badoo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 512
- 248
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ilichangia gharama za kuendesha serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitatu tu tangu 1965 - 1967 kwa asilimia kati ya 5 - 11.
Kwa mantiki hiyo Zanzibar inabebwa na Muungano! Hivyo gharama za mambo ya nje, jeshi, polisi, usalama wa taifa nk zinabebwa na Watanganyika.
Hivyo vyombo vyote hivyo ni mali ya Watanganyika! Zanzibar hawana chao!
Kwa muktadha huo endapo tutaunda serikali tatu, ni serikali ya Tanganyika itakayoumia. Au kwa maneno mengine ni Kodi za Watanganyika zitakazotumika.
Endapo muungano utavunjika rasilimali zote za jeshi, polisi, usalama wa taifa nk itabidi zirudishwe Tanganyika. Zanzibar itabaki bila jeshi, polisi wala usalama wa taifa nk. Usalama wa taifa la Zanzibar utakuwa mashakani.
Ni vema Wazanzibari wakaanza kujitafakari hivi sasa! Kuna hatari kubwa ipo mbele yao!
Zanzibar tafakari kabla hamjaamua! Heri kinga kuliko tiba!
Km umetumwa udanganye umma hapa utawapata wasiojua km wewe,sisi tulokuwepo ktk system tunaujua ukweli tena uliyoyasema ni unafiki,zanzibar inachangangi na haifaidiki chochote,mwisho mwezi julai mwaka jana zanzibar ilichangia kiasi cha asilimia iliyotakiwa kuchangia,na ukae ukijua kuwa uanzishwaji wa BOT zanzibar iliwekeza pesa nyingi zaidi kuliko sisi watanganyika,msitake kuwafanya wazanzibar hawawezi kujiendesha kiuchumi nyinyi mlowepo nje hamuwezi kuyajua ya ndani mnapiga kelele na kudanganywa tu,wa bara hatutaki kuwa wawazi kuwa wazanzibar ktk kuanzisha BOT WANA HISA KUBWA KULIKO BARA,nakushangaa mtoa mada kwa unafiki wako nadhani wewe ndio kwanza unaijua tanzania baada ya kuja dar es salaam.