Naombeni ushauri biashara ya kuchana na kusafisha mbao

JMF

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
1,735
2,686
Salaam wana JF,

Naombeni ushauri wa biashara ya kuchana, kusafisha na kuchoronga mbao kwa hapa Dar. Kuna eneo langu lipo center nzuri ya makazi mapya na kutokana na kukosekana kwa kiwanda karibu au mashine za kuchana(kuzalisha) mbao, kusafisha na ku choronga, nikapata wazo la kuanzisha mradi huo.

Hivyo naombeni mawili matatu toka kwa wazoefu na wanaoijua biashara hii. Ningependa kujua mtaji hasa bei za mashine, changamoto zake, faida na namna bora ya kuiendesha biashara hiyo. Pia ushauri mwingine ambao unaendana na wazo langu nitaupokea.

NB: Eneo la wazi ninalo na lipo barabarani, umeme wa kamba mbili(ule wa majumbani) upo hapo hapo.

Asanteni.
 
Wasiliana na mimi kwenye whatsapp no.
00971527369138, tubadilishe mawazo, niliwahi kuwa na kiwanda cha furniture miaka mitano nyuma
 
Back
Top Bottom