Kwa mliokaa Ulaya/Marekani hivi Wazungu na wao pia huchagua majina ya ubatizo kanisani?

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,321
Naomba kujua kwa mliowahi kukaa ulaya huko, je ikifika wakati wa ubatizo, wazungu pia huchagua majina ya kubatizwa kwa watoto wao kama tunavyofanya huku Afrika?

Huku Afrika ni kawaida kukuta mtu ana majina mawili, moja la nyumbani lingine la ubatizo na la ubatizo lazima liwe la kizungu ama kiarabu. Huwezi kukuta mtu anaitwa maduhu halafu akachagu jina la kubatizwa la Kimaro ama Masawe.

Sasa naomba kufahamu kwa wale ambao mmeishi huko mkajua tamaduni zao, je na wao watoto wao huchagua majina ya jamii nyingine kubatizwa?
 
Bongo hapahapa tunaruhusiwa kubatiza kwa majina yoyote yale.

Siyo lazima ya kizungu au kiarabu inategemea na viongozi wa kanisa unalosali au analobatiziwa mtoto. Kama kuna viongozi waliojawa na utumwa wa fikra watakulazimisha majina ya kigeni hayo.

Mimi nimebatiza mtoto kwa jina kama la kiswahili tu japo ni la kiyahudi, halipo kwenye Biblia na linaandikwa kwa kiswahili tu.
 
Kwani wewe ni myahudi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiyahudi ni lugha tu kama Kisukuma, Kiingereza, Kichaga, Kipare, Kimakua, kimwera, Kinyaturu,Kinyakyusa, Kimakonde au Kidigo.
Jina nililochagua nilitaka liwe fupi litamkike (sound) kama kiswahili, liwe na maana njema yenye baraka kwa mtu niliyempa.

Kwa kiswahili lingetumia maneno matatu lingekuwa refu ila kiyahudi ni neno moja tu lenye maana sawa na sentensi ndefu ya kiswahili.

Pia nilitaka lifanane na herufi ya kwanza ya jina langu.
 
Bongo hapahapa tunaruhusiwa kubatiza kwa majina yoyote yale...
Kuna mapadri wa ajabu sana...

Wenyewe tukaenda kubatiza mtoto, kuulizwa jina tukataja Clayton(mfano)

Basi akaendelea...
Nakubatiza Clayton Paulo kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu. Kha! tukabaki kushangaa na ndo ishatoka hiyo 🤣🤣😅😅

Yaani kaongeza jina la Paulo mbele ya jina tulilolitaja sisi.
 
Kuna mapadri wa ajabu sana...
Wenyewe tukaenda kubatiza mtoto, kuulizwa jina tukataja Clayton(mfano)

Basi akaendelea...
Nakubatiza Clayton Paulo kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu 🤣🤣😅😅

Yaani kaongeza jina la Paulo mbele ya jina tulilolitaja sisi.

Kuna mapadri wa ajabu sana...

Wenyewe tukaenda kubatiza mtoto, kuulizwa jina tukataja Clayton(mfano)

Basi akaendelea...
Nakubatiza Clayton Paulo kwa jina la baba na la mwana na la roho mtakatifu. Kha! tukabaki kushangaa na ndo ishatoka hiyo 🤣🤣😅😅

Yaani kaongeza jina la Paulo mbele ya jina tulilolitaja sisi.
Jina pekee zuri ni lile la kwenye cheti cha kuzaliwa na haya mengine ni ziada na laana tu.
 
La kwenye cheti cha kuzaliwa ndo hilo hilo la ubatizo. Ukichanganya majina kwenye vyeti itakuletea usumbufu kuhakiki majina yako pale utakapotakiwa kufanya hivyo kwa kutumia vyeti/vitambulisho.

Pia watu wanaweza kuandika majina yote mawili kwenye cheti cha kuzaliwa. Inafanyika sana
 
Back
Top Bottom