanya ili aweze kukidhi mahitaji yake madogo madogo kama vocha nk,

Je una mke? Isome tabia ya mkeo ikiwi ni wale mama huruma acha kununua vitu ndani kuna wanawake ukinunua mchele wa mwezi mzima unga sembe ngano , sukali na bidhaa nyingine utakuta hata wiki 3 hazifiki amewapa majirani ndugu yaani ni hovy hovyo tu ukiwan amwanamke wa hivi tunasema mama huruma acha kununua vitu vingi, nunua vile vinavyohitajika tu, kam mkeo yipo vizuli, ninakushauli nunua frii kisha fanya hivi

Nunua nyama ka kilo 3 chemsha weka ktk contena tia ktk friza

Nunua maharage kilo 2 chemsha weka ktk contena nunua sukali hta kilo 5 nk ukimaliza hapa mpe mkeo 50 elfu yaani hapa unaweza kaa wiki 3 usiambiwe jambo lolote hii mm nimeitumia sana, ile 50 elfu atakuwa ananunua kama mboga za majani viungo akitaka kubadisha kam samaki nk

Lkn kabla haufanya haya hakikisha ww namkeo mnazungumza lugha mojaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom