Kwa mliopo Mufindi na kwingineko, nataka nijitose kwenye biashara ya mbao, naombenini ushauri na uzoefu

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,471
Wadau wa JF,

Mada hapo imeeleweka bila shaka. Nataka nijitose katika biashara ya mbao baada ya kuhisi itanilipa kwa maoni yangu. Nataka ninunue kutoka mikoa ya Njombe na Iringa na kuzisafirisha kuuza mkoani Dodoma ambapo kuna fursa kubwa ya ujenzi hivi sasa.

Ni mgeni katika biashara hii na hata mikoa tajwa ila maisha ndiyo haya haya. Sijui chochote juu ya biashara hii, sina gari la kusafirisha mbao hivyo nitakodi malori. Pia sijajua ikiwa unaandaa hela ununue magogo au mbao zilizotayarishwa na kusafirisha? Nikununua mashine za kuchana magogo mwenyewe na kuzisafirisha baada ya hapo? Njia ipi inalipa? Siamini katika ushirikina biasharani.

Naombeni maoni, ushauri na tahadhari.

Asanteni sana.
 
Una mtaji wa sh ngapi?

Hapo Dodoma una eneo la kufanyia biashara? Jipange vizuri kuna changamoto ya vibali pia.

Kwanza nasubiri kujua mtaji ulio nao.
 
Freed Freed,

Hii biashara ni nzuri ukiwa na mazingira mazuri ya kifedha, watu wa kukusaidia kupata mzigo wasio waroho, uwe na yard ya kushushia mzigo, wauzaji wazuri na mwisho aina ya mzigo unaotafutwa sokoni.

Fanya hivi;

1. Nenda Mafinga mwenyewe ili upite kwenye vile viwanda upate bei za mbao kwa size tofauti.
2. Uliza wanaochana mbao msitu wa serikali, wanaombaje vibali. Ukipata taarifa za vibali na upasuaji wake utaweza kuamua kununua au kupasua.
3. Sikushauri kupasua toka kwenye misitu ya watu binafsi kama unaanza. Kuna figisu nyingi sana, labda ukipata GRL.
4. Angalia treated na Non treated timbers.
5. Ukitoka Mafinga nenda soko la mbao Makambako kapate bei na taratibu.
6. Nenda soko la mbao Njombe mjini ili ulinganishe.
 
Una mtaji wa sh ngapi?
Hapo Dodoma una eneo la kufanyia biashara?
Jipange vizuri kuna changamoto ya vibali pia..

Kwanza nasubiri kujua mtaji ulio nao..
Milioni 20, sina eneo Dodoma, nikipata ushauri mzuri nitatafuta eneo.
 
Milioni 20, sina eneo Dodoma, nikipata ushauri mzuri nitatafuta eneo.

Tafuta kwanza kijiwe cha kufanyia hiyo biashara huko Dodoma uliko. Ulizia na bei ya mbao aina zote zinazouzwa. Mfano Pines (Treated na Untreated), Mlingoti, nk. Halafu utalinganisha na bei ya Mufindi.

Ukishapata nitafute ili nikuunganishe na wadau waaminifu ili upate mbao nzuri zilizochanwa kwenye misitu ya Sao hill ambayo ndiyo inayotoa mbao nzuri na zenye ubora. Na pia bei zao ni rafiki.

Milioni 20 ni nyingi sana kwa kuanzia. Usije ukaja kujaribu kuchana. Nunua mzigo na safirisha. Vibali vya maliasili, halmashauri na TRA pamoja na usafiri wala siyo changamoto kihivyo hasa ukiwa na mwenyeji.
 
Tahadhari na utapeli na udhulumishi katika biashara hii. Mbao watu wanaibiana,tapeliana,dhulumiana sana usije muamini mtu
 
Nilishakuona kila nachoandika unateseka na mm, nimesema ada .km ada jua nilikua chini ya wazaz!naijuia vilivyo uwanja wa hom ulikua unajaa mbao. Ameifanya sana baba as had leo anauza misitu yake!ha leo tuna banda mfu basihaya!

Usiteseke na usiyemjua!
Duh

Masikini umenionea bure dear, sikukuuliza kwa ubaya asee..

So sorry kama nimekukwaza
 
Huwa naikubali sana michango yake kwenye nyuzi za biashara na ujasiriamali, ila hapo kwenye kufanya kila biashara huwa nafikiria labda ni fictions

Anyways, tuchukue yanayotusaidia tu.

😅😅watesekaji ni wengi. Wapi nimesema nimewah ifanya hii biashara mkuu.?hebu andika biashara 6 nizilizowahi sema nimefanya!

Jamani kuna umri hata wa kuleta habari za fictions!

Kifupi wazaz wangu wlikua waajiriwa, so na wajasiriamali wanaufanya had uzee wao. Ukiniona siku nyingine nacoment kuhusu ufugaji wa ngombe pia usishangae pia mkuu!najua abc zoote! Kwenye kilimo ndo kabisa hom ni familia ya kulima!mzee kasomea haya mambo na kwenye miti ukinikuta usije sema huy anafanya na hii?

Nop ni biashara za hom !yaan nipoteze muda kuandika fictions nipate nn?ili iweje.unahis napata relief yeyote maishani!? Kumuwish tu mtu all the best (as nina idea na mbao) bas imekuwa nongwa!jamani nipumzisheni basi!
Muwe mnacment nyie msiokuwa na fictions, ukiniona nina fictions niache!
 
Tafuta kwanza kijiwe cha kufanyia hiyo biashara huko Dodoma uliko. Ulizia na bei ya mbao aina zote zinazouzwa. Mfano Pines (Treated na Untreated), Mlingoti, nk. Halafu utalinganisha na bei ya Mufindi.

Ukishapata nitafute ili nikuunganishe na wadau waaminifu ili upate mbao nzuri zilizochanwa kwenye misitu ya Sao hill ambayo ndiyo inayotoa mbao nzuri na zenye ubora. Na pia bei zao ni rafiki.

Milioni 20 ni nyingi sana kwa kuanzia. Usije ukaja kujaribu kuchana. Nunua mzigo na safirisha. Vibali vya maliasili, halmashauri na TRA pamoja na usafiri wala siyo changamoto kihivyo hasa ukiwa na mwenyeji.
Asante sana kwa wazo lako zuri na ushauri mzuri. Wengine waliniogopesha kidogo
 
Back
Top Bottom